Tuyaenzi mapinduzi ya Zanzibar( Mapinduzi ya Afro-Shirazi Paty) January 12 ,1964

Abelyon

Member
Aug 17, 2016
31
6
TUYAENZI MAPINDUZI YA ZANZIBAR( MAPINDUZI YA AFRO-SHIRAZI PATY) JANUARY 12 ,1964.

Awali ya yote niwapongeze viongozi na watu wote wa Zanzibar na Tanzania bara ( Tanzania) kwa kuendelea kulinda na kudumisha Mapinduzi ya Zanzibar.

Ni vema zote tukajua kuwa Maandalizi na mipango ya watu wa Zanzibar ya kujikomboa kutoka katika dhuluma na Unyonyaji wa kikoloni na Waarabu ulianza miaka mingi sana kama zilivyo katika mataifa mengine ya Africa.

1.SABABU ZILIZOPELEKEA MAPINDUZI YA 1964.

Kwanza ni kushamiri kwa Dhuluma ya Waingereza na Waarabu dhidi ya Waafrika visiwani Zanzibar, Ambapo Waafrica walibaguliwa kwa rangi yao katika huduma zote za jamii na kutumikishwa katika mashamba ya waarabu na waingereza.

Pili ni Dharau ya serikali ya Mkoloni kugeuza kauli na kuwanyima Afro-Shirazi haki ya kujitawala baada ya kushinda mara kadhaa katika chaguzi mbalimbali tangu wa kwanza wa mwaka 1957 licha ya kutoa ahadi ya atakayeshinda atapewa fursa ya kuunda serikali.

Mwisho ni Matokeo ya Mkutano wa Katiba London wa mwaka 1963 ambapo ASP walikubaliana uhuru upatikane tarehe 10 Disemba 1963 lakini Waingereza wakalazimisha kuwakabidhi HIZBU ( Mwarabu-Sultani) nafasi ya kujitawala licha ya Wazanzibar kukataa katu katu suala hilo.

Matokeo yake ASP wakawa wamenunana kukasirika kutokana uamuzi huo na kubaki na uamuzi kumngojea Mwingereza aondoke, wapambane na Mwamwinyi wa Kiarabu na Sultani wao. "Sasa basi,tutajaribu njia nyingine, na Mwenyezi Mungu atatusaidia."Na matokeo yake kweli baadae walifanikiwa.

2. MIPANGO YA KUTEKELEZA MAPINDUZI.

Baada ya Mkutano wa Pili wa London Kamati kuu ya ASP ilikaa na kusononeka sana kwa matumaini yao ya kujitawala kuzimwa na Waingereza na Waarabu kukubaliana kupeana uhuru.
Kamati kuu ya ASP hatimaye ikatoka na Shauri kwamba baada ya Uhuru huo wa BANDIA, British Resident wakiondoka tu, Basi tushike Mapanga tumng'oe Sultani na hatimaye wote walikubaliana kwa pamoja.

Kamati kuu ikaamu kuu viundwe vikundi mbalimbali vitakavyoelekezwa kwenye kufanikisha Mapinduzo hayo, na kiongozi wa kazi hizo zote akateuliwa SHEIKH ABEID KARUME na Katibu Mkuu wa ASP wakati huo SHEIKH THABIT KOMBO alipewa kazi ya kuwatuliza wanachama kutokana na Uchungu waliokuwa nao wa kurudishwa Utumwani.

Mipango ya Kufundisha vikundi na maandalizi yaliendelea kusimamiwa na SHEIKH KARUME na kwa bahati nzuri zoezi liliendelea bila ya Wakubwa kujua.

Kamati kuu ya ASP ikaamua kuwa Mapinduzi yafanyike tarehe 11Jan 1964 na vijana walioteuliwa kuongoza mapambana na Mapinduzi hayo ni Seif Bakari, Saidi Washoto,Abdallah Natepe, Khamis Hemedi, Saidi Ali Bavuai, Yusuf Himid, Pili Khamis, Khamis Daruwesh, Saidi Mfaranyaki, Mohammed Abdallah, Hafidh Suleiman, Hamis Ameir, Ramadhani Haji na John Okello.

Katika kufanya Mipango ya Mapinduzi ilibidi kiombwe kibali cha kufanya Mkutano Wa hadhara wa Wanachama kote Visiwani kuanzua saa 10:00 Jioni hadi Saa sita Usiku ambapo itafanywa fete, Mungu Saidia vibali vilipatikana Mapema sana.

Kabla ya kufika saa 10 Jioni muda wa Mkutano taarifa za Kuwepo kwa Mapinduzi yalianza kuenea kwa uchache sana na hatimaye Saa 5:00 Mchana Sheikh Karume, Abdu Jumbe na Sheikh Thabit Kombo walikutana kufanya tadhimini ya Maandalizi na kusikia kuwa taarifa za mapinduzi zimeenea na watu wanajadili Hatimaye kukubaliana Kupeleke taarifa za kuwepo kwa watu wanaotaka kuvuruga mkutano wa ASP na Polisi wakapokea taarifa hizo na kuanza kuwasambaza jeshi la Polisi sehemu mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na hatimaye nguvu ya jeshi la Polisi ikapungua pale BOMANI Makao makuu ya Polisi ambapo ilisaidia kutekelezwa kwa Mapinduzi kirahisi.( MBINU).

Mkutano Ulianza Saa 10 Jioni kwa wanachama na Wananchi kuingia pamoja na vile vikundi vya vijana vilivyoandaliwa na mkutano ukafanyika Mpaka saa Sita Usiku na Fete ikavunjika.
Hapo ndipo ikawa mwanzo wa Mapinduzi kwa Vijana kuanza kuvamia na kushambulia kwa Ujasiri Makao makuu ya Polisi , Kituo cha Ziwani na Mtoni na Kuyateka haraka haraka na kuchukua Silaha mbalimbali na haukupita muda wakawa wamekamata Malindi. RAHALEO ndiko kulikuwa Makao makuu ya Mapinduzi na Sheikh Karume alikuweko kule tangu Muda.

Mpaka Alfajiri sehemu zote Muhimu zimekwisha kushikwa na Vijana wa ASP na Mapinduzi yakatangazwa katika SAUTI YA ZANZIBAR.
Note: Vijana wa ASP hawakuwa na Silaha za kisasa zaidi ya Mapanga,Mawe na Marungu.

Sultani hakufanikia kukamatwa baada ya kukimbia kuelekea Unguja na hatimaye Serikali ya Kiingereza Ikamuomba Mwalimu Nyerere Impokee Sultani na baadae watakuja kumchukua, Mwalimu Nyerere kwa moyo wa Busara akampokea Dar es Salaam na ASP kupitia viongozi na Vijana wake wakaimarisha Mapinduzi na hatimaye nchi nzima (Unguja na Pemba vilidhibitiwa).

Lakini ni dhahiri na vema kutambua mchango wa pekee wa Comred John Okello na vijana wenzake waliotekeleza mapinduzi ya Zanzibar ya 12, January 1964

Kama ilivyo tabia ya Mapinduzi popote Duniani watu wengi hupatwa na kifo, hivyohvyo Mapinduzi ya Zanzibar watu wengi wa rangi na kabila zote walikufa.

3.MAFANIKIO BAADA YA KUTEKELEZWA KWA MAPINDUZI.

Mafanikio ya haraka haraka baada ya Mapinduzi ni kama vile:

A.Kutaifishwa kwa Maduka ya rehani yaliyokuwa yanamilikiwa na Waarabu-Masultani na wenyeji kurudishiwa vitu vyao walivyoweka rehani ili kupata mkopo.

B.Kutaifishwa kwa Magari na njia zote za Usafiri mfano Magari ya Lingisha yaliyokuwa yanatumiwa na Wazungu na Waarabu.

C.Wazee waliokuwa ombaomba Barabarani walikatazwa na badala yake wakawa wanapewa posho ya Shilingi 60 kwa Mwezi kila mmoja na Wizara ikaundwa ya kuweka hali za Watu sawa.

D. Wazee na watoto yatima waliokuwa wanalala Barazani na Mitaani walianza kujengewa nyumba za kisasa kwa makazi yao.

E.Kupatikana kwa Elimu kwa Watoto wa Waafrika na kufutwa kwa Ada zote na watoto kusoma bure kabisa.

F.Kutaifishwa kwa Mashamba yaliyokuwa yanamilikiwa na Waarabu na kugaiwa kwa Wenyeji.

G.Kufutwa na gharama za Matibabu kwa wananchi wa Zanzibar na matibabu kuwa Bure kwa wote.

La mwisho na muhimu kabisa ni Kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar April 26, 1964.

4.MATATIZO BAADA YA MAPINDUZI.

Baada ya Mapinduzi kama ilivyo katika nchi zote duniani matatizo kadhaa yalijitokeza hapo Zanzibar.

A. Silaha zilizokuwa zimeenea mikononi mwa wananchi wengi baada ya kuzichukua kipindi cha Mapinduzi, na pengine zilianza kutumika kufatekeleza uhalifu na kuwatishia watu wengine.

B. Kuenea kwa Hofu.Watu wengi hasa wale ambao walikuwa sio Waafrika, walihofu sana watatendewa nini baada ya Mapinduzi na wengine wakaanza kukimbia licha ya ASP Kuwaondoa Hofu watu hao na kuwahakikishia kuwa hakuna tena Bughudha. Ilikuwepo pia hofu baina ya Waafrika kwa kipindi fulani kwa kuhofia kuvamiwa na Waingereza ama Wasultani.

La mwisho ni changamoto ya kugawa Rasilimali zilikuwepo kama Ardhi, Mali kwa wananchi walio wengi wa Visiwani.

5.KUUNDA SERIKALI YA MAPINDUZI.

Baada ya Mapinduzi ya January 11-12,1964, Ilifuatiwa na kuundwa kwa Serikali ya Mapinduzi Ambayo itajumuisha Waafrika na Wanamapinduzi chini ya Chama cha ASP na harakati ya kuunda serikali ilikamilika kama ilivyopangwa na Wanamapinduzi baadhi wakaingizwa katika baraza la Mapindizi ya Zanzibar lenye watu 14 kuanza kuwahudumia Wananchi.

6.MUUNGANO.

Kama ilivyokuwa kiu ya AFRO-SHIRAZI PARTY tangu hapo awali ya kuungana na wenzao wa Tanganyika (TANU), hatimaye baada ya kutekelezwa kwa Mapinduzi mipango ya Muungano ilianza kutekelezwa.
Na Mtakumbuka kuwa moja ya Manifesto ya ASP ni, *"Kuwa tukipata Uhuru azma yetu ni kuona Afrika yote inakuwa moja yenye nguvu."Lakini kwa Tanganyika na Zanzibar ahadi ya muungano ilikuwa ya Wanachama wenyewe waliyokuwa wanaitoa katika mikutano yao yote, "Kwamba tutakapopata uhuru tutaungana na wenzetu wa Tanganyika."
Na mkumbuke pia kuwa asili ya watu wa Zanzibar na Tanganyika ni walewale tofauti ni kutawaliwa na Sultani.
Na harakati na Maandalizi ya kutimiza azma hii ya ASP na watu wa Zanzibar ilianza mara moja kwa kufiatiwa na Mikutano na vikao halili na namna ya kutekeleza azimio la muungano na hatimaye tarehe 26 April 1964 nchi hizi mbili ziliuganishwa na baadae jina Tanzania kuzaliwa.
Sote tunajua manufaa ama Faida ya Muungano kuwa ni Kujenga Umoja na Ushirikiano pamoja na kuimarisha Ulinzi na Usalama baina ya Pande pili, ambapo mpaka leo tunafurahia muungano wetu.

7. WASALITI WA MAPINDUZI YA AFRO-SHIRAZI PARTY NA MUUNGANO WETU.

Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wetu ni matukio makubwa sana katika historia ya Tanzania na yenye manufaa makubwa mno na vyote vinategemeana. Lakini pingamizi kama ilivyo desturi ya binadamu haikwepeki na hivyohvyo Katika Mapinduzi na Muungano walikuwepo Wasaliti, kabla ya Mapinduzi na Muungano na hata baada ya Mapinduzi na Muungano wasaliti bado wapo wa ndani na nje ya Taifa letu.

Mtakumbuka usaliti wa Wanashirazi kuanzisha chama cha ZPPP! kitendo kilichopelekea kuchelewa kwa Uhuru na pengine Zanzibar (ASP) ingeweza kupata Uhuru kwa njia ya Voting mapema.

Lakini baada ya Mapinduzi wanachama wazito na mafisadi wa HIZBU -Waarabu walikuwa wanasononeka sana kupinduliwa kwa Serikali ya Sultani.
Na waliendelea kwa kushirikiana na wenzao huko nje kujaribu kutekeleza majaribio ya kupindua Serikali ya ASP lakini walishindwa mara kadhaa.

Mwishoni mwa mwaka 1964 mtu mmoja Amour Zahor na wenzake wenye itikadi ya Hizbu-ZNP wakijiita "People's Fighters Union", walitaka kuangusha serikali ya ASP kumrudisha Mwinyi-Sultani lakini walishindwa pia.

Mwaka 1967 yalitokea majaribio Matatu yakiongozwa na Suleiman Hamad wa Pemba, Waarabu na Saleh Ali Nassor wakijiita, "Freedom Fighter" wakitaka kupindua serikali ya ASP lakini waliendelea kushindwa pia. N.k

Lakini Jaribio la kusikitisha sana ni kuuawa kwa *SHEIKH ABEID AMANI KARUME*mwaka 1972 kifo kilichotokea katika Ofisi kuu ya AFRO-SHIRAZI PATY ambapo Sheik Karume kama ilivyokuwa desturi yake muda wa jioni hutembelea ofisi za ASP kwa lengo la kuzungumza na viongozi wa Chama pamoja na kucheza DHUMNA-BAO. Siku hiyo Sheikh Karume aliwakuta viongozi wengi wa ASP ofisi akiwemo, Mhe.Maalim Shaha Kombo, Mhe.Ibarahim Saadallah, Mzee Mtoro Rehani Pamoja na Sheikh Thabit Kombo ( Katibu mkuu wa ASP).

Muda mfupi Risasi kutoka mlangoni sikasikika na Sheikh Karume alipigwa Shingoni na kumiminiwa risasi sehemu zingine za mwili na kupelekea kifo chake licha ya kukimbizwa Hospitalini. Wengine waliodhurika na tukio hilo ni Sheikh Thabit Kombo ambaye alipigwa risasi kadhaa ila haikupelekea kupoteza kifo , Pomoja na Sheikh
Ibrahim Saadallah ambaye alipatwa na risasi kooni.

Hata baada ya Kifo cha Shujaa Sheikh Karume, Majaribio ya Kupindua Serikali ya ASP na kupinga muungano wetu hazikukomba. Na hata leo na kipindi hiki Mafisadi, Mabwenyenye pamoja na Viongozi wa Visiwa Vya Zanzibar na Tanganyika yapo dalili za kutaka kupinga mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wetu kwa kwa lengo la kuona Maslahi yao binafsi na Washirika wao zimekomesha.

Lakini hata baada ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar na kiongozi wa ASP pamoja na majaribio kadhaa ya kupindua serikali ya ASP yaliendelea kushindwa na Mapinduzi ya Zanzibar yaliendelea kudumu mpaka leo hii.

MWISHO.
Napenda niendele kutoa rai yangu kwa Viongozi na Wananchi wote wa Tanzania bara na Tanzania visiwani ( TANZANIA) Kuendelea kuenzi Mapinduzi ya Zanzibar yaliyopelekea kuwepo kwa Muungano wetu. Pamoja na Muungano wetu ambao umezidi kuimarika na kuleta tija katika Umoja na Mshikamano na kuimarika kwa Ulinzi na n Usalama wa pande zote za muungano. Kwani ni dhahiri kuwa bila muungano imara pande zote za Tanzania Bara na Tanzania Visiwani havitakuwa salama na maadui watatumia mwanya huo kutufarakanisha.

Imeandaliwa na:
Abel Elibariki
Common Mwananchi
abel.bariki@gmail.com
0658851802
Kutoka Maktaba yake.
 
Watanzania kama mnataka kujua mini kilikuwa kabla na baada ya mapinduzi someni kitabu kinachoitwa KWAHERI MKOLONI - KWAHERI UHURU.
Humo ndio mutaona Uongo na Unafiki wa Elibaraka.
 
Naunga mkono hoja, tuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kuenzi matokeo chanya ya Mapinduzi hayo ambao ni Muungano wetu adhimu ulituzalishia taifa moja tuu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kule Zanzibar wao wana msemo wao was
Mapinduzi Daima
Na sisi Watanzania katika umoja wetu tunasema kwa kauli moja
Tutaulinda Muungano kwa gharama yoyote, na hata kama gharama yenyewe ni kutengua demokrasia kama ilivyofanyika kwenye uchaguzi wa Zanzibar, for the sake of union, demokrasia na itenguliwe! .

Nawatakia mapumziko mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P
 
Back
Top Bottom