Tyson Ndunguru rafiki yake MC Joel wa (Tyzee SwahiliHood) aliyedaiwa amepotea apatikana

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,721
10,224
FB_IMG_1685505639892.jpg

Picha: Tyson Nduguru
Pichani ni ndugu yetu/rafiki yetu anayefahamika kwa jina la TYSON NDUNGURU maarufu mtandaoni kama Tyzee SwahiliHood.

Ndugu yetu tokea alivyotoka nyumbani kwake siku ya ijumaa ya tarehe 26/05/2023 hajarudi wala kuonekana nyumbani kwake hadi dakika hii tunapoandika tangazo hili.

Muda wote huo juhudi za kumtafuta zimekua zikiendelea lakini bado hatujafanikiwa kupata taarifa yoyote inayomhusu mpaka sasa maana hata simu zake za mkononi zote hazipatikani.

Mkewe na familia yake inamtafuta. Wafanyakazi wenzake nao wanamtafuta na sisi marafiki zake tunamtafuta.

Tunaomba ushirikiano kwako wewe unayesoma ujumbe huu wa hali na mali ili tuweze kumpata mwenzetu akiwa salama. Taarifa zimeshatolewa kwenye mamlaka husika. Juhudi zimefanyika na zinaendelea kufanyika tumekuja kuomba juhudi za pamoja zaidi.

Tafadhali tusaidie kusambaza taarifa hizi. Ukipata taarifa yeyote tafadhal piga namba hizi.

Mawasiliano
0694644530
0625634902
0655642321

---

UPDATE:

Tyson Ndunguru apatikana akiwa salama

1685627092754.png

Picha: Tyson Nduguru

Kufuatia taharuki kuibuka baada ya kijana Tyson Nduguru ambaye ni rafiki wa karibu wa Joel Misesemeko (MC Joel) aliyefariki siku chache zilizopita , kutoweka ghafla tangu kutokea kwa kifo cha MC Joel.

Taarifa zilizotolewa na ndugu, zinaeleza kuwa tayari Ndunguru amepatikana akiwa hai na familia hiyo inawashukuru wote walioshiriki kumtafuta vikiwemo vyombo vya habari.

Source: Globaltvonline
 
Angekuwa na mwili mdogo mdogo kama yule diwani wa Kawe tungejua yupo kwa mchepuko ila huo mwili wake looks sio mtu wa michepuko.(joking usitoke povu)

Any way apatikane kwa haraka akiwa mzima wa afya.

Nyumbani kwake ndio wapi tangazo halisemi kuhusu location!!
 
Ijumaa alitoka kwake kuelekea wapi? Kazini (kazi maalum) ama kwenye mishemishe? anafanya kazi gani?

Mkewe hana ABC kuhusu jamaa, kiasi kwamba unaweza tilia shaka jambo fulani? mfano kama alikuwa akipata jumbe ama simu zisizo za kawaida? huenda kuna kitu kidogo tu anafahamu.

Je, ni mtu wa starehe na muhudhuriaji wa nyumba za starehe? mpenda company za marafiki? kazi zake zinahusisha kusafiri mara kwa mara?

Mara ya mwisho simu yake ilipatikana (kuwa hewani) lini, kabla ya kutokupatikana kabisa? na kama aliongea ama kutuma ujumbe wa SMS alikuwa katika hali gani?

NB
Mkewe kwa 65% atawapa mwongozo wa kumpata ama kujua nini kinaendelea walau kwa % chache.
 
Taarifa au tangazo hili linatia ukakasi clues zote muhimu hazijawekwa kwa maana ya kazi anayofanya lakini pia location upotevu umetokea maeneo gani au mkoa gani generally?
 
TYSON NDUNGURU AMEPOTEZWA NA NANI?

Pichani ni ndugu anayefahamika kwa jina la Tyson Ndunguru maarufu mtandaoni kama Tyzee SwahiliHood. Tangu atoke nyumbani kwake Ijumaa tarehe 26 Mei 2023 hajarudi wala kuonekana nyumbani

Juhudi za kumtafuta zinaendelea lakini bado hakuna taarifa yoyote inayomhusu mpaka sasa na simu zake za mkononi hazipatikani. Mkewe, familia yake, rafiki zake na wafanyakazi wenzie wote wanamtafuta.

Ye yote akayemuona atoe taarifa kwa nduguze kupitia namba: 0694644530; 0625634902 na
0655642321 au atoe taarifa Kituo cha Polisi. Taarifa za kupotea kwa Ndunguru zimetolewa na Mariam Mbano muda mfupi ulipita. Tyson Ndunguru (Tyzee Swahili Hood), uhambi kooki
 
Mungu afanye wepesi
 
Angekuwa na mwili mdogo mdogo kama yule diwani wa Kawe tungejua yupo kwa mchepuko ila huo mwili wake looks sio mtu wa michepuko.(joking usitoke povu)

Any way apatikane kwa haraka akiwa mzima wa afya.

Nyumbani kwake ndio wapi tangazo halisemi kuhusu location!!
Mkuu kwaio sisi wenye miili hatupendi tamu tamu....
Fafanua mkuu..
 
All in all Kuna ndugu wa rafik angu alikuaga ni mtu wa graphics sana akapotea...
Mpaka alizikwa na city ilikujaa kujulikana baadae sana alikua anavuka barabara akagongwa na gari na kupotezaa maisha....

Hakuwa na Id yeyote Wala doc yeyote na hakutoa taarifa kua alikua ame enda wap yaan NDIO ivyo bwana.....

KIFO KIPO BUSY AKISUBIRI TUMALIZE MISHE MISHE
 
Back
Top Bottom