Kiwanja kinatunza hela vizuri zaidi kama hela yako ni ndogo, sababu ni hii,ukishanunua utakuwa na uhakika kuwa kiwanja kipo kina hela yangu kiasi kadhaa na huku ikiongezeka kama umenunua sehemu salama. Siku ukipata plan sahihi na unahitaji hela, waweza kukiuza na kujazia pale kwenye kiasi ulicho nacho mkononi, na pengine kiwanja hicho chaweza zaa kiwanja kingine huko mbele.
Taabu za kuweka mtaji mdogo ktk ardhi ni kwamba itabidi uanze moja tena kudunduliza, inachukua muda. Kukaa na hela mkononi ni risk zaidi, kupeleka benki ndio unaimaliza kabisa. Kama uko vizuri ktk mazingira yako, bora uzungushe zaidi ili ikupe uwezo mkubwa wa kuizalisha.