dfreym
JF-Expert Member
- Oct 14, 2010
- 342
- 87
Wadau najua kuna thread nyingi tofauti tofauti, ila nimeona nifanye kitu hiki kwani mimi ni mmoja wa wahanga wa luku. ninaishi kwenye nyumba ya kupanga, sina vitu vya kiviile vinavyotumia umeme mkubwa, kwani nina subwoofer watt 250. laptop moja, taa mbili energe server (sebuleni na chumbani) na pasi (ambayo huitumia kunyooshea nguo ninapotaka kwenda kazini, na sio kila siku).
Tuko wapangani wawili, mpangaji mwenzangu ana kiredio kidogo (huwa hakiwashi mara kwa mara japo kinatumia umeme), duka, ndani ya duka kuna friji, taa na huwa anachajisha simu, pia kuna saloon, ina tv, redio na mashine za kunyolea,
Mama mwenye nyumba ana friji, tv, pasi , na ana kimedical chenye taa na feni tu. ila juzi nimesikia kama kanunua brender kwani nilisikia kelele za brenda zikitokea kwake.
Tangu nihamie nina kama miezi mitatu hivi, mwanzoni nilikaa kama mwezi hivi bila kudaiwa hela ya umeme, nilifurahi nikajua hapa si kwenye gharama kubwa za umeme, then baada ya mwezi nikaambiwa umeme umeisha then nitoe tsh. 5000, nikatoa after 15 days, nikaambiwa tena nitoe 5000, ya umeme, nikatoa, sasa mwezi huu(june 2012, tarehe 8), umeme ukakata, nikaambiwa nitoe tena 5000, kishingo upande nikatoa, jana tena (17 june,)umeme ukakata tena, mi sikusema kitu ila nilijikuta natumbukia kwenye dimbwi la mawazo mwenyewe tu, then naambiwa tena hela ya luku 5000, nikaishiwa pozi. SIKU TISA! luku gani hii?
sasa wanabodi hebu tushauriane, tatizo ni tanesco au mama mwenye nyumba? kwani inaonesha huwa ananunua umeme kwa njia ya m-pesa, anajaza mwenyewe, au huwa ananunua wa elfu mbili mbili?
NINGEPENDA KUJUA YAFUATAYO,
1. UNIT @ MOJA HUWA INAUZWA SHILINGI NGAPI?
2. KUNA TOFAUTI GANI KATI YA MTU AKINUNUA UMEME KATI KATI YA MWEZI, MWANZONI AU MWISHONI?
3. KUNA TOFAUTI YOYOTE MTU AKINUNUA UMEME KWA MAX MALIPO AU M PESA?
4. KUNA TOFAUTI YOYOTE MTU AKINUA UMEME WA 25000, KUSHUKA CHINI, NA MTU AKINUNUA UMEME WA SH. 25000 KUPANDA? (INTERMS OF UNITS).
nawasilisha.........