Suala la ajira na mishahara wakati wa JK mimi naweza kuwa shahidi mzuri manake niliona haya mambo kwa macho yangu baada ya kuwa nimeajiriwa na NMB 2 years earlier.Kweli kabisa, maana huyo aliyekuwa anatumbua lakini wafanyakazi alikuwa akiwalipa, wa vyeti feki wote walikuwa wanalipwa, nyongeza za mishahara zilikuwepo, ajira kibao, mikopo ya wanavyuo kama kawa. Sasa huyu mbona yanamshinda pamoja na kubana matumizi???
Enzi za Mkapa unaweza kupita hata mwaka bila kufungua akaunti yoyote ya mfanyakazi. Mkwere alipoingia madarakani ikawa kufungua akaunti za wafanyakazi wa serikali ni shughuli za kila wakati na mara kwa mara mnafungua kwa makundi manake unakuta manispaa imepokea wafanyakazi angalau 50 kwa mkupuo!
Kwenye mishahara sasa! Nakumbuka siku ya kwanza tunaingiza mishahara ya wafanyakazi kwenye akaunti zao (officially), walimu wa certificate wanaonza kazi walikuwa wanalipwa Sh. 60,100 na hiyo ilikuwa 2006.
Yaani hapo hata ukizingatia suala la inflation, bado utakuta hivi kawaacha wakiwa wanalipwa zaidi ya mara 3 ya alivyowakuta!
Yote 9, kumi studying opportunities! Kama kuna mtumishi wa umma hakuchukua digrii wakati wa JK then I doubt kama atachukua tena digrii maishani mwenzake!!