Tuzo ya Mwana JF anayepambana na Ufisadi kwa Dhati

Mimi nilikuwa na wazo dogo, kwa nini tusiwe na category kama tatu hivi

1. special talents, commitment on fight agaisnt corruption (Wazee wa nondo za maana)
2. Most commited reporters-Wenye kutumia resources zao to keep us informed on time
3.Member mwenye uwezo mkubwa wa kuchambua maada na kumwaga point za maana on balanced basis

Tuzo, Tunaweza kuwapa kazi MOD wakaongea na asasi za kiraia and NGO'S ili waweze ku sponsor awards but JF itatoa certificates of apreciation
 


Msando, naunga mkono mawazo yako kuhusu mwanakijiji lakini nikuombe gurudumu asiwe mmoja wa watakaopendekezwa kwa tuzo hii. Tuzo hii ni kwa ajili ya mpambanaji mahiri wa ufisadi kupitia JF. Gurudumu hana sifa hiyo kabisa. Samahani sikuisoma hii post jana.

Asante kwa kunielewa mkuu
 

Usiwape nguvu wasizo kuwa nazo. Hawana hizo nguvu pamoja na ufisadi wao. Narudia tena mauti na uzima uu mdomoni mwa mhusika, ukitishiwa nyau ukaingiwa hofu unawapa uwezo wa kutimiza kukiri kwako. Ukiamini na kusimama katika haki hata mawe yatakulinda kama wanadamu watashindwa.
 
Kigezo peke yake kinachoweza kumpima mtu kama ni mpambananji dhidi ya uovu na ukandamizaji ni pale mtu huyu anapokosa mshipa wa wogana anakuwa tayari kusema chochote hata mbele ya muuaji wak. Tanzania tumefika hapa kwa sababu hatuna watu waliokatika mishipa ya woga.

Wapo wanaojaribu lakini baadaye huja kuwagundua kuwa hawawezi kuendelea na harakati zao wakiwa na njaa. Wanaposhikwa na njaa watu hawa huwa wapo tayari kugeuzwa kwa kupewa eti tu chakula. Tumewashuhudia watu waliojiita wanapanduzi lakini baadaye tumekuja kuwaona wakiingia kwenye kashfa ya kuhongwa na watawala na kuanza kulegeza misimamo yao na kwa maara nyingi wamejionyesha wazi kuwasaliti wenzao kwa singizia wamekua na wanfanya mambo kwa busara hivyo wanaweza kukaa tena hata na watu waliowapinga zamani wakaelewana ili hali watu hawa bado wanawanyonya watanzania.

Ni nani aweza kujiita mpambanaji akiwa na tabia hii ya kukosa consistance kwa sababu ya njaaa. Hawa ni watu wabaya kuliko hata wale ambao wameamua kuwanyonya waliowengi tangu mwanzo na kuendelea na msimammo yao. Wanamapinduzi uchwara tuwaogope kama ukoma na hakuna haja ya kuendelea kuwakumbatia, waende kwa wenzao tujue moja.

Tuzo ya uanamapinduzi ni lazima itolewe kwa mtu ambaye ameonyesha msimamo usiobadilika mpaka ukombozi unapatikana.
 
Mwanakijiji,
Unastahili tuzo na heshima hii. Unapambana sio humu JF pekee. Jiulize kwa nini mimi au mwanaJF mwingine hatutajwi! Tuambie tukusaidieje ili uendelee na kazi hii takatifu inayoweza kufanywa na wachache sana humu Tanzania. Hao wanaokupatia hizi taarifa wamekuamini sana kama ambavyo baadhi yetu humu tunakuamini.
 
Naona Mwanakijiji ameungwa mkono na wengi, mimi nikiwa mojawao. Sidhani hilo lina mjadala tena.

Lakini tutaomba mods watuambie ameungwa mkono na wachangiaji wangapi, just for record.

Pengine tujiulize kama ni yeye peke yake kafuzu hivyo vigezo kisha tuamue tena kama tuongeze idadi, jumla wawe wangapi?

Kisha tuamue tuzo yenyewe itaitajwa na ni nini?

Halafu tujiulize kama kutakuwepo na garama za kifedha, zitapatikanaje na nani atazitunza.
 
Mkulima Maskini Mwanakijiji (a.k.a Mzee Mwanakijiji) you are my idol, your are my champion. KEEP IT UP BRODA, I salute you!
 
Malaria sugu labda kama angepewa tuzo ya fisadi mkubwa na mtetezi wa mafisadi........ kisha nyingine angepewa mwiba na kibunango kwa utetezi wa ufisadi! Rest in havoc malaria sugu
 
Jamani tunapotaka kusifu mtu tumpe kwanza angalizo ili kumsifu kwetu kusimpore uwezo wake wa kufikiri na akili...waasisi wa harakati za kutoa elimu ya uraia kwa njia ya kusaidia udadisi wa fikra wasimamie tu mawazo yao mpaka demokrasia ya kweli itakapoanza kuota mizizi na kukomaa katika nchi
 
Mwanakijiji kwa mara nyingine lakini pia asisahaulike Rev. Kishoka nafasi ya pili.
 
1.Mzee mwanakijiji
2.Dr.W.Slaa

These two make a good pair,i think conceptually what they do is like a team and its a winning team!
+ the others i don't know behind the scene
 

Mimi ningempa hii tuzo Invisible au Max Shimba. Kutupatia hii jamii forum mahali ambapo tunaweza kujadili na kupata taarifa za kuhusu huo Ufisadi. Huyo mwanakijiji amepata umaarufu au documents zake huwa zinatufikia kupitia hii jamii forum.

So wa kwanza kabisa kumtambua na kumpatia tuzo hii nafikiri awe Max Shimba. He is just extra ordinary, committed, patriotic, dedicated, ambitious and a truly Tanzanian.
 

nakuunga mkono aisee! phew.. thanks.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…