Uaminifu wa mapenzi na password ya simu

Uaminifu wa mapenzi na password ya simu

nanjilinji

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
1,206
Reaction score
566
Kwa sasa kila mtu anatamani au anatumia Smartphones,hata huku kwetu vijijini akinadada na makaka wa kishua wanatumia hizo simu tunaita simu-tanashati.

Ukitaka kujua kuwa mpenzi wako anaaminika au haaminiki, ni kuangalia kama simu yake ina Password unayoifahamu.
Kama mpenzi au mwenzi wako anaweka password ambayo huijui, jua si MWAMINIFU na muogope kama ukoma maana udanganyifu wa mapenzi umezidi.

Ujumbe: kabla ya kugegedana muombe mpenzi wako kama njia ya kumuandaa akupe simu yake/zake na uchungulie; akikupa jua ni mwaminifu na endelea hata bila ndomu ila akikataa geuka mzungu wa tano.


Wekeend njema
 
Sema ukiona umeenda dukan kununua sumu ya kujiua ukakosa, muombe mwenza wako cm yake!!!
kiulaiiiin UNA REST IN PEACE
 
Napataga wakati mgumu sana kuwaelewa wapenzi hasa wanandoa wanaowekeana passwork kwa simu zao......ni maajabu lakini ndio ukweli...unapofikia hatua ya kuweka siri ya password ya simu tu tena mwenzi wako, akitaka kuijua unakua mkali kama simba alieshikwa makalio, mimi nadhani tayari unakua una mapungufu katika hayo mapenzi manake mapenzi ni matamu kuliko utamu kukiwa hakuna hata chembe ya siri jamani!
 
Binadamu yeyote haaminiki kwa lolote .kwetu wakristo tunasema amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu.
 
Mwalimu...kwa kauli iyo itakuwa bila shaka na ww c mwaminifu aka michepuko processing officer!
 
Najiona nikidondoka na kupooza mwilii pindi nitakaposhika cm ya manziiii anguu
 
Ndugu yangu unasema? Akikupa jua ni muaminifu mwingine anakupa.
Ukifungua huko ni balaaa mpk unajuta kwann uliomba..tena ht hasiti.
 
Mapenzi ya kweli... Ujumbe ukiingia mpenzi anamwambia mwenzie, naomba nisomee huo ujumbe tafadhali
 
Unageuka mzungu wa 5, anatoka nje anampigia " baba mlezi" baby naomba
unifate nimekosa usafiriii.ahaaaaa dkd 0 ndinga hiyo ahaaaaaa
 
Haya mapenzi ya siku hizi ni shidaaaaaa. Anaweza asiweke password Bali akawa na line nyingine ya siri.
 
Ndugu yangu unasema? ?? Akikupa jua ni muaminifu...mwingine anakupa...ukifungua huko ni balaaa mpk unajuta kwann uliomba..tena ht hasiti ...
Huyo achana naye hakufai
 
Back
Top Bottom