Tuzungumze kidogo kuhusu Supreme Maestro Ndalla Kasheba

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
11,141
20,787
Mwaka huu imetimia miaka 17 tangu tumpoteze gwiji wa muziki mnamo mwaka 2004 na kuzikwa makaburi ya kinondoni. Nataka tujadili uwezo na mchango wa Ndala Kasheba kwenye muziki wa Tanzania.

Kwa kuanza nataka tuwekane sawa kuhusu baadhi ya kazi zake. Mfano wa Kwanza ni Wimbo wa kumuaga mama Maria Nyerere ...mwaka 85. Wimbo huu kuna magita ya solo mawili. Solo ya Kwanza kapiga Ndala na solo ya pili kapiga Nguza. Ni hatari Sana wazee...😄

Karibuni tushee notice.
 
ZAITA Musica. ZAI yaani Zaire ambayo ndiyo DRC sasa na TA yaani Tanzania. Ndiyo bendi yake baada ya kupita bendi kadhaa tangu aingie nchini kutoka kwao.

Napenda kazi zake "marashi ya pemba", " nimlilie nani", "dunia msongamano" , ile aliyokopi Tshalla Muana "dezodezo" , kesi ya kanga". Jamaa alifanya kazi kubwa.
Mwenyezi Amrehemu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom