Uaminifu wa mapenzi na password ya simu

Uaminifu wa mapenzi na password ya simu

Wanaume mnaongoza ni michepuko tu ukiyaona yaliyomo unaweza kuzimiaaaaaaaa
Wewe unaona bora kufa kwa ukimwi bila kujua kama mwenzi wako ni kicheche au uhakikishe kama ni mcharuko ili uamue kunyoa au kusuka?
 
Kwa sasa kila mtu anatamani au anatumia Smartphones,hata huku kwetu vijijini akinadada na makaka wa kishua wanatumia hizo simu tunaita simu-tanashati.

Ukitaka kujua kuwa mpenzi wako anaaminika au haaminiki, ni kuangalia kama simu yake ina Password unayoifahamu.
Kama mpenzi au mwenzi wako anaweka password ambayo huijui, jua si MWAMINIFU na muogope kama ukoma maana udanganyifu wa mapenzi umezidi.

Ujumbe: kabla ya kugegedana muombe mpenzi wako kama njia ya kumuandaa akupe simu yake/zake na uchungulie; akikupa jua ni mwaminifu na endelea hata bila ndomu ila akikataa geuka mzungu wa tano.


Wekeend njema
C-AcZrbWsAEbT5n.jpg
 
Password ni kipimo tosha cha kuzuia ukimwi. Naomba nijieleze, unaweza kupima mwenza wako nyote mashallah mkawa hamna, baada ya miezi mitatu mkarudi mkathibitisha hamna. Mkaanza kutumbua ile halua kwa raha zenyu nyama kwa nyama. Kivumbi mmoja wenu anachepuka na kuupata, mwenzangu na mie anaamini kuwa mwenzake hachepuki, la haula kumbe anaogelea katika liukimwi. Lakini kama unafahamu password, kuchepuka hakuwezekani. Siku hizi mtu akitaka kutongoza anaomba namba ya simu, kama unajua mpenzi wako ana password, huwezi kumpatia na hapo umeepusha ukimwi. Miss Chagga hii ni kweli au uongo
Nafikiri ifikie wakati watu tuondoe hii dhana potofu ya kutoaminiana hivi nikweli watu walikuwa hawachepuki kabla ya uwepo wa hizi smart phone au simu kwa ujumla?
Nadhani swala la kuchepuka ni hulka ya mtu anaweza akakupa hiyo password na ukatumia simu yake na kuichunguza uwezavyo na bado akawa smart kwenye kuchepuka
La msingi ni kumwamini na kukumbushana kwa upendo endapo utagundua mwenzako hakuelewi au siyo mwaminifu nikujikalia pembeni tu.Sioni sababu ya kuishi na mtu wakati una mashaka naye unahaha kumtega kumpekua mbona hata penzi huwezi faidi maana muda woote wewe roho jujuu tu si bora uachane naye tu.
 
Back
Top Bottom