Gazeti la mwananchi la tarehe sita septemba,ukurasa wa kumi lina habari nzuri sana. Kumbe kuna jamaa/majangiri wanakamata vinyonga wenye pembe moja kichwani na kuwauza kwa dola 60 mpaka dola 100 kwa njia haramu. Vinyonga hawa wanapatikana Uluguruni tu hapa duniani ( hata home kwetu wapo), kabla hujashangaa sana na kinyonga huyo, Mvomero kuna vipepeo wa pembetatu (sijui wanafananaje) na jamaa wanapiga dili kiaina, kuna nyoka wanazaa huko milima ya Usambara,na wanakaa ktk mti mmoja kama nyumba zao.
Sasa ni wakati wa sisi kushiriki ktk kufaidi hizi fursa tulizopewa bure na Muumba.
Sasa ni wakati wa sisi kushiriki ktk kufaidi hizi fursa tulizopewa bure na Muumba.