Ushauri sahihi Ni upi? Na ushauri kutoka kwa Mtume Mwamposa

Third eye judge

Senior Member
Aug 9, 2016
133
119
Ushauri sahihi Ni upi ??. Na ushauri kutoka kwa Mtume Mwamposa.

Je mtaji yafaa kuingizwa kwenye biashara au kujenga nyumba ya kuishi ?

Hii inawahusu zaidi waajiriwa.

Mtume na Mchungaji Boniphace Mwamposa Bulldozer alipokuwa akiongea na wafanyabiashara na wafanyakazi katika Madhabahu ya Arise and Shine Kawe Dsm, alizungumza jambo ambalo wengi hupata utata katika kujua kipi Ni sahihi zaidi.

Mtume Mwamposa alisema kuwa hashauri mfanyakazi kuchukua hela ya mkopo na kwenda kuitumia kwaajili ya kujenga nyumba ya kuishi, badala yake yafaa hela hiyo aiingize kwenye biashara, izalishe, na kisha fedha inayotoka katika biashara aliyoianzisha ndio aitumie kujengea nyumba ya kuishi.

Aliendelea na kusema kuwa hata yeye angeamua kujenga nyumba ya kuishi nyumbani kwao lakini aliona Ni bora zaidi kujenga kwanza hoteli izalishe fedha kwanza.

Swali hili limekuwa Ni gumu kwa wengi juu ya uamuzi sahihi kuhusu kipi kianze. Je maoni yako Kama mdau unasemaje juu ya hili ?
 
Bora kujenga nyumba, biashara haina uhakika, ukishindwa rejesho utaenda ikopea hiyo nyumba bank nyingine ili ulipe hilo deni la awali.

Pia usikope hela ukaanzisha biashara ambayo hautaisimamia wewe, utalizwa na hautaamini macho yako.
Inategemea umeipata wapi hiyo Hela.kama ni sadaka kutoka kwa watu unaweza amua kufanya chochote.Ila watu siyo wajinga,kila mtu anamipango yake.siyo kila mtu anaweza kufanya biashara
 
Binafsi nasimama na mchungaji ila kama Biashara unaenda isimamia mwenyewe kwa asilimia 99 fanyia Biashara ila kama hauisimamii jenga aisee....
Zakuambiwa changanya na zako
 
Ndio maana 'business plan' huwa ni muhimu sana mtu kuwa nayo kabla ya kuanza biashara.
Wote unao waona wenye viwanda, pesa imetoka 'bank'/mkopo; na wakati mwingine kiwanda hicho hicho kinachojengwa hutumika kama dhamana.

Kama 'business plan' yako iko vizuri; anza na kitu kitakachokuletea pesa
 
Ushauri sahihi Ni upi ??. Na ushauri kutoka kwa Mtume Mwamposa.

Je mtaji yafaa kuingizwa kwenye biashara au kujenga nyumba ya kuishi ?

Hii inawahusu zaidi waajiriwa.

Mtume na Mchungaji Boniphace Mwamposa Bulldozer alipokuwa akiongea na wafanyabiashara na wafanyakazi katika Madhabahu ya Arise and Shine Kawe Dsm, alizungumza jambo ambalo wengi hupata utata katika kujua kipi Ni sahihi zaidi.

Mtume Mwamposa alisema kuwa hashauri mfanyakazi kuchukua hela ya mkopo na kwenda kuitumia kwaajili ya kujenga nyumba ya kuishi, badala yake yafaa hela hiyo aiingize kwenye biashara, izalishe, na kisha fedha inayotoka katika biashara aliyoianzisha ndio aitumie kujengea nyumba ya kuishi.

Aliendelea na kusema kuwa hata yeye angeamua kujenga nyumba ya kuishi nyumbani kwao lakini aliona Ni bora zaidi kujenga kwanza hoteli izalishe fedha kwanza.

Swali hili limekuwa Ni gumu kwa wengi juu ya uamuzi sahihi kuhusu kipi kianze. Je maoni yako Kama mdau unasemaje juu ya hili ?
Yupo sahihi kabisa, pesa inahitaji kuwa kwenye mzunguko ndio maana inaitwa currency. Ukijenga nyumba ya wewe kuishi umeipaki pesa.
 
Back
Top Bottom