^^
Nimekuelewa vema kabisa, kama hautachoshwa na udadisi wangu, Je kusamehewa kwa mwanamke kuna maana ipi ktk mahusiano?
^^
mkuu Himidini siwezi kuchoshwa in fact we are doing each other a very great favour!
sijui kama hoja yako nimeielewa mkuu naomba nichangie kwa namna nilivyoelewa nikiwa kinyume tafadhali nitakuomba urejee hoja yako.
kwa asili yetu wanadamu tumepewa uwezo wa kupendana na kushimiana(utii),hii ni "angle" moja katika mengi tuliyoumbiwa kuyatenda.
mwanaume kumpenda mkewe
mwanamke kumitii mmewe(kwa mujibu wa vitabu vya kidini),lakini ukifuatilia vizuri upendo ni neno ambalo ndani yake limebeba utii na uaminifu,ie mtu utayempenda utampa heshima na utamuamini na kumtendea kwa uaminifu,utii pia ni neno linalobeba upendo na uaminifu i.e kitu/mtu unayempenda ni rahisi sana kumheshimu tofauti na yule usiyempenda,
mwisho wa siku watu wanopendana wanabadilishana baina yao vitu vingi(they exchange between each other) lakini vya umuhimu ni upendo(uaminifu ,kujali,n.k) na utii baina yao kwa mafano ambapo simu inavyobadilishana mawimbi na minara ya mawasiliano kimoja kikizimwa kinazuia mbadilishano huu na tatzio mara nyingi linaanzia hapa,kwa kipindi hiki ndio pindi msamaha,uaminifu na uvumilivu unapaswa kutumiwa lakini wengi wetu hatufnyi hivi.
mapenzi na mahusiano ni kitu kinachokuja kwa kuambanatana vitu vingin,i.e ni kama cafeteria yaani upendo uje in "packages" uwe na uaminifu,kujali,kuvumilia n.k,pengine utahitaji kutumia uvumilivu pengine kujali katika kuyaimarisha mapendo baina yenu.
ndio maana nimetoa mfano wa cafeteria ya chakula kuna vyakula vya aina nyingi lakini mchana utaweza kuamua kula ugali lakini jioni ukala kitu tofauti,ndio hivyo kwenye mahusiono pengine unapswa utumie kujali kwa kiwango kikubwa wakti mwingine unapaswa kuja na kitu kingine zaidi na vyote hivi visukumwe na upendo na si ubinafsi.
msamaha ni kitu chenye faida(athari chanya)kwa watu wawili kwanza yule anaetoa msamaha anafutia yule anayesamehewa,msamaha unaotoa kama haukufaidishi wewe(haufadiki nao wewe pengine si msamaha halisi) hautakua na manufaa kwa anayesamehewa pia.i.e msahama wa kweli una vionyesho vingi(indicators) nyingi lakini kikubwa ni kuleta amani ya moyoni na furaha,hivyo msamaha kwa kuanzia utaleta furaha na amani kwa mtoa msamaha na hali hiyo ya furaha na amani itashia kwa anayeomba msamaha baada ya hapo kitakachotokea ni historia.
kwa kumalizi mtu yeyote anayekuja kuomba msamaha kwa kuwa kweli ameoliona kosa lake na kujutia haombi msamaha ilimradi haijalishi ni mmwaume au mwanamke kuna maana ya kutafuta nafasi ya pili ya kutengeneza palipokosewa.