Twiga wetu wa Barrick azidi kurefusha shingo yake, atanuka, anenepa na kuzidi kutanua! Anunua mgodi wa jirani kwa $ Milioni 6, kuinvest $ Milioni 9

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi,

Wale wasoma kizungu, nendeni moja kwa moja jikoni,

Barrick’s Bulyanhulu Acquires Highly Prospective Licences in Tanzania

Kampuni ya Twiga Minerals Corporation (“Twiga”), ambayo ni joint venture kati ya Barrick na serikali Tanzania, kupitia mgodi wake wa Bulyanhulu Gold Mine Limited (“Bulyanhulu”) wameinunua leseni ya prospecting licences ya mgodi wa jirani.

Mkataba wa mauziano hayo umefanyika jana, ambapo mgodi wa Bulyanhulu kupitia Barrick, imenunua leseni ya mgodi wa Tembo Gold Corp. (“Tembo”), inayomilikiwa na kampuni ya Mineral Industry Promotion and Consulting Company Limited (“MIPCCL”), kwa kuzinunua hisa zote 100%, hivyo sasa Barrick ndio inamiliki mgodi huo wa Tembo, kwa kuilipa dola $6 million na Barrick ita invest dola $9 million kuuboresha mgodi huo ndani ya miaka 4!.

Mauziano hayo yatakamika rasmi baada ya Barrick kupata approval of the TSX Venture Exchange, na Tanzania kuridhia.

Rais wa Barrick na chief executive Mark Bristow amesema, ununuzi huo ni muhimu kwa Barrick kuongeza uwekezaji nchini Tanzania.

My Take.
  1. Kwenye ulimwengu wa biashara, "the business world", any acquisition ni healthy ni kukua, na kwa vile Tanzania tunamiliki 16% ya Twiga, upanuzi wowote wa Twiga ni neema kwa Tanzania.
  2. Tuwe makini sana na hawa ma giant kuwanunua wadogo, umiliki wa migodi mikubwa ndio unao control bei ya dhahabu kwa carteling
  3. Japo tulielezwa Makao Makuu ya Twiga yako Mwanza, sijawahi kuona taarifa yoyote ya Twiga, ikitolewa kutokea Mwanza, Taarifa zote za Twiga, zinatolewa na Barrick, kutokea London!, Why?.
  4. Japo tulielezwa kuwa zile zilizokuwa ofisi za Acacia London, zimefungwa na kuhamishiwa Mwanza, ukweli ni kuwa address ya Barrick London ni ile ile iliyokuwa ya Acacia, na Ofisa habari yule yule wa Acacia, bado ndie ofisa habari wa Barrick pale London!.
  5. Tulielezwa hata fedha wana bank na banks za Tanzania, ukweli ni hawa jamaa wana bank na City Bank ya Marekani, ila ina Tawi Tanzania. Lengo la kubank na local bank, ni ili manufaa ya kiuchumimi yanayotokana na hiyo bank, yawafaidie Watanzania, uki bank na a foreign bank ambayo ina tawi Tanzania, faida inakwenda inje kwa banki mama!.
  6. Tulielezwa tutagawana faida za kiuchumi pasu kwa pasu, yaani 50/50, bado nasubiria kwa hamu sana kutolewa taarifa rasmi ya mgoa huo, ambayo inaonyesha Twiga imetengeneza faida kiasi gani, nini kimebaki Tanzania na wao wamepata kiasi gani ili hiyo 50/50 ionekane wazi.
Hongera Twigwa kuzidi kurefusha shingo na kujitanuaa.
Hongera Tanzania na Watanzania kwa mgao wetu wa 16% kuzidi kutuna.
Mungu Ibariki Tanzania.
 
Bongo movie za awamu ya 5 ni noma,hawachelewi kusema wamenunua kampuni ya barrick, ukiwa murongo huwezi kua na akili CCM woyee
 
Uhakika wa Kipato cha Tanzania ni kuachiwa Makorongo na Mazingira Mabovu baada ya hawa watu kumaliza kuchukua kinachochukuliwa na Ukizingatia hivyo visenti vinavyopatikana sasa havifanyi any long lasting projects vitukuu lazima wajiulize mababu zao kama walikuwa wamerogwa
 
Back
Top Bottom