Uamsho - Akutendae mtende, mche asiyekutenda

Mkandara

Platinum Member
Joined
Mar 3, 2006
Posts
15,998
Reaction score
9,434
Namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma aliye nijalia kwa rehma zake mfungo wa Ramadhan salama salimin. ALHAMDULILLAH.

Hoja yangu ya leo ni UAMSHO kwa ndugu zangu waafrika juu ya nadharia ya Uchumi kuwa NI elimu ya juu ya mfumo bora wa maendeleo ya watu na nchi zote duniani. Mfumo mmoja kandamizi kwa wote. Labda nusjereheshe hapa chini..

Hoja yangu inahusu Elimu hii ya Uchumi ambayo kwanza inatudhalilisha sana sisi Waafrika kama kwamba sisi hatuwezi kufikiri nje ya mfumo huo isipokuwa kwa mapokezi ya mafundisho ya Wakoloni walotutawala na wakafaidika na rasilimali zetu kwa njia za udanganyifu wa mapambo ya wadhifa ya Uhuru wa bendera.

Hivi leo tunapodai tupo huru, uhuru huo tunao kweli ikiwa bado tunatumia Elimu ya Uchumi wa Ukoloni Mambo leo? Tofauti gani iliyopo na Ukoloni ule ikiwa leo wakoloni wanakuja nchini kama wawekezaji wakiwa na matrillioni ya fedha walizo zichapisha wao wenyewe toka viwanda vyao, na kutuhadaa kwa mikataba walioandika wao, kisha wakachimba na kuchukua dhahabu yetu, wakaichua na kuiweka katika hazina zao kwa thamanisho sawa na karatasi walizochapisha wao zikithaminishwa kama ni fedha?

Hivi kweli sisi Waafrika kwa akili gani tulizojaaliwa, tunakubali kuhodhi kama akiba yetu hazina hizo karatasi ambazo hazina thamani ila kwa mzani wa Wakoloni wakati wao wamehifadhi dhahabu yetu kwa gharama ya karatasi walizochapisha kama fedha! Sijui kama nimeeleweka hapo..

Yawezeka mimi nashindwa kuelewa mantiki ya Biashara hii mnijuze wataalam wa Uchumi. Inawezekanaje kampuni ya madini kutoka Marekani, Canada, Uingereza au Australia inawekeza mathlan dollar millioni 300 ambazo watanunua vifaa vinavyotegenezwa kwao wenyewe kuja kuchimba dhahabu ilihali mzunguko wa fedha hizo za uwekezaji umebakia kwao? (Mtaji wa uwekezaji ni karatasi zao na wamenunua zana zao) kuja kuchimba madini yetu kwa ahadi ya faida ya mauzo yao sii yetu!

Kampuni zao za utengenezaji zana na uchimbaji ndizo zIlofaidika na matrillioni ya fedha hizo kukuza Uchumi wao wa ndani, halafu wanakuja kwetu wanachimba dhahabu kama mali yao na kuondoka nazo kwa faida nyingine wakati sisi tunaachiwa mashimo yalojaa kemikali hatariahi kwa mazingira yetu wakitupa matumaini ya kuvuna karatasi walochapisha wao kama fedha na akiba yetu.

Kwa maana nyingine tumenufaika na karatasi zao na kuzilimbikiza hazina kama pato la Taifa lakini lenye deni kubwa zaidi kwa sababu tulikopa fedha nyingine kutoka kwao zenye riba ili kutengeneza barabara, nguvu ya umeme, maji, mawasiliano na kadhalika. Kibindoni hazina tumeshehena karatasi ambazo tunajigamba kuwa na uchumi imara na tuna akiba ya kutosha.

Mimi naamini hapa hakuna usawa kabisa na inatakiwa Hatua ya Uthibitisho (affirmative action) juu ya dhulma hii ambayo imetulemaza nchi maskini na kubakia tegemezi miaka yote.

Huu ni wakati muafaka kwa Waafrika tuamke ili haki itendeke maana tusipoweza kutambua ghirba hii ya Elimu ya Uchumi na maendeleo basi tutaendelea kujenga maghorofa kama mahekalu ya Pyramid ilihali maisha ya Wananchi yataendelea kuwa duni kwa sababu hawa wakoloni wana hila na katu hawaweza kutupa elimu yenye manufaa kwetu. Haiwezekani wao wahifadhi dhahabu yetu kama akiba ya utajiri wao, wakati sisi tumeshehena karatasi zao hazina.

Allahu yaalam, sijui ni lini lakini itafika wakati sisi tutazitafuta hizo dhahabu tusiwe nazo tena, halafu itatulazimu sisi tuzinunue kutoka kwao kwa gharama nyingine kabisa wala sii tena karatasi zao bali Uhai wetu.
Uamsho - Akutendae mtende, mche asiyekutenda.

Maasalaam - EID MUBARAK
 
Lah!
Mkandara bhwanah!

Sijui kwa nini umekuja na mawazo ya namna hii wakati huu tunapopigiwa kelele kila kona kuwa hatuwezi kupata maendeleo sisi wenyewe bila ya hao wakoloni wetu.

Ngoja nijaribu kupanua mtiririko wa mawazo yako kwa kutaja tu kiufupi tunavyozidi kuingizwa ndani ya ukoloni wa hawa watu.
1. Bunge la hao wakubwa wanaona mabunge yetu hayana maana. Mfano: Bunge la Uganda wametunga sheria yao ya kukataa ushoga. Bunge la Ulaya wanasema kila njia zitumike kuwaadabisha waganda kama M7 atakubaliana na sheria hiyo. Uhuru wa waganda upo wapi hapo.
Lakini ni hao hao wabunge wa Ulaya, wanaosema sasa, kwamba kama kuna kahwa, cocoa au zao lolote linalolimwa kwa kufyeka misitu, bidhaa hizo kwao ni marufuku! Kila siku wanaendelea kutafuta njia za kutuweka chini ya himaya zao. Si ni hao hao hawataki bomba la mafuta toka Uganda?

2. Moody's kaja juzi kwetu kutukagua kujua kama tunayo adabu ya kutosha na kufuata yote tunayoelekezwa kuyafanya. Kafurahishwa na juhudi zetu tunazofanya, sasa katuonjesha asali kwa kutupa alama ya B2+ na kuahidi tukiendelea kuwasikiliza IMF na kutimiza masharti, alama nzuri zaidi tutazipata. Sisi tunakenua meno yote, na kuanza kujipigapiga tuvifua twetu kama sokwe aliyenogewa na asali!

3. Nini, unazungumzia madini ya dhahabu? Hayo yana faida gani kwetu zaidi ya Graphite, nickel, Rare Earths wanazozoa hapa kwetu kama kichwani hatuna kitu? Miaka 60 baada ya kujitangazia kuwa tupo huru, lakini tunashindwa sisi wenyewe kutumia akili zetu kuufaidi uhuru huo kwa kuzitumia mali alizotujaalia Mwenyezi Mungu. Tunatupa tu kama takataka vile.

4. Nyimbo mashuhuri tunazoimbishwa siku hizi na hao wakoloni wetu ni :Uwazi, demokrasia n.k., ili kupitia humo wapate njia nzuri za kututawala kwa maslahi yao. Wanasema mtindo wao wa utawala ndio "best practice" unaotakiwa kuigwa kila mahala, kumbe hiyo 'best practice' yao ndiyo njia yao ya kututawala na kututaka nasi tudumishe wanazoziita "values" zao, kana kwamba sisi hatuwezi kuwa na "values" tunazoona zinatufaa wenyewe, kama kukataa hayo mambo ya ushoga.

5. Wana kila aina ya vyombo vya kutupima na kutuweka kwenye ordha zao kufuatana na tunavyokaribia kuwa kama wao. Kwa hiyo, hata miji yetu inapimwa nafasi zinazoshikilia katika utajiri, kwa kuhesabu mabilionea ndani ya miji hiyo, bila kujali ni matumbi wangapi mabilionea ndani ya hiyo miji. Kwa hiyo Nairobi wana nafuu zaidi kutushinda sisi Dar, na tunapoona hivyo roho zetu zinasononeka sana, tunatamani tuwe kama Johanesburg au Capetown, nasi tufurahi, hata kama asubuhi ya jana hata kikombe cha chai hatukukipata, kwa sababu sukari haishikiki bei.

Viongozi wetu, ndio wamekuwa wakala wakubwa wa kutuuza kwenye ukoloni huu mpya, hawaamini kamwe kwamba wakifanya kazi nasi wananchi, tunaweza kabisa kuleta mageuzi makubwa sana katika maisha yetu. Kwa hiyo, kila siku utasikia nyimbo za kuvuta wawekezaji, lakini husikii juhudi kubwa za kuwahimiza wananchi wajikaze hata kufanya mambo yaliyomo kwenye uwezo wetu wa kuyafanya.

Hawa wanaokuja kuwekeza hapa hawatuletei zawaidi, wanakuja kuwafanyia kazi watu wao ili faida itakayopatikana hapa iwanufaishe wao zaidi yetu sisi.

Mbona hadithi hii ni ndefu sana bila mwisho!

Niseme tu, watakaotaka kuukata huu mpango wa kutawaliwa upya, nafasi ipo. Mfumo wa uchumi kutegemea masharti ya nchi za Magharbi sasa utapata upinzani toka kwa mataifa mengine makubwa yanayouktaa mpango huo. Watakaotaka kudandia huko, na kukataa ukoloni mpya ni heri yao.
 
Jazakallah khairan Mallam Mkandara,

Kwa mfano, bluprinti ya mifumo ya fedha katika UCHUMI HAI -- UCHUMI MAMA, hulandana na seti za tololojia fikirifu kwa topografu za Mwili Hai -- 'Moyo na Damu' katika anatomia ya Mwili. Mwalimu alikuwa na magutu juu ya hili, lakini 'wakati haukuwa sahihi kwa maarifa haya kumfikia yeye na wengine wa nyakati zake'. Kwa hivi hili yeye daima alikuwa akilibaini kama 'Mwili Mmoja, Viungo Mbalimbali'--Ontolojia na Metafizikia ya Uongozi katika 'Ushirika wa Kiroho'... Kwa kuwa shauri hili, lilikuwa pia kwa Paulo; akielekeza kuhusu 'Kristu' na 'Utawala' mpya... Kwenye Kitabu cha 'TUJISAHIHISHE'; Mwalimu alikuwa 'akitafuta kurekebisha mitambo ya tabia' ya 'ulimbukeni wa tawala' angali mapema. Sisi wabantu tuna methali, Samaki Mkunje Angali Mbichi…

Kwa Uono na Ufikirifu Mifumo, tunatafuta kubaini 'nguvu' na 'misukumo' ya kifedha ina kuja kwa 'vitovu' vipi Utaasisi wa Kijamii, na kufungamana vipi na hiyo. Jambo hili ndilo lililoleta mvutano kati ya Jefferson na Hamilton wakati wa Kuanzishwa kwa Taifa la Merekani. Kule Amerika, jambo hili linalotengenezewa njia katika Bara la Afrika, lilitengenezewa njia Merekani. ELIMU 3.0 itatupatia funguo kwa ufunuo kuhusiana na 'wacheza mchezo' wa wakati mmoja kule Amerika ndiyo wale wale wanacheza mchezo huku... Hispania iliendelea barani Ulaya kwa 'fujo za kikoloni' walizozifanya Amerika ya Kati, ambapo uporaji wa dhahabu, mateso na maangamizi ya wazawa wa kule 'kulitengeneza hazina' ya tawala za Kifalme Hispania. Waingereza walipotamani na wao waende 'India ya Magharibi' wakakombe visivyo vyao, walifikia jimbo la Virginia lakini sasa kule hakukuwa na dhahabu, bali ardhi ya bwerere na jamii zisizokuwa na makuu za Wahindi Wekundu. 'Wanamapinduzi' kutoka Ulaya walijipenyeza katika 'Siasa za Tawala' za 'Nchi Mpya' kwa kuwa 'malaika watu' wa 'Kumaliza Vita za Wenyewe kwa Wenyewe' za wahamiaji--wote wakiwa ni wahamiaji katika kutafuta utajiri na mafanikio nchi ya wazawa wa Kihindi--Wahindi Wekundu.

Merekani, iliinuka na kustawi kwa kuanzia chini kabisa badala ya kuwa koloni la 'Muingereza'. Kwa 'ndoto ya dhahabu kuota mbawa', nchi hii kutoka awali ilijinasibu na 'Ujamhuri', 'Utawala wa Sheria' na 'Ubunifu na Mbinu za Kazi' kama 'ngome ya pamoja ya maendeleo na ustawi' kwa majimbo yenye kufanya Muungano ulio nishirikisho la Utawala wa Majimbo katika Amerika. Sasa, sisi kama watu wa Taifa Changa la Tanzania, tunayoyakujifunza kutoka kwa mataifa yaliyodumu kwa muda mrefu. ELIMU 3.0 itatupatia ufunguo kwa Ufunuo wa kushangaza siku za mbele... Miaka hii yote, takriban 400, watesi ndiyo wamekuwa wateswaji--na kinyume chake vivyo hivyo. Janga la Utumwa na Biashara ya Utumwa, wote huo umekuwa ni mchezo... Watu wote ambao leo hii wanakata shauri kuwa 'watu wema' ni kwa kuwa 'wamezicheza pande zote mbili' na wakati umefika, wanakata shauri 'kujua ilivyo bora'... Afrika Inajengwa na Itajengwa zaidi na watu wenye kutafuta kusahihisha 'makosa ya jana'... Afrika tayari inayorasilimali 'watu wa njia' kulinasibu hili bara na maendeleo yasiyotegemea 'Unyonyaji' ama 'Udhalilishaji wa Utu'...

Kwa uono na Ufikirifu Mifumo, hekima inafanyika kutambua ni namna gani taifa moja linaweza kuendelea na jingine kukwama na hali watu ni walewale kimaumbile, jiografia, na mifumo ya msingi ya maisha. Kwa kuwa jibu rahisi linadhihirika kupitia 'Ontolojia ya Taasisi' za jamii. Hili ndilo lafanya fremu-kazi ya 'uono na ufikirifu mifumo' kuwa zana rahisi ya kuwapa wepesi wanajamii wazungumze masuala ya jamii na maendeleo kwa ufasaha--ufasaha wa kuweza kubaini ukweli wa mambo na si porojo za 'mijadala ya hoja' ama 'midahalo'. Jamii inahitaji ujuzi na uwezo wa kubaini jiometria ya utendekavyo maamuzi jamii na si hasa porojo za 'demokrasia za kiliberali'. Ikiwa jamii itajinasibu na muktadha wa fremu-kazi ya uono na ufikirifu mifumo, mazungumzo ya wanajamii yataanza kupata umakini na koherensia ya mashauri yenye kuakisi kujua ilivyobora... Na basi jamii itakuwa na nyenzo ya kujenga ushawishi kwa sura na mielekeo bora na fasaha ya maendeleo na ustawi wake.

Alhamdullillah, Nuru imo ndani yetu!
EID MUBARAK
 
Namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma aliye nijalia kwa rehma zake mfungo wa Ramadhan salama salimin. ALHAMDULILLAH.

Hoja yangu ya leo ni UAMSHO kwa ndugu zangu waafrika juu ya nadharia ya Uchumi kuwa NI elimu ya juu ya mfumo bora wa maendeleo ya watu na nchi zote duniani. Mfumo mmoja kandamizi kwa wote. Labda nusjereheshe hapa chini..

Hoja yangu inahusu Elimu hii ya Uchumi ambayo kwanza inatudhalilisha sana sisi Waafrika kama kwamba sisi hatuwezi kufikiri nje ya mfumo huo isipokuwa kwa mapokezi ya mafundisho ya Wakoloni walotutawala na wakafaidika na rasilimali zetu kwa njia za udanganyifu wa mapambo ya wadhifa ya Uhuru wa bendera.

Hivi leo tunapodai tupo huru, uhuru huo tunao kweli ikiwa bado tunatumia Elimu ya Uchumi wa Ukoloni Mambo leo? Tofauti gani iliyopo na Ukoloni ule ikiwa leo wakoloni wanakuja nchini kama wawekezaji wakiwa na matrillioni ya fedha walizo zichapisha wao wenyewe toka viwanda vyao, na kutuhadaa kwa mikataba walioandika wao, kisha wakachimba na kuchukua dhahabu yetu, wakaichua na kuiweka katika hazina zao kwa thamanisho sawa na karatasi walizochapisha wao zikithaminishwa kama ni fedha?

Hivi kweli sisi Waafrika kwa akili gani tulizojaaliwa, tunakubali kuhodhi kama akiba yetu hazina hizo karatasi ambazo hazina thamani ila kwa mzani wa Wakoloni wakati wao wamehifadhi dhahabu yetu kwa gharama ya karatasi walizochapisha kama fedha! Sijui kama nimeeleweka hapo..

Yawezeka mimi nashindwa kuelewa mantiki ya Biashara hii mnijuze wataalam wa Uchumi. Inawezekanaje kampuni ya madini kutoka Marekani, Canada, Uingereza au Australia inawekeza mathlan dollar millioni 300 ambazo watanunua vifaa vinavyotegenezwa kwao wenyewe kuja kuchimba dhahabu ilihali mzunguko wa fedha hizo za uwekezaji umebakia kwao? (Mtaji wa uwekezaji ni karatasi zao na wamenunua zana zao) kuja kuchimba madini yetu kwa ahadi ya faida ya mauzo yao sii yetu!

Kampuni zao za utengenezaji zana na uchimbaji ndizo zIlofaidika na matrillioni ya fedha hizo kukuza Uchumi wao wa ndani, halafu wanakuja kwetu wanachimba dhahabu kama mali yao na kuondoka nazo kwa faida nyingine wakati sisi tunaachiwa mashimo yalojaa kemikali hatariahi kwa mazingira yetu wakitupa matumaini ya kuvuna karatasi walochapisha wao kama fedha na akiba yetu.

Kwa maana nyingine tumenufaika na karatasi zao na kuzilimbikiza hazina kama pato la Taifa lakini lenye deni kubwa zaidi kwa sababu tulikopa fedha nyingine kutoka kwao zenye riba ili kutengeneza barabara, nguvu ya umeme, maji, mawasiliano na kadhalika. Kibindoni hazina tumeshehena karatasi ambazo tunajigamba kuwa na uchumi imara na tuna akiba ya kutosha.

Mimi naamini hapa hakuna usawa kabisa na inatakiwa Hatua ya Uthibitisho (affirmative action) juu ya dhulma hii ambayo imetulemaza nchi maskini na kubakia tegemezi miaka yote.

Huu ni wakati muafaka kwa Waafrika tuamke ili haki itendeke maana tusipoweza kutambua ghirba hii ya Elimu ya Uchumi na maendeleo basi tutaendelea kujenga maghorofa kama mahekalu ya Pyramid ilihali maisha ya Wananchi yataendelea kuwa duni kwa sababu hawa wakoloni wana hila na katu hawaweza kutupa elimu yenye manufaa kwetu. Haiwezekani wao wahifadhi dhahabu yetu kama akiba ya utajiri wao, wakati sisi tumeshehena karatasi zao hazina.

Allahu yaalam, sijui ni lini lakini itafika wakati sisi tutazitafuta hizo dhahabu tusiwe nazo tena, halafu itatulazimu sisi tuzinunue kutoka kwao kwa gharama nyingine kabisa wala sii tena karatasi zao bali Uhai wetu.
Uamsho - Akutendae mtende, mche asiyekutenda.

Maasalaam - EID MUBARAK
My friend colonialism is still there in Africa but in more modern state,Afrika haikuwahi kupata Uhuru iwe kiuchumi,kisiasa,au kijamii.Tuko kwenye uchumi wa kikoloni ambao sifa yake kuu ni Afrika kuwa na uchumi tegemezi.Wazungu kilichopekekea kuitawala Africa ni kupata sehemu ya kukidhi mahitaji ya mapinduzi ya viwanda huko kwao ambayo ni kupata malighafi Kama madini,mazao ya kilimo na mifugo na raailimali nyingine,kupata masoko ya bidhaa zao,kupata maeneo ya kuwekeza mitaji yao,kupata maeneo ya kuweka makazi n.k.Katika kufanikisha hayo njia rahisi kwao ni kumtumia mikataba ya ulaghai,wakina mangungo wa msovero tuliosoma kwenye vitabu kwamba Carl Peter aliwasainisha mikataba ya ulaghai hadi Leo wapo,unadhani kwa nini katiba ya nchi inasema mikataba ni Siri,ni Siri kwa faida ya waafrika au wazungu? Kama Mali ni zetu kwa nini tusijue tulichokubaliana?je Mambo yetu kisiasa tunayaamua wenyewe au tunaamriwa ,maswala ya kijamii tunayaamua wenyewe? Huu ushoga unaoanza kuingizwa kidokidogo haitafikia muda tukalazimishwa kwa mashinikizo mbalimbali? Sasa Uhuru wetu uko wapi.Magufuli alipigwa Vita kwa sababu alitaka tujitegemee na si kuwategemea wazungu wakati sifa kuu ya ukoloni ni Afrika iwe tegemezi .kwa nini misaada na mikopo tunayopewa hailengi kujenga viwanda? Isipokuwa madarasa barabara na Mambo mengine ambayo hayatupelekei kujitegemea kiuchumi.Njia wanazotumia ni zilezile za tangia zamani za diplomacy, signing bogus treaties, collaboration, intimidation/gunboat na military force.Kwa ufupi ukoloni kwa Afrika bado upo na tunatawaliwa kirahisi kwa sababu mawakala wa ukoloni tunaishi nao ndani ya Taifa
 
Kwakifupi ni kwamba hatuko huru. Hauwezi kuwa tegemezi alafu ukawa 'huru'.

Jamaa wametuzidi akili sio siri, na wataendelea kututawala milele.
 
Hauwezi kuwa Tegemezi halafu Ukawa Huru

Hili neno zito sana, tujitambue! Hivi kweli Waafrika kwa umoja wetu tunashindwa kabisa kujinasua katika minyororo hii?
 
Lah!
Mkandara bhwanah!

Sijui kwa nini umekuja na mawazo ya namna hii wakati huu tunapopigiwa kelele kila kona kuwa hatuwezi kupata maendeleo sisi wenyewe bila ya hao wakoloni wetu.

Ngoja nijaribu kupanua mtiririko wa mawazo yako kwa kutaja tu kiufupi tunavyozidi kuingizwa ndani ya ukoloni wa hawa watu.
1. Bunge la hao wakubwa wanaona mabunge yetu hayana maana. Mfano: Bunge la Uganda wametunga sheria yao ya kukataa ushoga. Bunge la Ulaya wanasema kila njia zitumike kuwaadabisha waganda kama M7 atakubaliana na sheria hiyo. Uhuru wa waganda upo wapi hapo.
Lakini ni hao hao wabunge wa Ulaya, wanaosema sasa, kwamba kama kuna kahwa, cocoa au zao lolote linalolimwa kwa kufyeka misitu, bidhaa hizo kwao ni marufuku! Kila siku wanaendelea kutafuta njia za kutuweka chini ya himaya zao. Si ni hao hao hawataki bomba la mafuta toka Uganda?

2. Moody's kaja juzi kwetu kutukagua kujua kama tunayo adabu ya kutosha na kufuata yote tunayoelekezwa kuyafanya. Kafurahishwa na juhudi zetu tunazofanya, sasa katuonjesha asali kwa kutupa alama ya B2+ na kuahidi tukiendelea kuwasikiliza IMF na kutimiza masharti, alama nzuri zaidi tutazipata. Sisi tunakenua meno yote, na kuanza kujipigapiga tuvifua twetu kama sokwe aliyenogewa na asali!

3. Nini, unazungumzia madini ya dhahabu? Hayo yana faida gani kwetu zaidi ya Graphite, nickel, Rare Earths wanazozoa hapa kwetu kama kichwani hatuna kitu? Miaka 60 baada ya kujitangazia kuwa tupo huru, lakini tunashindwa sisi wenyewe kutumia akili zetu kuufaidi uhuru huo kwa kuzitumia mali alizotujaalia Mwenyezi Mungu. Tunatupa tu kama takataka vile.

4. Nyimbo mashuhuri tunazoimbishwa siku hizi na hao wakoloni wetu ni :Uwazi, demokrasia n.k., ili kupitia humo wapate njia nzuri za kututawala kwa maslahi yao. Wanasema mtindo wao wa utawala ndio "best practice" unaotakiwa kuigwa kila mahala, kumbe hiyo 'best practice' yao ndiyo njia yao ya kututawala na kututaka nasi tudumishe wanazoziita "values" zao, kana kwamba sisi hatuwezi kuwa na "values" tunazoona zinatufaa wenyewe, kama kukataa hayo mambo ya ushoga.

5. Wana kila aina ya vyombo vya kutupima na kutuweka kwenye ordha zao kufuatana na tunavyokaribia kuwa kama wao. Kwa hiyo, hata miji yetu inapimwa nafasi zinazoshikilia katika utajiri, kwa kuhesabu mabilionea ndani ya miji hiyo, bila kujali ni matumbi wangapi mabilionea ndani ya hiyo miji. Kwa hiyo Nairobi wana nafuu zaidi kutushinda sisi Dar, na tunapoona hivyo roho zetu zinasononeka sana, tunatamani tuwe kama Johanesburg au Capetown, nasi tufurahi, hata kama asubuhi ya jana hata kikombe cha chai hatukukipata, kwa sababu sukari haishikiki bei.

Viongozi wetu, ndio wamekuwa wakala wakubwa wa kutuuza kwenye ukoloni huu mpya, hawaamini kamwe kwamba wakifanya kazi nasi wananchi, tunaweza kabisa kuleta mageuzi makubwa sana katika maisha yetu. Kwa hiyo, kila siku utasikia nyimbo za kuvuta wawekezaji, lakini husikii juhudi kubwa za kuwahimiza wananchi wajikaze hata kufanya mambo yaliyomo kwenye uwezo wetu wa kuyafanya.

Hawa wanaokuja kuwekeza hapa hawatuletei zawaidi, wanakuja kuwafanyia kazi watu wao ili faida itakayopatikana hapa iwanufaishe wao zaidi yetu sisi.

Mbona hadithi hii ni ndefu sana bila mwisho!

Niseme tu, watakaotaka kuukata huu mpango wa kutawaliwa upya, nafasi ipo. Mfumo wa uchumi kutegemea masharti ya nchi za Magharbi sasa utapata upinzani toka kwa mataifa mengine makubwa yanayouktaa mpango huo. Watakaotaka kudandia huko, na kukataa ukoloni mpya ni heri yao.
Shukran sana kwa maneno mazito, mimi nadhani ipo haja kubwa sana ya kurudisha falsafa ya Pan Africanism tena kwa nguvu kubwa sana kama KIMBUNGA.
 
"Vita Baridi" mpya imeanza, kwa hiyo inawezekana pia "Pan Africanism" ikarudi tena.
Sioni jinsi gani hawa wakoloni watakavyoweza kufanikiwa kututawala tena.
Watatuvuruga mara kwa mara, lakini kututawala tena hawataweza.
 
Kwakifupi ni kwamba hatuko huru. Hauwezi kuwa tegemezi alafu ukawa 'huru'.

Jamaa wametuzidi akili sio siri, na wataendelea kututawala milele.
Ninakubaliana na maneno ya mstari wako wa kwanza.

Sikubaliani kamwe na hiyo dhana potofu ya mstari wa pili..

"...kuwa tegemezi..." haina maana ya kutokuwa na akili.

Huyo anayekufanya uwe tegemezi kwake kwa mbinu mbalimbali, unaweza kumkatalia takwa lake la wewe kuendelea kuwa tegemezi kwake.

Lakini,niseme, ni kama maudhui ya mada hii bado hujaielewa vizuri. Kiuhalisi, ni nani hasa tegemezi kati ya hao wakoloni na sisi tunaoporwa mali zetu na uhuru wetu ili huyo mporaji aendelee kustawi?
 
"Vita Baridi" mpya imeanza, kwa hiyo inawezekana pia "Pan Africanism" ikarudi tena.
Sioni jinsi gani hawa wakoloni watakavyoweza kufanikiwa kututawala tena.
Watatuvuruga mara kwa mara, lakini kututawala tena hawataweza.
Mbona bado wametutawala
 
Mbona bado wametutawala
Ninakubali "bado wanatutawala", lakini vita vya ukombozi ndivyo hivyo vimekwishaanza kwa mara ya pili.

Safari hii tutamalizana moja kwa moja, hakuna tena cha kutumia ujanja ujanja kuendelea kututawala kama walivyofanya mwanzo.
 
Kitabu THE NEW CONFESSIONS OF AN ECONOMIC HITMAN-John Perkins.

Waalaikumsalaam kamarada.

I'd ul Mubarrak [emoji120]
 
My friend colonialism is still there in Africa but in more modern state,Afrika haikuwahi kupata Uhuru iwe kiuchumi,kisiasa,au kijamii.Tuko kwenye uchumi wa kikoloni ambao sifa yake kuu ni Afrika kuwa na uchumi tegemezi.Wazungu kilichopekekea kuitawala Africa ni kupata sehemu ya kukidhi mahitaji ya mapinduzi ya viwanda huko kwao ambayo ni kupata malighafi Kama madini,mazao ya kilimo na mifugo na raailimali nyingine,kupata masoko ya bidhaa zao,kupata maeneo ya kuwekeza mitaji yao,kupata maeneo ya kuweka makazi n.k.Katika kufanikisha hayo njia rahisi kwao ni kumtumia mikataba ya ulaghai,wakina mangungo wa msovero tuliosoma kwenye vitabu kwamba Carl Peter aliwasainisha mikataba ya ulaghai hadi Leo wapo,unadhani kwa nini katiba ya nchi inasema mikataba ni Siri,ni Siri kwa faida ya waafrika au wazungu? Kama Mali ni zetu kwa nini tusijue tulichokubaliana?je Mambo yetu kisiasa tunayaamua wenyewe au tunaamriwa ,maswala ya kijamii tunayaamua wenyewe? Huu ushoga unaoanza kuingizwa kidokidogo haitafikia muda tukalazimishwa kwa mashinikizo mbalimbali? Sasa Uhuru wetu uko wapi.Magufuli alipigwa Vita kwa sababu alitaka tujitegemee na si kuwategemea wazungu wakati sifa kuu ya ukoloni ni Afrika iwe tegemezi .kwa nini misaada na mikopo tunayopewa hailengi kujenga viwanda? Isipokuwa madarasa barabara na Mambo mengine ambayo hayatupelekei kujitegemea kiuchumi.Njia wanazotumia ni zilezile za tangia zamani za diplomacy, signing bogus treaties, collaboration, intimidation/gunboat na military force.Kwa ufupi ukoloni kwa Afrika bado upo na tunatawaliwa kirahisi kwa sababu mawakala wa ukoloni tunaishi nao ndani ya Taifa
[emoji2956]
 
Back
Top Bottom