Uadilifu Vs Ubadhirifu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uadilifu Vs Ubadhirifu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkaa Mweupe, Nov 17, 2009.

 1. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Jambo!

  Kwa kitambo sasa kuna jambo lilikuwa likinitatiza kati ya haya maneno mawili. Kwa Watanganyika walio wengi ni neno gani haswa lampasa kuwa kingamo kwa maisha yake.

  Kwetu sisi Watanganyika habari zinazoshika kurasa za usoni kwa kiasi kikubwa ni zile za simanzi au tanzia. Na tulio wengi kwanza twaulizana wasihi wa marehemu. Aah huyu ni mtu mzito sana, al maaruf, machachari sana, alijulikana na watu wengi; mara swali tunalojiuliza ni kuwa atapumzishwa wapi? Hapa ndipo utata unapoanza. Je, ni heri marehemu alivyokuwa muadilifu au alivyokuwa mbadhirifu?

  Wengi huoji atazikwaje kwake wakati ni pamechoka sana? (lakini zingatia kuwa uchokaji huo ndivyo hali halisi ya Watanganyika walio wengi). Ni heri jamaa angejenga kwake mapema.

  Zingatia kuwa huyu jamaa alipata umaarufu kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu au minne, alikuwa ni mtumishi wa umma na si mfanyabiashara, alikuwa akipokea mshahara wa mtumishi wa umma na sio wa kifisadi, ndivyo hali halisi. Je iweje basi watu kuhoji maendeleo yake ingali wakijua kuwa alikuwa mtumishi safi?

  Sasa basi wanaJamii, kwenu ni lipi limfaalo marehemu, kujilimbikizia ili asiaibike au kuheshimu mamlaka ili afedheheke? Weka akili katika hili.

  Nawasilisha.
   
Loading...