Tzdaima inaelekea kaburini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tzdaima inaelekea kaburini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by thatha, Apr 25, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  HII NDIO FRONT PAGE.
  NDIO INAYOUZA GAZATEI.
  LICHA ya tambo zilizotolewa na serikali kwamba ingetoa maamuzi magumu dhidi ya mawaziri waliotuhumiwa kutumia vibaya madaraka yao na kulisababishia hasara kubwa taifa, jana Waziri Mkuu Mizengo Pinda alishindwa kabisa kufurukuta na kuzima kilio cha Watanzania waliotamani kuona wahusika wakiwajibishwa.

  Sakata la kutaka kujizulu kwa wabunge takriban nane wakiongozwa na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, Pinda alimaliza hotuba yake bila kusema lolote zaidi ya kudai kuwa itayashughulikia maoni yote ya wabunge waliyotoa kuhusiana na uimarishaji bora wa utendaji wa serikali.
  Kwa wiki nzima iliyopita, wabunge walitoa tuhuma nzito dhidi ya baadhi ya mawaziri, ambapo katika hatua inayoweza kuwa kilele cha kuchukizwa na ubadhirifu wa mawaziri hao, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, aliongoza harakati za hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
  Hoja hiyo ambayo ilipokelewa kwa nguvu kubwa na kufikisha zaidi ya wabunge 70 waliosaini kukubaliana na pendekezo la kupiga kura ya kutokuwa na imani, ilisababisha hofu kubwa serikalini, kiasi cha kuilazimisha kamati ya wabunge wa CCM kukutana kwa dharura ambapo inaaminika kuwa mawaziri nane walilazimishwa kuandika barua za kujiuzulu.
  Hata hivyo, siku moja baadaye, habari za kuaminika zilidai kuwa Rais Kikwete alikuwa ameonyesha dalili za kutowawajibisha mawaziri hao na kwamba kusingelikuwa na hatua zozote dhidi yao hadi Bunge linaisha.
  Lakini Ikulu kwa namna ya kipekee ilikanusha taarifa hizo ambazo hatimaye tetesi za kutochukuliwa hatua yoyote kwa mawaziri hao zimebainika kuwa kweli baada ya Pinda kuhitimisha kikao cha saba cha Bunge bila kuchukua hatua yoyote kama ilivyokuwa imeahidiwa
   
 2. paty

  paty JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  kweli we KIZIWI,
   
Loading...