TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 5,723
- 10,232
Picha: Tyson Nduguru
Ndugu yetu tokea alivyotoka nyumbani kwake siku ya ijumaa ya tarehe 26/05/2023 hajarudi wala kuonekana nyumbani kwake hadi dakika hii tunapoandika tangazo hili.
Muda wote huo juhudi za kumtafuta zimekua zikiendelea lakini bado hatujafanikiwa kupata taarifa yoyote inayomhusu mpaka sasa maana hata simu zake za mkononi zote hazipatikani.
Mkewe na familia yake inamtafuta. Wafanyakazi wenzake nao wanamtafuta na sisi marafiki zake tunamtafuta.
Tunaomba ushirikiano kwako wewe unayesoma ujumbe huu wa hali na mali ili tuweze kumpata mwenzetu akiwa salama. Taarifa zimeshatolewa kwenye mamlaka husika. Juhudi zimefanyika na zinaendelea kufanyika tumekuja kuomba juhudi za pamoja zaidi.
Tafadhali tusaidie kusambaza taarifa hizi. Ukipata taarifa yeyote tafadhal piga namba hizi.
Mawasiliano
0694644530
0625634902
0655642321
---
UPDATE:
Tyson Ndunguru apatikana akiwa salama
Picha: Tyson Nduguru
Picha: Tyson Nduguru
Kufuatia taharuki kuibuka baada ya kijana Tyson Nduguru ambaye ni rafiki wa karibu wa Joel Misesemeko (MC Joel) aliyefariki siku chache zilizopita , kutoweka ghafla tangu kutokea kwa kifo cha MC Joel.
Taarifa zilizotolewa na ndugu, zinaeleza kuwa tayari Ndunguru amepatikana akiwa hai na familia hiyo inawashukuru wote walioshiriki kumtafuta vikiwemo vyombo vya habari.
Source: Globaltvonline