Rufiji,
ndugu yangu umeanza vizuri sana na unastahili pongezi kwa mchango wako. tatizo la sisi Wabongo lazima uwe na uwezo wa kupima hoja yako hadi tone la mwisho., sawa na mpishi ambaye lazima ahakikishe chunvi haikuzidi wala kuacha chuzi lina maji mengi.
Nakubaliana na wewe sana ulipotoa hoja ya radio na Mbowe anawafahamu vijana wote wazuri sana ktk habari na Utangazaji. Mbowe anawafahamu vijana wengi waliochipukiaktk uandishi wa magazeti na usanii. Free anawafahamu vijana wa rika lake na chini kuliko hata JK na kiongozi mwingine yeyote ndani ya CCM tena kwa ukaribu. lakini kibaya ni kwamba Free hatumii nafasi hiyo kwa manufaa ya chama isipokuwa hisia zake za kibinafsi. Mbowe ni mtu anayetaka umaarufu na kufuatwa yeye kama vile anavyowafuata yeye wale walioko juu yake. Mbowe anataka watu kama akina Mwanakijiji, Mzee Es wakaombe kazi kwake na hata siku moja Mbowe hawezi kumuomba Mwanakijiji awe mwakilishi wa Chadema ktk nchi za nje.
Matumizi ya ndege ya helikopta yalikuwa hayana maana kabisa zaidi ya umaarufu. hakuna hata sehemu moja aliyokwenda Mbowe ambayo magari hayawezi kufika. Uharaka wa kufika sehemu hizo haukuwepo kwani Tanzania nzima usafiri wa siku moja upo toka kila kona. Na uzuri wa msafara wa magari hasa bus kubwa la chama hupitia vituo vidogo muhimu.
Pili, Chadema inatakiwa kuyainua majina ya viongozi wa ndani ambao wanatyegemewa kushika uongozi kesho. leo hii ukimuondoa Mbowe hakuna jina lililobakia kama tishio zaidi ya Zitto na ndugu yetu JJ. hata hivyo hawa hawana nguvu kabisa na majina yao yapo magazetini tu, hakuna kiongozi Chadema anayeweza kwenda mikoani na kuwavutia watu kuhudhulia mkutano ama warsha. Yote haya yanatokana na kutowaanda watu kuwa kivutio cha wananchi. Media coverage ni muhimu sana hata iwe scandal maadamu jina la mhusika liwe ktk ndimi za wananchi.
Anayoyafanya Bush leo hii ni kutayarisha viongozi wa kesho na tayari majina yao yapo midomoni mwa watu. Wenzetu nchi za Ulaya, all politicians, wasanii wa Sinema na sanaa vyinginezo hutumia mbinu za kujitangaza ili kupandisha thamani sanaa zao pia kukuza majina yao. Mtakapo jenga majina ya viongozi wenu nje ya Mbowe, thamani ya Chadema kama chama itapanuka. Hivi sasa Chadema ni Mbowe, asiyempenda Mbowe basi hata Chadema haipendeki kama ilivyokuwa CUF na Seif Sharrif.
Mwisho ndugu Rufiji, samahani sana hoja yako ya mwisho kusema kweli ni tishio kubwa sana na Chadema wasiombe kujaribu mbinu kama hiyo. Mbinu hiyo ndiyo iliyowaangusha CUF na wao CUF wanaamini Chadema ni chama kilichoundwa kuivunja nguvu CUF kwa kutumia imani kama hizo. Kwa maana hiyo CUF na Chadema hawawezi kula sahani moja na kwamwe vyama hivyo haviwezi kuungana. Matokeo yake CCM anaendelea kupeta na marungu mtarushiana wenyewe.