Kwanza inabidi upange vituo viwili kati ya Kashozi na Katerero yaani kituo A na B.

Kwanza utambebesha ngamia ndizi 100 toka kashozi hadi kituo A chenye umbali wa kilometa 20 toka kashozi. Hivyo kati ya hizo 100 njiani atakula ndizi 20 na atafikisha ndizi 80. Basi utaacha hapo kituoni ndizi 60 na kumbebesha tena ndizi 20 ili arudi kashozi kufuata mzigo mwingine.

Kashozi utambebesha mzigo mwingine wa pili wa ndizi 100 kwenda kituo A. Njiani atakula ndizi 20 na atafikisha ndizi 80. Hapo hapo kituo A utashusha ndizi 60 na kumwacha arudi na ndizi 20 kumalizia zilizobaki 100 kule kashozi. Safari ya tatu Katika mzigo wa ndizi100 zilizobaki huna haja ya kumbebesha zote, mbebeshe ndizi 96 kati ya 100 na atakula njiani ndizi 20 na kufikisha ndizi 76 kituo A. Jumla ya kituo A zitakuwa ndizi 196 yaani 60 + 60+76 na Kilomita 80 zitakuwa zimebaki kufika katerero.

Basi utafanya kituo kingine B ambacho ni kilometa 33 toka kituo A. Mzigo wa kwanza utaweka ndizi 100 kati ya zile 196. Ngamia atakula njiani ndizi 33 njiani na kufikisha kituo B ndizi 67. Basi utaacha hapo kituo B ndizi 34 na kupandisha tena ngamia na ndizi 33 ili ale njiani akirudi kumalizia zile 96. Safari ya mwisho toka kituo A kwenda B.. ngamia atabeba zile ndizi 96, atakula njiani ndizi 33 na kufikisha kituo B ndizi 63 ambazo ukijumlisha na zile ndizi 34 za mwanzo zitafanya jumla ya ndizi 97 huku safari ikiwa imeenda kilometa 33 + 20 = 53 na kubaki na kilometa 47 kufika katerero.

Basi safari ya mwisho itakuwa kutoka hapo kituo B kwenda gulioni katerero ambako ni umbali wa kilomita 47 kutoka kituo B. na utambebesha zile ndizi 97 zilizobaki. Njiani ngamia atakula ndizi 47 na kufikisha gulioni ndizi 50.