Buswelu
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 1,998
- 352
Mambo ni aje?
Nimekukumbuka ewe rafiki mwema mweledi. Mvumilivu asiyeua inzi kwa rungu. Anayejua kuwa leo ni kesho ya jana. Asiyeamini katika hali ya kumgoja chini aliyeko juu. Wewe unayejua kuwa kasi ya baiskeli inatokana na nguvu yako ya kunyonga pedeli.
Nakusalimia sana wewe ambaye ni mgumu kuingia ama kutoka mahali popote kama kotapini. Wewe ambaye unajua kuwa si kila mwenye pua kubwa anazo kamasi nyingi. Na unajua kabisa kuwa mwenye shavu kubwa kama .............. siye alikuibia bisi zako..
Nakusalimia sana...
Wasalaam,
Buswelu