TYD yatoa fursa kwa wabunifu

tyd

Member
May 22, 2018
6
2
1523975739.jpg


"TYD Innovation Incubator ikiwa kama mdau anayependa kuchagiza maendeleo endelevu ya
viwanda nchini Tanzania kupitia ubunifu na wabunifu wa ndani ya Tanzania na Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania, imeonelea kuwa sasa ni muda muafaka wa kukaribisha mtu yeyote na zaidi ni kijana, ambaye ana wazo la kiubunifu". Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Incubator hiyo Bwana Geofrey Chami, siku ya Jumanne tarehe 17 Aprili, 2018 wakati anatoa taarifa kukaribisha wabunifu wapya.

Imeelezwa kuwa, TYD inatambua changamoto ambazo jamii yetu inakumbana nazo, na pia inatambua changamoto ambazo wabunifu wa kitanzania wanakumbana nazo wanapohitaji kurasimisha ubunifu wao kuwa jawabu la matatizo ya jamii zetu. Na ndiyo maana ikaanzisha mfumo wa kupokea mawazo ya kiubunifu na majawabu yake kisha yenyewe kuwa sehemu ya kurasimisha majawabu hayo kwa ajili ya kusaidia jamii ya kitanzania, tena katika kipindi hiki ambacho sera kubwa ya Taifa ni ukuaji wa uchumi wa viwanda.

TYD ambayo ilianza rasmi mwaka jana (2017) kwa Rasilimali ndogo sana za Watanzania wenye nia ya kusimamia ubunifu bila ya kutegemea pesa za wahisani au wawekezaji, mpaka sasa imefanikiwa kukamilisha miradi midogo miwili ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), na iko mbioni kukamilisha miradi mingine miwili, kisha itaanza utekelezaji wa miradi yake mikubwa ambayo imo kwenye mipango ya muda mrefu. Hayo yote yalifanyika kwa ajili ya kuifanya “Incubator” hiyo iwe na kitu cha kuonesha kabla ya kukaribisha wawekezaji au wafadhili ambao tayari wameshaanza kuonesha nia ya kuongeza nguvu, lakini pia kuiwezesha kuingiza kipato cha kujiendesha.

Hivyo TYD imewakaribisha watu wote wanaohisi kuwa ni wabunifu, kwanza kwa kuwasilisha wazo la kiubunifu, kujiunga na taasisi na kisha kutengeneza jawabu la wazo hilo kwa kushirikiana na wataalamu wengine waliopo tayari.

Vilevile, endapo wazo husika litahitaji uwekezaji wa kifedha zaidi, TYD itawavutia wawekezaji na wafadhili na hivyo kugeuza wazo husika kuwa biashara ambayo mleta wazo atanufaika nalo katika kipindi chote ambacho wazo husika litakuwa likitumika kama jawabu la kutatua changamoto fulani kwenye jamii yetu.

Bonyeza hapa kutuma wazo lako
 
Karibuni kwenye fursa hii
Hii safi sana. Itasaidia kunyanyua vijana wabunifu wa kitanzania.
Ila swali langu kwenu: Wabunifu watajihakikishiaje kuwa hamtatumia mawazo yao ya ubunifu kwa maslahi yenu wenyewe na kuyatumia mawazo hayo kama vile ni ya kwenu? Kuna makubaliano yoyote mnayoingia na hawa wabunifu??
tyd
 
Hii safi sana. Itasaidia kunyanyua vijana wabunifu wa kitanzania.
Ila swali langu kwenu: Wabunifu watajihakikishiaje kuwa hamtatumia mawazo yao ya ubunifu kwa maslahi yenu wenyewe na kuyatumia mawazo hayo kama vile ni ya kwenu? Kuna makubaliano yoyote mnayoingia na hawa wabunifu??
tyd
Ndio yapo.
Karibu
 
Back
Top Bottom