Ualimu ni kazi au shughuli?

Ualimu ni kazi au shughuli?

mAgaziJuTO.

Senior Member
Joined
Feb 22, 2014
Posts
119
Reaction score
37
Mimi ni mwalimu wa kawaida(msingi)Mshahara(soma posho) wangu kutokana na kufuta ujinga watoto wa kinyamwanga ni Tgts C1 ukitoa makato yote+deni la faidika ninabaki na 163,250 mkononi.Nina mke na watoto wawili+mama mzazi.Nimepanga uswahilini ambapo ninalipia 30,000 kwa mwezi(ukitoa kwenye 163,250 kinachobaki ndicho changu).mwezi uliopita nilipokea mshahara(soma posho)tarehe 26,hadi kufikia tar.10 april sikuwa na kitu,hivyo kutoka hapo hadi leo tar 20 naishi kwa mikopo na mizinga.Hadi leo nina deni lisilopungua 70,000 hivyo hadi kufikia mshahara(soma posho)sijui nitakuwa nimebaki na kiasi gani!hivyo nataka kujua,ualimu ni KAZI au SHUGHULI?
 
Nyumba usio lala hujui kunguni wake kote nishida tupu vumilia utatoka kimaisha

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
acha kazi uone ilivo ngumu kupata kazi.
 
Mimi ni mwalimu wa kawaida(msingi)Mshahara(soma posho) wangu kutokana na kufuta ujinga watoto wa kinyamwanga ni Tgts C1 ukitoa makato yote+deni la faidika ninabaki na 163,250 mkononi.Nina mke na watoto wawili+mama mzazi.Nimepanga uswahilini ambapo ninalipia 30,000 kwa mwezi(ukitoa kwenye 163,250 kinachobaki ndicho changu).mwezi uliopita nilipokea mshahara(soma posho)tarehe 26,hadi kufikia tar.10 april sikuwa na kitu,hivyo kutoka hapo hadi leo tar 20 naishi kwa mikopo na mizinga.Hadi leo nina deni lisilopungua 70,000 hivyo hadi kufikia mshahara(soma posho)sijui nitakuwa nimebaki na kiasi gani!hivyo nataka kujua,ualimu ni KAZI au SHUGHULI?

sio wakati wa kulalamika ni wakati wa kuangalia ni jinsi gani utaweza kupambana na maisha halafu umesema unamkopo uliolea nini? au kama vipi acha kazi na unakoelekea utakuwa tapeli,kwel kazi ya ualimu ina mshahara mdogo ila kuwa hata mjasiriamali
 
WITO

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
sio wakati wa kulalamika ni wakati wa kuangalia ni jinsi gani utaweza kupambana na maisha halafu umesema unamkopo uliolea nini? au kama vipi acha kazi na unakoelekea utakuwa tapeli,kwel kazi ya ualimu ina mshahara mdogo ila kuwa hata mjasiriamali

mkopo nilinunua shamba ila bado sijaliendeleza inawezekana likaniepusha na utapeli ulionitabiria.
 
kweli wizara ya elimu imeingiliwa mwalimu mzima hujui kuandika unafundisha nini wanafunzi mnaferisha wanafunzi sababu ya kwanza ni nyie
nani kakudanganya kuwa mshahara unakutoa kimaisha badala ya kufungua biashara na kubana matumizi hata upewe milion kama mtu wa pombe haisaidii unalalamika mshahara mdogo hutaki kujiendeleza unategemea ulipwe kiasi gani tukulipe milion wakati darasa la saba soma tutakuongeza mshahara kwa kufuatana na elimu yako kama unaona kazi acha kazi kalime au nenda ulaya ukawe mbeba mabox na sio kuja kulalamika hapa JF jitu zima na watoto wafanyaje
 
huyo anaesema polisi huna uhakika polisi sasa hv kidogo wanaliowa pesa nzuri ilw makazi ndio shida mm kama mm mdau ualimu ni shughuli upo kijijin nauli kutoka shuleni hadivtarafan kwa bodaboda elfu20 bado kwenda wilayani mhh shughuli kwa mshahara wa mtoo mada bado hujanywa maziwa.
 
kweli wizara ya elimu imeingiliwa mwalimu mzima hujui kuandika unafundisha nini wanafunzi mnaferisha wanafunzi sababu ya kwanza ni nyie
nani kakudanganya kuwa mshahara unakutoa kimaisha badala ya kufungua biashara na kubana matumizi hata upewe milion kama mtu wa pombe haisaidii unalalamika mshahara mdogo hutaki kujiendeleza unategemea ulipwe kiasi gani tukulipe milion wakati darasa la saba soma tutakuongeza mshahara kwa kufuatana na elimu yako kama unaona kazi acha kazi kalime au nenda ulaya ukawe mbeba mabox na sio kuja kulalamika hapa JF jitu zima na watoto wafanyaje
sasa wewe unampa ushauri au unamponda!
 
Usishangae,ualimu ni kimbilio la waliofeli. Div 4 ndio pass mark zinazohitajika.

Unauhakuka na unacholopoka?
They are the most advanced learner in Tz.
Siku moja chukua vyeti vyao na uangalie pass zao.
 
Ndugu, mshahara pekee hautoshi, fanya ujasilia mali, angalia mahali unapoishi na buni biashara itakayo kupa faida ya 10% au zaidi.

Kama mkeo hana kazi kabisa mfungulie kamradi ka kuku wa kienyeji kama mazingira yanaruhusu (kama upo pembezoni mwa mji/kijijini na kama mazingira yanabana fuga kuku wa kisasa (wa mayai/nyama)

Mradi huo utasimamiwa na mkeo mwenyewe wakati wewe ukiendelea na kazi yako ya ualimu.

Mambo mengi yahusuyo biashara na kama una maswali yahusuyo biashara ingia jukwaa la BIASHARA NA UCHUMI kule utasaidiwa na hakuna mtu atakae kukejeli, there every one is serious with what they are doing, no jokes at all.

Dzudzuku.
 
Mimi ni mwalimu wa kawaida(msingi)Mshahara(soma posho) wangu kutokana na kufuta ujinga watoto wa kinyamwanga ni Tgts C1 ukitoa makato yote+deni la faidika ninabaki na 163,250 mkononi.Nina mke na watoto wawili+mama mzazi.Nimepanga uswahilini ambapo ninalipia 30,000 kwa mwezi(ukitoa kwenye 163,250 kinachobaki ndicho changu).mwezi uliopita nilipokea mshahara(soma posho)tarehe 26,hadi kufikia tar.10 april sikuwa na kitu,hivyo kutoka hapo hadi leo tar 20 naishi kwa mikopo na mizinga.Hadi leo nina deni lisilopungua 70,000 hivyo hadi kufikia mshahara(soma posho)sijui nitakuwa nimebaki na kiasi gani!hivyo nataka kujua,ualimu ni KAZI au SHUGHULI?

sasa wewe ni mwalimu halafu unashindwa kujua kama unafanya shughuli au kazi, hao unaosema unawafuta ujinga unawafutaje wakati wewe ndio mjinga namba moja?
 
Nenda ukasome au usmfanye mkeo kuwa goal keaper utakufa na dhiki
 
Ni kazi ila wewe umeamua kuifanya iwe shughuli kwa vile umeamua kuwa unapumzika kila masaa ya ualimu wa kuajiriwa. Ongeza masaa ya kufanya kazi, halafu kaka mama mzazi anaweza kuwa amechoka anapumzika na mke naye unapangia hesabu si ungetafuta namna akawa anachangia na ukawa unaangalia unakolenga. Inaonekana wewe ualimu siyo mahali pako fanya kazi kwa bidii utafute pa kwenda maana kinachowaweka watu kazini sio kipato tu.
 
Back
Top Bottom