Tuwe wakweli, tatizo sugu la Watanzania ni Uoga, siyo Unafiki. Hayati Membe hakuwa muoga

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,447
11,143
Hello JF crew!
👇👇👇
Kipekee naomba niweke bayana tatizo mojawapo kuu na sugu la watanzania ni UOGA sio Unafiki-, ifahamike ya kwamba kichuguu cha UOGA ndicho hubeba unafiki, uongo, kutojiamini na matakataka yote.

Ndugu Hayati Membe alikuwa jasiri, mzalendo, na mfia nchi na mpigania taifa, kuna mambo ya msingi alimpinga Hayati Magufuli katika haki na kweli tena kwa maslahi ya Tanzania na sisi sote, mfano ukurupukaji, kukosa weledi, upofu wa diplomasia, ujuha wa kijima, kujiona ndio mwenye akili kuliko wote, conclusive opinions, self-centered judgement, kutopenda dialogue hasa katika masuala ya kiushauri, kukosa subra na ukomavu wa kimaamuzi, Ni baadhi ya mambo ambayo ndugu Membe aliyaona na kumkemea Magufuli kwa dhati kabisa.

B.C. Membe hakuwa muoga, alikuwa jasiri na mwenye fikra jumuishi na fikra za mawanda tanzu, he had mtambuka thinking and mindset.

Benard C. Membe was a true believer in Nationality na constitutionality.

Kwa heri Mkuu Membe, wanaohani msiba wako watamke wewe hukua muoga, waseme ulikuwa jasiri mzalendo ukiakisi kiapo cha utumishi kama state agent, no one is above the state, the state is under collective ownership.

Nice Sunday to all.

Wadiz
 
Wasije hapa tu kusema wazuri hawafi, watz ni noma sana. OP nimeandika.
 
Ccm ndio muasisi wa system ya uoga kwa watanzania.(WAO WANAITA UZALENDO)
Uwe ni mtu wa jipendekeza, kujinyenyeza kinafiki nafiki, fumbia macho ukweli, utafika mbali.
 
Back
Top Bottom