Ualimu ni kazi au shughuli?

Ualimu ni kazi au shughuli?

Usidanganyike acha hofu ya maisha.ualimu ni umaskini mwanaume gani ulipwe hivyo jipange acha kazi mungu yupo utafanikiw
 
kweli wizara ya elimu imeingiliwa mwalimu mzima hujui kuandika unafundisha nini wanafunzi mnaferisha wanafunzi sababu ya kwanza ni nyie
nani kakudanganya kuwa mshahara unakutoa kimaisha badala ya kufungua biashara na kubana matumizi hata upewe milion kama mtu wa pombe haisaidii unalalamika mshahara mdogo hutaki kujiendeleza unategemea ulipwe kiasi gani tukulipe milion wakati darasa la saba soma tutakuongeza mshahara kwa kufuatana na elimu yako kama unaona kazi acha kazi kalime au nenda ulaya ukawe mbeba mabox na sio kuja kulalamika hapa JF jitu zima na watoto wafanyaje

Duuuh. Yaani na wewe ndugu yangu maelezo yako yote hapo juu umeamua kuyafanya sentensi moja na inaonekana dhahiri kwamba bado ulikuwa unaendelea! Hakuna koma wala full stop.
 
Pole sana mkuu I know deeply what you mean,but find other alternatives kwa kutumia hicho hicho kidogo unachokipata
 
Ndugu, mshahara pekee hautoshi, fanya ujasilia mali, angalia mahali unapoishi na buni biashara itakayo kupa faida ya 10% au zaidi.

Kama mkeo hana kazi kabisa mfungulie kamradi ka kuku wa kienyeji kama mazingira yanaruhusu (kama upo pembezoni mwa mji/kijijini na kama mazingira yanabana fuga kuku wa kisasa (wa mayai/nyama)

Mradi huo utasimamiwa na mkeo mwenyewe wakati wewe ukiendelea na kazi yako ya ualimu.

Mambo mengi yahusuyo biashara na kama una maswali yahusuyo biashara ingia jukwaa la BIASHARA NA UCHUMI kule utasaidiwa na hakuna mtu atakae kukejeli, there every one is serious with what they are doing, no jokes at all.

Dzudzuku.

we ni mshauri mwema,ninashukuru.
 
TZ tajiri nenda kwenye jukwaa la biashara omba msaada utaelimishwa.daima uwoga ni umaskini thubutu utafanikiwa.
 
Usishangae,ualimu ni kimbilio la waliofeli. Div 4 ndio pass mark zinazohitajika.[/QUOTE

Acha bangi zako wewe unafikiri bila mwalimu ungeweza kujiunga na jamiiforums? Mwalimu ni mtu muhimu sana ambaye hata rais anapaswa kumpa heshima zote.
 
Embu mtuulize wakongwe wa vijijin tuliopo maeneo ya umwagiliaji ungeacha kazi fasta uje ulime.toka mjini nenda kalime.
 
Hakuna msomi tajiri yeyote duniani ambaye anaendesha maisha yake kwa kusubiri mwisho wa mwezi apate mshahara then apange matumizi,karibu wote wanategemea biashara na ujasiliamali...nadhan ungetumia kambuzi hako kadogo katika ujasiliamali kaka...mshahara 2pu hata uwe m5 hautatosha asilani...kwa ushauri mzur na wakitaalam tembelea jukwb la biashara na uchumi teacher or sorry kumbe ni Sir...
 
Na bado walimu wengi wanatamani kupangwa mjini ilhali wanajua mjini ni matumizi tu.
Ukiwa kijijini na msahara huo unaweza ku-save kiasi kila mwezi na ukapata cha kufanya ili kujiongezea kipato.
Kingine mwalimu punguza kulalamika na uchukue hatua.Unafahamu kuna watu ni walinzi tu wanalipwa elfu 80 kama mshahara na bado wana familia!?
Tumia taaluma yako kujua namna ya kuondokana na kuwa tegemezi kwa serikali ambayo iko busy na UKAWA.
 
kweli wizara ya elimu imeingiliwa mwalimu mzima hujui kuandika unafundisha nini wanafunzi mnaferisha wanafunzi sababu ya kwanza ni nyie
nani kakudanganya kuwa mshahara unakutoa kimaisha badala ya kufungua biashara na kubana matumizi hata upewe milion kama mtu wa pombe haisaidii unalalamika mshahara mdogo hutaki kujiendeleza unategemea ulipwe kiasi gani tukulipe milion wakati darasa la saba soma tutakuongeza mshahara kwa kufuatana na elimu yako kama unaona kazi acha kazi kalime au nenda ulaya ukawe mbeba mabox na sio kuja kulalamika hapa JF jitu zima na watoto wafanyaje

Duh! Na wewe unajiita Administrator au ? Hivi unaweza kuandika upuuzi kiasi hicho.acha kudhalilisha taaluma za watu.

Ebu nambie mwalimu wa degree unamlipa sh ngapi? Unapomwambia akasome huo mshahara wa diploma na degree ni sh ngapi? Nyie ndo chanzo cha kuua elimu inchini Shem on you .

Eti acha kazi kalime au nenda ulaya uwe mbeba mabox. Kwani kilimo siyo kazi! Kwa taarifa yako bila kilimo wewe huna lolote utakula pesa? Nina Mashaka na elimu yako, uchumi wa taifa unategemea kilimo kama wewe unadhani wakulima ni wajinga katika nchi hii mwenyezi Mungu akusamehe lakini mimi sikusamehi.

Mwisho nakuahauri unapokuwa huna majibu mazuri kaa kimya wapo wataalam wa ushauri nasaha wangemshauri mwalimu na watoto wetu wakaendelea kufundishwa kwa upendo na huyo mwalimu
 
Mimi ni mwalimu wa kawaida(msingi)Mshahara(soma posho) wangu kutokana na kufuta ujinga watoto wa kinyamwanga ni Tgts C1 ukitoa makato yote+deni la faidika ninabaki na 163,250 mkononi.Nina mke na watoto wawili+mama mzazi.Nimepanga uswahilini ambapo ninalipia 30,000 kwa mwezi(ukitoa kwenye 163,250 kinachobaki ndicho changu).mwezi uliopita nilipokea mshahara(soma posho)tarehe 26,hadi kufikia tar.10 april sikuwa na kitu,hivyo kutoka hapo hadi leo tar 20 naishi kwa mikopo na mizinga.Hadi leo nina deni lisilopungua 70,000 hivyo hadi kufikia mshahara(soma posho)sijui nitakuwa nimebaki na kiasi gani!hivyo nataka kujua,ualimu ni KAZI au SHUGHULI?

nyamuhanga?
 
kweli wizara ya elimu imeingiliwa mwalimu mzima hujui kuandika unafundisha nini wanafunzi mnaferisha wanafunzi sababu ya kwanza ni nyie
nani kakudanganya kuwa mshahara unakutoa kimaisha badala ya kufungua biashara na kubana matumizi hata upewe milion kama mtu wa pombe haisaidii unalalamika mshahara mdogo hutaki kujiendeleza unategemea ulipwe kiasi gani tukulipe milion wakati darasa la saba soma tutakuongeza mshahara kwa kufuatana na elimu yako kama unaona kazi acha kazi kalime au nenda ulaya ukawe mbeba mabox na sio kuja kulalamika hapa JF jitu zima na watoto wafanyaje

Kwan wewe ndo unajua kuandika? Mbona haufuati kanuni za uandishi? Mbona hiyo sentensi yako kubwa kama aya? ------- mkubwa. kumbe nyani haon kundule
 
Duuuh. Yaani na wewe ndugu yangu maelezo yako yote hapo juu umeamua kuyafanya sentensi moja na inaonekana dhahiri kwamba bado ulikuwa unaendelea! Hakuna koma wala full stop.

Mkuu achana na huyu kirazaaa, kazaa juzi juzi tu bado halali vizuri mtoto analia sana usiku kucha mpaka akili imekaaa kiusikusiku.
 
Back
Top Bottom