Tuwe wasafi haijalishi nini. Ukinuka kikwapa, miguu au mdomo umeshajivua heshima yako

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,081
Kwa mtu wa aina hii bila kujali hadhi yake unaanza kuona ni heri awepo paka aliejipumzikia pembeni kuliko yeye. Haya sio mambo madogo kwa mtu mzima, ustarabu ni jambo muhimu na heshima ni kitu cha bure jaribu kuheshimu wengine kwa kuwa msafi, shida ya kuumiza wenzio pua ili iwaje?

.
1676921699615.jpeg



KIKWAPA

images

Yaani usipooga asubuhi au / na jioni kikwapa kinaanza kutema, wewe ushazoea kuoga kila baada ya siku 2 au tatu na pua yako ishazoea kuanza kusikia harufu baada siku hizo lakini jua kwamba utaratibu wa kawaida ni kuoga kila siku, wanaooga kila siku unaanza kuwaumiza kwa kikwapa.

Kurudia Soksi, boxer/chupi, vest/bra

360_F_514899742_z0E5okmGzLbqRLwLNzP80CAconwzxwgK.jpg


ya jana unairudia vp kwa mfano tena hasa kwenye jiji lenyye joto? Ni kwamba utaona kawaida lakini ukishazoea hii tabia huwezi sikia harufu lakini jua kwamba utaratibu wa kawaida ni kubadili soksi kila siku, wanaobadili soksi kila siku utawaumiza pua ukienda nje ya utaratibu.

MDOMO

get-rid-of-bad-breath.jpeg


Mdomo wako unanuka hatari yani hata kutamka tu maji jarufu hio, Umezoea kupiga mswaki mara 1 tu kwa siku basi jua wengi tunapiga asubuhi na jioni na wapo wanaopiga kila wakila, jaribu kuwa na ubinadamu tafadhali, hewa hii ya wote ifanye iwe nafuu kwa wote.
 
.Yani usipooga asubuhi au / na jioni kikwapa kinaanza kutema, wewe ushazoea kuoga kila baada ya siku 2 au tatu na pua yako ishazoea kuanza kusikia harufu baada siku hizo lakini jua kwamba utaratibu wa kawaida ni kuoga kila siku, wanaooga kila siku unaanza kuwaumiza kwa kikwapa.

Soksi ya jana unairudia, ukishazoea hii tabia huwezi sikia harufu ya soksi ikivaliwa siku 1 lakini jua kwamba utaratibu wa kawaida ni kubadili soksi kila siku, wanaobadili soksi kila siku utawaumiza pua ukienda nje ya utaratibu.

Mdomo wako unanuka hatari yani hata kutamka tu maji jarufu hio, Umezoea kupiga mswaki mara 1 tu kwa siku basi jua wengi tunapiga asubuhi na jioni na wapo wanaopiga kila wakila, jaribu kuwa na ubinadamu tafadhali, hewa hii ya wote ifanye iwe nafuu kwa wote,

Haya sio mambo madogo kwa mtu mzima, ustarabu ni jambo muhimu na heshima ni kitu cha bure jaribu kuheshimu wengine kwa kuwa msafi, shida ya kuumiza wenzio pua ili iwaje ?
Kuna siku mwizi aliiba.
Subil kidogo narudi kuendelea na story.
 
Oga vizuri kwa showergel, safi ,swali fresh hata kila ukienda kuswali inapendeza ni Sunnah ,pakaa mafuta vizuri ya nywele ya mwili kama ni sehemu za joto hata lotion za kiume zipo kiboa ...Pendeza vizuri unakuwa comfortable Kuna unyunyu Tena Bei che hata huu wa Bei mbaya unaweza kununua wa kupima ukaenda na flow.

Ila Kuna watu wachafu kama mbuzi yaani huko kweny daladala ni hatari
 
Oga vizuri kwa showergel, safi ,swali fresh hata kila ukienda kuswali inapendeza ni Sunnah ,pakaa mafuta vizuri ya nywele ya mwili kama ni sehemu za joto hata lotion za kiume zipo kiboa ...Pendeza vizuri unakuwa comfortable Kuna unyunyu Tena Bei che hata huu wa Bei mbaya unaweza kununua wa kupima ukaenda na flow.

Ila Kuna watu wachafu kama mbuzi yaani huko kweny daladala ni hatari
hasa sehemu zenye joto, daladalani watu wananuka hatari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchafu ni ujinga na unakera kwa asiye oga, hata uwe na pesa ukawa mchafu mi nakuona bwege tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom