Tuzungumze magazeti asubuhi kutoka star TV

murumbasi

Member
Dec 3, 2014
75
0
Ndugu wana JamiiForums. Mimi ni mpenzi wa kipindi hiki lakini ninakwazwa sana asubuhi wakati kipindi kinataka kuanza. Kwanza kipindi hakianzi saa 12.30 asubuhi kama ilivyo kwenye ratiba.

Pili kabla ya kipindi kuanza kuna matangazo mengi yanayotangulia na kufanya kipindi kuanza hata 12.37 na tatu mara nyingi wanaomba radhi kwa kutorushwa kwa kipindi. HIVI NI KWA NINI?.
 

Myamba

Senior Member
Jun 29, 2008
103
170
Nami ni mpenzi wa kipindi hicho na hayo uliyosema ni kweli yapo. Sasa tungoje wahusika watupe ufafanuzi.

Isipokuwa matangazo yanaletwa na wafadhili na huo ndio wakati muafaka wa kuyarusha, maana kabla ya hapo kuna kipindi kingine cha amka na BBC kinachatangulia.
 

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,068
2,000
Ndugu wana jamii Forums. Mimi ni mpenzi wa kipindi hiki lakini ninakwazwa sana asubuhi wakati kipindi kinataka kuanza. Kwanza kipindi hakianzi saa 12.30 asubuhi kama ilivyo kwenye ratiba.

Pili kabla ya kipindi kuanza kuna matangazo mengi yanayotangulia na kufanya kipindi kuanza hata 12.37 na tatu mara nyingi wanaomba radhi kwa kutorushwa kwa kipindi. HIVI NI KWA NINI?.
Mkuu, wadhamini wa kipindi ndio wenye kupindi; hicho kipindi ndicho kinaingiza pesa nyingi RFA maana kina wasikilizaji wengi, na ndio maana kumepata wadhamini wengi.

Vv
 

penhe

Member
Jan 3, 2013
36
95
Mara nyingine kikianza sauti haitoki unakuwa unasikia background ya kipindi cha magazeti cha RFA
 

MZAWA JF

JF-Expert Member
Apr 4, 2014
2,482
2,000
ndo ujue tz tuko nyuma kwn ICT. mawasiliano yanawasumbua mara nyingi cm inakata. ila cjui kwa nn magazet yasiwe yanasomwa kwn internet hadi wapigiane cm toka dar
 

MBATATA

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
544
225
Star TV wana matataizo yao .......fanya uchunguzi utatambua!

1. Mara nyingi mtangazaji hutokea kwenye screen lakini huzungumza bila kusikika...kama katuni fulani hivi (ICT yao bado iko chini mno)

2. Kukiwa na jambo lenye kuikosoa serikali Star TV watachagua gazeti lenye mlengo wa kujikomba kwa serikali ndio kama habari kuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom