Tz na kilimo kwanza

Mkwaruzo

JF-Expert Member
Feb 21, 2011
563
98
Mvua ndiyo hizi. Ni mategemeo yangu kuwa wakulima tumeipokea kwa mikono miwili na kuifurahia sana. Kwani ni matarajio yetu kuwa baada ya miezi kadhaa tutavuna mazao kedekede kutokana na mbegu tutazopandikiza ktk mashamba yetu. Lakini kwaku kuasana siyo vibaya, napenda kuitumia fursa hii kwa wakulima wenzangu. Haitopendeza kama mbegu zako utazipanda katika shamba ambalo siyo la kwako, kufanya hivyo ni kumdhulumu mwenye shamba kwani na yeye anafurahia apande akipendacho. Pia kuna mashamba ambayo siyo rasmi kupandwa mazao yeyote, hivyo tahadharini na kufanya uvamizi katika mashamba hayo, sheria kali zitachukuliwa kwa watakaokiuka agizo hili. Pia umakini uwepo ktk upandaji wa mbegu hizo, kwani haifurahishi kuona zinapandwa kinyume na inavyotakiwa. Pia natoa nasaha zangu kwa wale ambao hawana mashamba, wafanye haraka kwenda kuyanunua na kwa wauzaji wapunguze gharama za uuzaji. Mwisho kwa yale mashamba ambayo yapo tayari, basi inabidi yatendewe haki pia yatunzwe ili yasije kuvamiwa na magugu yakaja kugeukwa msitu. Jamani ni wajibu wetu kuitendea haki kauli mbiu ya Tz ya KILIMO KWANZA.
Ni hayo tu.
 
MMU ishageuka kilimo kwanza!!!

haya jamani wadau thread ndio hiyo!!!
 
susy umeibiwa, huyu anazungumzia kile kilimo chetu kileeee, enhe hicho hicho
 
susy umeibiwa, huyu anazungumzia kile kilimo chetu kileeee, enhe hicho hicho

aahhhhhhh!!! nilishapandisha mori ati!!!

Mkwaruzo uwe basi unawekaga hata aya ili zituvutie kusoma japo thread yenyewe si ndefu sana, ila inahitaji akili za ziada!!

Kama si Gurta hapa ningekuwa nishafeli mtihani tayari!!

Haya jamani msio na mashamba mje mnunue mie nauza langu ila kwa bei ya Harmer!!!!
 
Mh, humu ilikuja thread ya miliyo ya gari, mi nilifikiri tupo gereji siku hiyo. Ila sawa, siku nyengine nitaweka vikorombwezo kidogo.

Na unasema shamba lako unaliuza kwa bei ya hermer, kama utakosa mteja nikopeshe mm ila nitakulipa kwa installment. Si unajuwa kuwa na mm natafuta?
 
Kwa mkopo tena ? sasa huo si ndio usharobaro/umarioo unaopigwa vita kila kukicha ? wasikusikie Sarafina na Sweetdada.
 
Kwa mkopo tena ? sasa huo si ndio usharobaro/umarioo unaopigwa vita kila kukicha ? wasikusikie Sarafina na Sweetdada.

Acha basi nizichange. Muhimu shamba nilipate tu tena kabla ya mvua kumalizika. Kwasababu vipando vyengine vinahitaji baridi, naomba nipate shamba kabla ya mvua kuisha.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom