Mfano kuna dada Mtanzania alikwenda ughaibuni, alijilipua Kinyarwanda, baada ya muda alipata boyfriend mzungu. Kurahisisha mambo yule dada alimwambia mzungu yeye Mnyarwanda. Basi mzungu alikutana na Wanyarwanda wakaanza urafiki akijua mashemeji. Wanyarwanda wakamwalika kwao, akaenda na girlfriend wake, wamefika kule mdada Kinyarwanda hajui, ilibidi awaambie yeye hajatoka Rwanda ila ametoka Tanzania. Wamefika nyumbani mzungu anasema kama ulinidanganya mimi na wewe mwisho wetu ni hapa. Sasa huu si ni uongo jamani.Unazungumzia uwongo wa kiasi gani?
Maana kwa uzoefu wangu wa maisha sijawahi kukutana na mtu ambaye hajawahi kudanganya.
Au wapo watu wasiodanganya?
Mfano kuna dada Mtanzania alikwenda ughaibuni, alijilipua Kinyarwanda, baada ya muda alipata boyfriend mzungu. Kurahisisha mambo yule dada alimwambia mzungu yeye Mnyarwanda. Basi mzungu alikutana na Wanyarwanda wakaanza urafiki akijua mashemeji. Wanyarwanda wakamwalika kwao, akaenda na girlfriend wake, wamefika kule mdada Kinyarwanda hajui, ilibidi awaambie yeye hajatoka Rwanda ila ametoka Tanzania. Wamefika nyumbani mzungu anasema kama ulinidanganya mimi na wewe mwisho wetu ni hapa. Sasa huu si ni uongo jamani.
Uaminifu mgum saaanaa
Kila sehemu unasema 'inashauriwa'. Nani anayeshauri mambo ya aina hiyo?Kwa wale walioko kwenye ndoa, neno uaminifu ni silaha kubwa kwenye mahusiano. Uaminifu ninao uongelea hapa leo maana yake ni 100% kwa mwenza wako. Hii inamaanda kuwa wazi na kipato unachopata na jinsi ya kutumia.
Inashauriwa wanandoa kuwa na account tatu yaani kila mtu anakuwa na account ambayo mshahara au pesa za biashara inaingia kila mwezi. Baada ya hapo kunakuwa na joint account ambayo mnakubaliana kuwa kila mwezi wote wawili ni kiasia gani kitaingia. Hii inarahisisha mipango mikubwa ya maendeleo huko mbele, kama kununua kiwanja au gharama za elimu kwa watoto.
Kwenye hii joint account, inashauriwa kuwe na discipline ya kuchukua pesa. Kama uhusiano wenu unabaraka zote na mnaishi kwa amani, hata unapoona mume ametoa laki tano juzi kutoka kweny joint account, utafahamu ni za nini au alishakutaarifu. Sasa pale laki tano inapotoka kumsaidia mama wa mchepuko ndio hatari.
Jamani wapo waaminifu.
1. Ukishakua mwaminifu kwenye tendo la ndoa mengine yanawezekana.
I know ni theory lakini it can be applicable, kwa msaada wa Mungu mkuu. Kupata mke mlevi ambae anasahau kweka akiba ni shetani na anahitaji kukemea.Kila sehemu unasema 'inashauriwa'. Nani anayeshauri mambo ya aina hiyo?
Unachoandika hapa ni 100% theory ukimaanisha partners wote wako sawa, family status kila pande ziko sawa, mahitaji ya baba na mama pamoja na tabia zao ziko sawa. Tabia zetu zinarekebishika kutegemea partners tunaoishi nao. mume akiwa mlevi au akigeuka na kuwa mlevi baadaye, utamshawishije aweke pesa yake pamoja na mke.
Unaweza kumpa awe anaweka yeye bank kila mwisho wa mwezi na yeye awe anashirikishwa kwenye mipango ya nyumba, pia ni vizuri awe na uzoefu ili hata ukiwa na shida au ukiwa umesafiri anaweza yeye kuchukua pesa kwa niaba yako.Inakuwaje kwa wale wamama wa nyumbani ambao hawaingizi kipato? hiyo joint account itafanyaje kazi?
ni hayo tu asante.
Wakati mwingine uaminifu wa pungufu ya %100 ndio kitu kinachofanya mambo yaende, vinginevyo pasingekalika.
Watu kama wewe ndio likitokea la kutokea mali zinapotea kwasababu mke wako hajui kila kitu. Kwa kifupi ni mke anapaswa kuwa best friend wako, sasa kama unaweza kumweleza mke wako matatatizo yako ya kutokupata choo kwanini asijue bank una pesa ngapi?Ok good.
Nadharia yako ya uaminifu imeegemea upande wote wa mume na mke wana kazi nzuri na wanauwezo wa kuweka akiba kwa kushirikiana wote wawili.
1. Ikiwa mume ndo anafanya kazi nzuri na ndo anaihudumia familia na mke hana/hajapata kazi?.
2. Ikiwa mke anafanya kazi yenye kipato kikubwa na mume kipato kidogo sana ukilinganisha na mke yan anabangaiza kwenye shughuli zake ili mradi familia hailali njaa.
(Usiombe mke akuzidi kipato au elimu!! uwe na uvumilivu100%)
..........................................
Kumwamini mwanamke100% ni sawa na kumuamini rafiki yako ambae ni polisi kumuweka wazi na kumueleza kila kitu chako coz siku akighadhibika/ akichukia au akikasirika(au akitaka kupiga bingo) utajuta na kutafuta sura pakuiweka usipaone (observe it).
Dunia imebadilika, Kumuamini mke 100% na kumuweka wazi ni sawa na kumpa mbinu na kuusoma mchezo na akitaka kufanya lake anapita humo humo kwenye 100%
Teh teh teh...hiyo nayo ni kweli ingawa kusema waziwazi si politically correct!
Tena mwanaume mjanja mjanja ndio simshirikishi kabisa, kheri nicheze kibati.