Opaque
JF-Expert Member
- Oct 24, 2008
- 1,359
- 732
Kama wana Mtwara wanadhani viwanda vikijengwa huko itazuia watanzania wasioishi huko kupata ajira, basi wamegonga mwamba. Binafsi ninajiandaa kwenda huko kuchukua ajira kutokana na ujuzi na taaluma niliyo nayo, na kuna kundi lingine kubwa tu la vijana tunasubiri ujenzi wa viwanda uanze. Yaani ni kwamba tunakamata ajira kuanzia wakati wa ujenzi hadi uendeshaji wa viwanda. Vijana wahandisi na mafundi mchundo, wachakataji kemikali, wataalamu wa jiolojia na gesi, na mazao ya petrolium, twendeni tukakamate ajira Mtwara kwani vigezo vya ajira ni ujuzi na pengine uzoefu kidogo, wala wakati wa usaili hakuna atakayekuuliza unatokea wapi!