Twite atua yanga, mamia wamlaki, simba hawakuonekana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Twite atua yanga, mamia wamlaki, simba hawakuonekana

Discussion in 'Sports' started by nngu007, Aug 30, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h][TABLE]
  [TR="bgcolor: transparent"]
  [TD="bgcolor: transparent, align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: transparent"]
  [TD="bgcolor: transparent, align: center"]Twite baada ya kutua Uwanja wa ndege akiwa na viongozi wa Yanga[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR="bgcolor: transparent"]
  [TD="bgcolor: transparent, align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: transparent"]
  [TD="bgcolor: transparent, align: center"]Shabiki wa Yanga Babu Ally, akiwa na jezi ya Rage na4[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR="bgcolor: transparent"]
  [TD="bgcolor: transparent, align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: transparent"]
  [TD="bgcolor: transparent, align: center"]Twite akizungumza na Waandishi huku amevaa jezi namba 4 yenye jina Rage[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
  [TABLE]
  [TR="bgcolor: transparent"]
  [TD="bgcolor: transparent, align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: transparent"]
  [TD="bgcolor: transparent, align: center"]Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya Yanga, Francis Kifukwe kushoto akiwa Uwanja wa Ndege na kigogo wa Usajili, Seif Ahmad 'Magari'[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Na Mahmoud Zubeiry


  BEKI mpya wa Yanga, Mbuyu Twite ametua Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere na kulakiwa na mamia ya wapenzi wa klabu hiyo, kabla ya kupakiwa kwenye gari kuelekea makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.


  Hakuna kiongozi yeyote wa Simba wala askari polisi aliyemsogelea kama ambavyo kulikuwa kuna tishio kwamba akitua tu beki huyo wa kimataifa wa Rwanda, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watamkamata kwa tuhuma za kuwatapeli dola za Kimarekani 30,000.

  Inadaiwa, kabla ya kusaini Yanga, Twite aliyekuwa akichezea APR ya Rwanda alisaini Simba na kuchukua dola 30,000.

  Hata hivyo, baadaye mchezaji huyo alighairi na kuamua kwenda Yanga na kurudisha fedha za Simba kupitia viongozi wa APR na St Eloi Lupopo ya DRC, ambazo zilikuwa zinammiliki kwa pamoja mchezaji huyo.

  Lakini viongozi wa Simba waligoma kupokea fedha hizo ingawa viongozi wa APR na Lupopo walifika hadi ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka kuzikabidhi fedha hizo, ili Simba wakazichukulie hapo.


  Twite aliianza kuichezea Yanga wiki iliyopita ilipokuwa Kigali, Rwanda kwa ziara ya wiki moja lakini alishindwa kurejea na wenzake Jumatatu kwa kile kilichoelezwa anakamilisha kuhama kwake rasmi na kuja kuanza maisha mapya Dar es Salaam,

  Lakini upande wa pili, Simba SC waliamini beki huyo amekwepa kukamatwa kufuatia kuvuja kwa habari za mpango wa kumtegea akitua nchini wamkamate.

  Ametua na amekwenda Jangwani, maana yake jaribio la kumkamata akitua limefeli na sasa tusubiri kama Simba watamuwekea mtego mwingine.


  Chanzo: Binzubery blog
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nchi Yetu basi tu... Nyerere hakutupa TV na Mambo ya ANASA mapema... SISI tukaangukia kwenye MICHEZO; Angalia

  tunavyopenda Mpira wa MIGUU Tuna MOYO HASWA... KENYA, UGANDA na NCHI zote za Afrika Mashariki wanaona

  DONGE... Na hatufanyi vizuri saaaana...
   
 3. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  timu yenye mwenyekiti mwanasiasa itaendeshwa kisiasa na timu ya mwenyekiti mfanyabiashra itaendeshwa kibiashara
   
 4. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  hao polisi mbona wamemzunguka 2bila kumkamata,au hawna taarifa zake!!!
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Na timu yenye mwenyekiti fisadi itaendeshwa kifisadi fisadi..
   
 6. Jaslaws

  Jaslaws JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 5,129
  Likes Received: 2,186
  Trophy Points: 280
  2meona wangapi??asamoah,mwape na wengne kbao wako wapi??yangu macho..sie ngoja 2jifue for champions league,nyie komaeni na twitta.
   
 7. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,732
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  timu ya mwenyekiti msomali itaendeshwa kwa kujilipualipua kama alshababu
   
 8. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,732
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  twite kafata kuchukua kombe la kagame hataki hadithi za champion league wakati hata kagame umebakiza historia tu.
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Sawa mbuyu kaja Yanga mimi njaa yangu ni vikombe Afrika, lini tutabeba ushindi wa Afrika?
   
 10. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Naitakia kila na kheri timu yangu pendwa yanga
   
 11. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kaja na mipira iliyoachwa Rwanda?
   
 12. Jaslaws

  Jaslaws JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 5,129
  Likes Received: 2,186
  Trophy Points: 280
  Kaifksha wapi timu yake?akuna k2 hapo kelele tu za magazeti.
   
 13. g

  gongolamboto JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 509
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Waambie haoe. Wamempokea kwa mbwembwe watamtimua bila mshahara
   
 14. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mshabiki wa yanga toka niko mdogo na nimefurahi huyu jamaa amesign for young africans the best team in east africa lakini kama jamaa kweli alisign for simba alafu akapewa hela zaidi akabadilisha mawazo then thats wrong kisheria anatakiwa ashtakiwe kwenye relevant football authorities., bt we know how the game is played in africa anyways
   
 15. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  unfounded hype .. kama kawaida ya wavaa ndala
   
 17. M

  Maswalala Senior Member

  #17
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maneno ya mkosaji na nikukumbushe tu sikuzote mfa maji hakosi kutapatapa ndo nyie sasa....RAGE OYEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!@@@
   
 18. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hivi Twite kwanini timu yake (Lumpopo FC) ilimpeleka APR kwa mkopo????, Yanga mtakuwa mmeuziwa Mbuzi kwenye Gunia: kama si swala la nidhamu mbovu basi nina wasiwasi na kiwango chake ......mh! yetu macho.
   
 19. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huo wasiwasi wenu umeanza sasa hv baada ya Jamaa ku'sign Yanga, wkt Rage akichukua allowance na hela ya kupiga kambi kule Rwanda kumsainisha mlikuwa na uhakika na kiwango chake,si ndiyo?
  Sasa nyie endeleeni kuwa na wasiwasi naye sisi we have no doubt kuhusiana na kipaji chake cha asili,labda muingize mambo yenu, we know the guy we have seen him playing in the Kagame competition, kwahiyo hatuna shaka naye.
   
 20. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #20
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  ''Anselm'' kumbuka kuna mtu anatamani msichana mara baada ya mwinzie kumu-approach, na tena yuko tayari kupandisha dau la kumpata ili nayeye aonekane hayuko nyuma; that is what happened on Twite's saga: Twite ni wakaida sana'' the rate of 30Millions was quite enough for him, but simply w'have administered and full up with hypocrisy not easy to realize and accept the truth..
   
Loading...