Tuzo za kimataifa zamnyemelea Godbless Lema

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,778
239,451
Hii ni baada ya ujumbe wake alioutoa bungeni alipokuwa akitoa mchango wake wa kile kinachoitwa mpango wa Taifa wa maendeleo kuvuka mipaka na kutua nchi za nje.

Ikumbukwe kwamba dunia imekuwa ikitumia nguvu kubwa sana katika kutatua migogoro hasa ya Africa inayosababishwa na misuguano ya kisiasa, sasa anapotokea mtu mwenye maono ya utatuzi usio na gharama ya pesa ama umwagaji wa damu basi ni lazima Jumuiya na Taasisi kubwa za kimataifa zitambue mchango wake.

Zipo taarifa zinazoelea duniani zinazodokeza uwezekano wa Mh Lema kupewa Tuzo ya Amani hasa baada ya Taasisi hizo kuguswa na mchango wake alioutoa bungeni.

Taarifa zaidi zinatanabaisha kwamba kushindwa kwa watu mashuhuli na hasa wale wenye ushawishi katika nchi hii kulizungumzia kwa uwazi na ukweli suala la Zanzibar kumewashangaza wazungu wengi!

Kuibuka kwa kijana mdogo sana Mh Lema ambaye dunia iliaminishwa kwamba ni mtu wa fujo na vurugu kulisemea bila kumung'unya maneno suala zito la dhuluma ya Zanzibar tena katika lugha ya kushawishi amani kumewashangaza zaidi wazungu .

Kila la heri Mh Lema, Mwenyezi Mungu ambaye amekuwa tegemeo lako kuu akuongoze katika mkakati wako wa kupigania amani ya nchi yako.
 
Hii ni baada ya ujumbe wake alioutoa bungeni alipokuwa akitoa mchango wake wa kile kinachoitwa mpango wa Taifa wa maendeleo kuvuka mipaka na kutua nchi za nje.hahahahha. lema bahnaa kwa kujipigia promo jf

Ikumbukwe kwamba dunia imekuwa ikitumia nguvu kubwa sana katika kutatua migogoro hasa ya Africa inayosababishwa na misuguano ya kisiasa, sasa anapotokea mtu mwenye maono ya utatuzi usio na gharama ya pesa ama umwagaji wa damu basi ni lazima Jumuiya na Taasisi kubwa za kimataifa zitambue mchango wake.

Zipo taarifa zinazoelea duniani zinazodokeza uwezekano wa Mh Lema kupewa Tuzo ya Amani hasa baada ya Taasisi hizo kuguswa na mchango wake alioutoa bungeni.

Taarifa zaidi zinatanabaisha kwamba kushindwa kwa watu mashuhuli na hasa wale wenye ushawishi katika nchi hii kulizungumzia kwa uwazi na ukweli suala la Zanzibar kumewashangaza wazungu wengi!

Kuibuka kwa kijana mdogo sana Mh Lema ambaye dunia iliaminishwa kwamba ni mtu wa fujo na vurugu kulisemea bila kumung'unya maneno suala zito la dhuluma ya Zanzibar tena katika lugha ya kushawishi amani kumewashangaza zaidi wazungu .

Kila la heri Mh Lema, Mwenyezi Mungu ambaye amekuwa tegemeo lako kuu akuongoze katika mkakati wako wa kupigania amani ya nchi yako.
 
Thread za namna hii ni ishara tosha kuwa ni kweli upinzani Tanzania ulikufa august 2015 (mlipomchukua EL) na kuzikwa rasmi tar 25 October!
hapa hujanidharau mimi wala UKAWA , bali umedharau amani ya zanzibar , kitu ambacho hakitakusaidia chochote , tuliweka angalizo la Dr Magufuli kuongea na wazee wa dsm , kama nakumbuka vizuri ilikuwa nov ama dec , mlitukana matusi yote , lakini leo mmeumbuka .
 
Kwa kweli Nchi za Africa tunaamini katika "SIASA ZA UJIMA" na kuamini siasa ni "UONGO ULIOKITHIRI KUWALAGHAI WANANCHI WAKUPE KURA" lakini kwa maana halisi ni kinyume chake zaidi ni kuwa MTUMISHI WA WANANCHI ANAESIMAMIA UONGOZI BORA WA PAMOJA,HAKI,WAJIBU,UKWELI,MAENDELEO ENDELEVU,USHIRIKIANO NA UPENDO. huku kwetu ukiwa mkweli ni shida kama swala la zenj kila mtu ataongea hili na lile lakini ukweli unajulikana ni UBINAFSI ULIOKITHIRI ni chachu kuu,ambayo imejenga mambo mengi ikiwamo DHULUMA,UONGO,WIZI,HUSUDA,ULAFI,UCHU,WOGA,TAMAA,UNYANGANYI,CHUKI KUU,UBAAZAZI,&^%$$#.....etc.
sasa basi ifike wakati tuwe WAKWELI maana hata vitabu husema "UKWELI HUTUWEKA HURU" na kama hatutaki ukweli basi tukubali ya upande wa pili,siasa za ujima.
 
Back
Top Bottom