Twendeni Chalinze waungwana

Twendeni Chalinze waungwana

Rose Kamili akamatwa na Polisi kwa kugawa rushwa Kalenga!


Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Manyara kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo amekamatwa leo na Polisi katika Kata ya Luhota kijiji cha Kitawaya akigawa pesa (rushwa) kwa wapiga kura wa jimbo la Kalenga.


.............................. .................


By nngu007
SATURDAY, MARCH 15, 2014














Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Bi.Jesca Msavatavangu akizungumza na wanahabari jioni ya leo mara baada ya tukio hilo la kukamatwa kwa Mbunge wa CHADEMA akigawa fedha kwa wanakijiji siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika. Uchaguzi wa Jimbo hilo unatarajiwa kufanyika kesho siku ya jumapili, ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.


Ikiwa imebaki siku moja kabla ya uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh.Rose Kamili amekamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota, Iringa Vijijini kwa tuhuma za kugawa Fedha kwa wanakijiji hao, akijua fika Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.


Pichani shoto ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Rose Kamili akielekezwa sehemu ya kupita wakati wakiondoka ofisi za makao makuu ya CCM mjini Iringa jioni ya leo,akituhumiwa kukutwa akigawa fedha kwa Wanakijiji wa Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini,ambapo Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.


Mbunge huyo wa Chadema akipakizwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi kwa taratibu nyingine za kisheria.


Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh.Rose Kamili akiwa ndani ya gari ya polisi mara baada ya kukakamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini akituhumiwa kugawa Fedha kwa wanakijiji


Gari ya Polisi PT 1895 ikiondoka na mtuhumiwa huyo,mara baada ya kuchukuliwa kwenye makao Makuu ya chama cha CCM alikokuwa ameshikiliwa na uongozi wa chama hicho,kwa taratibu nyingine za kisheria. PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA-IRINGA.






: Michuzi
Attached Thumbnails
 
image.jpg
Rose kamili akiwa chini ya ulinzi wa polisi akipekwa korokoroni
 
image.jpg
Rose kamili baada ya kutiwa nguvuni akigawa rushwa
 
Mkuu Chikaka Sumuni,kama uchakachuaji wa kura utadhibitiwa ipasavyo,CCM hatuna chetu Kalenga. Ripoti za wataalamu wa CCM zinaainisha hivyo. Hadi sasa,CHADEMA inaongoza

Mzee Tupatupa


mkuu mbona wewe unaakili sana kwanini uko huko? Nikiri wewe ndo mwanaccm mwenye akili kuliko wote duniani
 
Last edited by a moderator:
To be honest sitakuepo huko physically lakini najua kuwa kutakuwa na mabadailiko na changamoto kubwa sana, hapa ni mwendo wa pesa na sio hoja. kwa bahati mbaya sana sana nawajua vizuri hawa watu, last time walimchangua Bwana nanihii kwasababu tu eti aliwaletea mipira ya kucheza na kuwanunulia pombe baadhi yao. Huku ile DHANA YA huyu ni mwenzetu ndio inafanya kazi kweli kweli. Huyu ni mtoto wa fulani, mtoto wa mjomba wangu mtoto wa dadake na bibi yangu....hapa ndio nyumbani kwao. Mara ya Mwisho nilikua KIWEANGA-Bagamoyo kwenye msiba wa rafaiki yangu Mpenzi yaani ukiwasikiliza kwakweli wanakatisha tamaa kabisa ya kuishi. ni kama vile wamefikia mwisho wa safari yao na hakuna tumaini tena. Akili zao na kila kitu chao wamemkabidhi mtu mmoja, awajengee shule, awalishe, awanyeweshe na hatimae kuishia kugombana na Jamii ya Wafugaji wao kutwa kucha ni story za hapa na pale na kusifiana kuwa wako kwenye ardhi yenye rutuba nzuri. hawa jamaa walinichosha sana. Samahani kwa kuyasema haya hata kama yatawaumiza baadhi yetu lakini huo ndio ukweli...
MANI na zumbemkuu njooni mnaitwa huku na Mpwa wangu
 
Last edited by a moderator:
Elli mpwa wangu kwa kweli itachukua muda hawa watu kubadilika kama kalenga pamoja na shida zote walizonazo wameamua kuendelea nazo inasikitisha sana.
 
Last edited by a moderator:
Elli mpwa wangu kwa kweli itachukua muda hawa watu kubadilika kama kalenga pamoja na shida zote walizonazo wameamua kuendelea nazo inasikitisha sana.

Sasa wewe na akili yako unaamini katika Chadema ya babu,Mbowe,Lema na Lissu?
 
Back
Top Bottom