Tz shilling gained strength today | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tz shilling gained strength today

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Bei Mbaya, Aug 19, 2011.

 1. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Tanzania's shilling strengthened for the first time in three days against the dollar as some mining companies sold the U.S. currency to pay for local costs.

  The currency of East Africa's second-biggest economy appreciated as much as 0.6 percent to 1,618.3 per dollar and traded at 1,627.5 in Dar es Salaam, the commercial capital.

  "Inflows came in from non-governmental organizations and some mining companies supplying dollars," Zainul Chandoo, head of Treasury at Standard Bank Group Ltd.'s local unit, said by phone "There otherwise have not been any major deals; we have had normal inflows and outflows."

  source: bloomberg.com

  Tanzania's shilling appreciated the most in more than 14 months against the dollar as mining and tourism companies sold the greenback.

  The currency of East Africa's second-biggest economy's surged as much as 3.6 percent, the most since June 2010, to 1,562.5 per dollar and traded 0.2 percent up at 1,619 by 1:41 p.m. in Dar es Salaam, Tanzania's commercial capital. It rebounded from 1,633.2 on Aug. 19, the weakest intraday level since at least 1994.

  "There have been inflows of dollars from the mining companies and tourism proceeds," Eric Chijoriga, a trader at National Bank of Commerce Ltd., Absa Group Ltd. (ASA)'s local unit, said by phone. "This is when tourist season begins."

  Tanzania vies with Mali to be Africa's third-biggest producer of gold after Ghana and South Africa. The country's inflation rate climbed to 13 percent in July, the fastest pace in 15 months, on higher energy and food costs, the National Bureau of Statistics said on Aug. 15.

  [news via
  bloomberg.com]

   
 2. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Siasa nyingi mno!! hakuna financial control yeyote!! BOT wapo pale kukwiba kila wakati wanabuni namna ya kuiba! huwezi kuwa na Bureau - De Change hazina mguu wala kichwa kina kona, na huwezi kuruhusu uhuni unaofanywa na makampuni ya kigeni! eti uko nchini lakini ukienda kununua bidhaa lazima ulipe kwa USD, this is crazy!

  Where is BoT? What is our money doing in our country? Tunafurahishwa na hili jamani au ndo kila mtu anakula kivyake, hata kama ni hivyo lakini at some point lazima tuheshimu nchi yetu na vitu vyetu.

  Money is one of our National Symbol. Agrrrrrrrrrrrrrrrr!!
   
 3. B

  Bucad Senior Member

  #3
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sijaona jipya bado sababu shilingi yetu ni sawa na mfa maji kamwe haishi kutapatapa!
   
 4. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  ni kwa kiasi gani hizi Bureau De Change zimeathiri shilingi yetu
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Siyo kweli nimetoka kuuza dola kwa TZS 1,617 sasa hivi
   
 6. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,314
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Craaaaaap!!
   
 7. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  shilingi yetu ndo chanzo kikubwa cha bei kubwa ya MAFUTA...! halafu ati gavana ni prof. ...crap..! shilling inge stabilize mafuta yangeshuka saana tu bei ..! MAGAMBA HOVYOOOOOOOO...!

  " tukimchagua tena kikwete kuongoza nchi hii litakuwa janga la kitaifa" Dr W Slaa
   
 8. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  umeuza sehem ngap?

  hio ya Bloomberg ni wastani
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  hatuna coordination za taasisi zetu zinazogusa uchumi moja kwa moja,bei ya mafuta inashushwa na Ewura then kupandishwa ghafla sababu ya depreciation of Tsh! Fun enough our monentary system inaguswa direct na BOT!
   
 10. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Itakuwa imepanda ki'Masebu'!
   
 11. G

  Godwine JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  watu wengi hawajui tatizo letu ni nini? kuna kiwango kikubwa cha fedha kwenye mzunguko kuliko ilivyotakiwa hii ni sababu ya kutoweza kutawala kiwango cha fedha kwani kuna noti za aina mbili na wahusika wameacha fedha nyingi katika mzunguko kuliko kiwango kinachotakiwa
   
 12. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  kama kawaida yao watajitetea kuna mawasilaino kati ya izo taasisi mbili

  Fiscal na Monetary zinaendeshwa na wanasiasa hapa kwetu

  mtaalam anampigia magoti politician suggest anything and i will make it legal
   
 13. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  sina uhakika na hili la fedha zilizopo kwenye mzunguko ni nyingi kuliko uhitaji. kwani hata kushuka kwa thamani kwa fedha yetu hamna taasisi iliyogusia kwamba tatizo ni mzunguko wa fedha kuto'balance'

  ila nami lanishangaza kutumika kwa fedha mbili zenye thamani sawa kwa karibu mwaka sasa
   
 14. G

  Greard Member

  #14
  Aug 20, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  yote hiyo ni kwasababu Ewula wanataka kushusha bei ya mafuta kdg. Wanataka wapate sababu maana kelele za watu (nguvu ya uma)
   
 15. b

  babap Member

  #15
  Aug 20, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  labda ungesema pesa nyingi ambayo ni haramu au feki imezidi kwenye mzunguko ningekuelwa.
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Godwine,

  Nafikiri wewe ndio hujui tatizo liko wapi katika sarafu ya nchi hii. Kusema kuwa kiwango cha pesa kiko katika kiwango kingi katika mzunguko pekee ndio sababu ya kushuka sarafu nakukatalia kwasababu serikali muda maalum wa kuzitoa pesa katika mzunguko. Huo muda tukaja kuambiwa umeondolewa kwasababu zile pesa zilizoletwa mpya zina walakin sijui serikali ina msimamo gani sasa katika sarafu za zamani na sarafu za sasa. Na ikiwa mzunguko wa fedha ni mkubwa serikalini kwanini basi benki kuu inaendelea kuuza treasury bonds na bills zake kwa bei ya chini badala ya kupandisha bei ya Tbills and bonds at high prices ili kupandisha interest rate on loans nchini na kupunguza kiwango cha pesa katika mzunguko. Vile vile kuna njia mbali mbali BOT inaweza kusaidia mzunguko wa pesa kupungua na BOT wameshindwa kuzuia kuanguka kwa shillingi nchini.

  Sababu za kushuka sarafu ya Tanzania kwa ninavyoona mie:-
  a. Kuzidi ama kuongezeka kwa matumizi ya foreign currency nchini. Tanzania ndio nchi inayoongoza East Africa kwa watumiaji wake account katika benki za biashara zinazomilikiwa in foreign currencies. Dollar inatumika kama sarafu ya kulipia bidhaa mbali mbali kama kodi ya majengo, school fees, TRA, na kadhalika. Demand ya fedha za nje ikipanda basi demand ya sarafu yako ya madafu itashuka na ndio hali halisi ya kinachoendelea nchini. Watu wanamiliki dollars kuliko Tshs na matokeo yake shillingi inakosa mwelekeo.

  b. Kupandisha mshahara bila kuangalia kiwango cha ukuaji wa uchumi. Mishahara imekuwa ikipanda na kusababisha purchasing power iongezeke na kuongeza mzunguko wa fedha katika nchi. Serikali imekuwa ikipandisha mishahara kiholela pasina kuangalia athari zake katika uchumi na sarafu ya nchi. Watu wakiwa na hela nyingi mfukoni gharama za maisha zinapanda, gharama za maisha zikipanda gharama za uzalishaji zinapanda. Vyote hivi vikipanda matokeo ni sarafu inaporomoka kwani mahitaji ya pesa yanakuwa machache ila upatikanaji wa fedha unakuwa mkubwa na matokeo tunayaona kwani mkate sasa unaweza kununua mpaka Tshs 2000 kutoka Tshs 250 by average.

  c. Ufisadi nao umechangia kuporomoka kwa sarafu yetu kwasababu pesa zinazoibiwa zinasafirishwa nje ya nchi. Mfano thamani ya Shilling miaka 2004-2005 iliporomoka kwa kiwango kikubwa (chukua Excel Sheet ya BOT uangalie mwenyewe). Pesa zinazosafirishwa nje ya nchi zinabadilishwa na Tshs na matokeo bei ya fedha za kigeni inapanda.

  d. Kukosekana kwa sheria ya kuzuia speculative behavior kutoka kwa currency traders, business personell na benki za biashara. Kama umeangalia tofauti ya bei ya USD BOt na Commercial banks utagundua kuna dalili ya speculations inafanyika kwa baadhi ya wadau wa sekta husika. Mfano jana thamani ya British pound BOT ilikuwa 2670 wakati NBC walikuwa wanauza 2780 na CRDB wakiuza 2735. Difference hii ni kubwa na inaumiza kwa baadhi ya wafanyabiashara. Mfano mtu kama Bakhressa akitaka kununua £1,000,000 kutoka CRDB atalipa Tshs 2,735,000, 000 na NBC atalipa Tshs 2, 780,000,000 na benki za biashara zitalipa Tshs 2,670,000,000 kuna tofauti ya karibu millioni 100 benki za biashara zinapata kutokana na kulangua bei ya sarafu ya kigeni. Ukienda bureau de change ndio kabisa kwanza utakuta wanazipoteza katika mzunguko kupandisha bei ya fedha za kigeni na ukizipata utauziwa bei ghali. Hizi tabia ni hatari kwani kutokana na speculation hii anayeumia ni mtumiaji kwani bakhressa atauza kwa bei ya juu kurudisha gharama zake na matokeo mfumuko wa bei.

  Kinachotakiwa kufanyike jitihada za haraka kuikoa sarafu wapunguze mzunguko wa fedha kama unavyoshauri ila vile vile wapunguze matumizi ya fedha za kigeni nchini mwetu. Kulipwa watu mishahara in foreign currencies, school fees kulipwa in foreign currencies, nyumba unalipia kodi kwa foreign currencies vyote ni hatari kwani thamani ya shillingi inaonekana haina maana. Vyenginevyo tuvumilie tu na tumsikilize gavana wetu anayesema sarafu kushuka ina faida wakati hata kiatu hatuuzi nje ya nchi. Bidhaa tunazouza nje ya nchi hatuna hata sauti ya kupanga bei mwishoe tunaumizwa na sarafu dhaifu na mapato dhaifu. Nilikuwapo!!!
   
 17. G

  Godwine JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kuna vitu lazima kujadili kuna mfumuko wa bei(inflation) na kushuka kwa uwiano fedha(exchange rate) hivi vitu kuna wakati vinaendana na kuna wakati kila kimoja kinaenda njia yake

  shillingi ya tanzania imeshuka thamani kutokana na kuwepo kwa fedha nyingi kwenye mzunguko na hii imepelekea watu wanaozimiliki fedha hizi kutaka kuzibadili kwenda kwenye mfumo wa fedha zingine kwa kuhofia kushuka kwa dhamani ya fedha yetu siku za baadae.

  pia kipindi cha migongano ya wafanyabiashara wa mafuta kulikuwa na kutoelewana kati ya serikali yetu na wafanyabiashara wa mafuta na kampuni nyingi za uagizaji za mafuta walikuwa katika shaka kuhusu kuendelea na biashara ya mafuta katika tanzania na ilipelekea ubadilishwaji mkubwa wa dhamani za makampuni haya kwenda kwenye fedha za kigeni na nyingi za fedha hizi walizitum makoa makuu ya makampuni haya yani nje ya nchi hii imepelekea pia kuondoa fedha nyingi za kigeni nchini hivyo imepelekea mahitaji yake kuongezeka

  sipingi sababu zingine lakini sababu ya kuwepo kwa fedha nyingi kwenye mzunguko na kuondoshwa kwa fedha nyingi na makampuni ya kigeni ya mafuta na mitandao ya simu ndio inayopelekea tatizo ili kuwa kubwa
   
 18. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  nashangaa pale mlimani city kuna maduka yanauza bidhaa kwa dola! Kila nikipita kwenye lile duka karibia na shoprite huwa napandwa hasira!
   
 19. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  bot waache kujifungia maofisini tu,watoe changamoto kwa taasisi zingine kufatilia matumizi ya dola kinyume cha sheria,polisi,Tra,takukuru,social funds n.k wasaidie kufatilia ktk maeneo yao.nafikiri BOT haijajipanga vizuri.
   
 20. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  hii nchi usanii umezidi,wanasiasa wanatoa matamko kuridhisha raia tu,mfano BP wamefungiwa lakini upo ushahidi bado wanauza! Nani anafatilia? Tumeridhika? Kuna wanahabari wanaofatilia utekelezaji wa haya?
   
Loading...