Mkuu hapo mbona hakuna cha kujadili? Labda cha kujadili kiwe hiki:
1. Tuivunjeje (rasmi) hii kitu?
2. Tukishauvunja hawa wapemba waliojaa huku kwetu wamepora ardhi yetu na kujenga kwenye ardhi yetu tumawapeleka wapi?
Udini utakuja kulimaliza hili taifa utakuja kufanya hii amani tuliyo nayo itajabaki kuwa historia na lawama zitamwelekea jk aliyeanzisha mwaka 2010 kwenye campain
Sio kweli Mkiristu kwenye BLM ni Mwakanjuki pekee, alishakuwepo John Okello, Isack Sepetu na kuna wakristu wengi tuu wenye majina ya Kiislamu.
Hata kina Wolfgang Dourado, Agustino Ramadhani, Charles Hillary etc ni Wakristo Wanzanzibari!.
Kanisa lilianzia Zanzibar na Bagamoyo kufuatia kupigwa marufuku biashara ya utumwa. Soko lilikuwa Bagamoyo na Zanzibar, Kanisa liliwalipia fidia watumwa ili kuwagomboa na ndio Wakristu wa kwanza!.
Kiukweli udini halihawahi kuwa tatizo Zanzibar!.
Viongozi wetu hawatuambii ukweli kwamba tatizo la zanzibar sio kero za Muungano, ni ubaguzi wa kidini. Viongozi wanafanya hivyo kwa makusudi wakidhani kwamba wakieleza ukweli wataamsha chuki za kidini. Mimi ni muumini wa ukweli maana maandiko yananiambia "ukweli utaniweka huru". Ukiondoa Bri. Gen. Adam Mwakanjuki ambaye pia ana asili ya uislamu, hakuna Mkristo aliye shika nafasi ya juu katika SMZ na mpaka sasa SUK (sERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA).
hata ukijiuliza maswali mawili madogo utapata jibu.
Mosi: Kwanini harakari za "kupinga muungano" ziendeshwe na kikundi cha kidini JUMIKI (Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu?
Pili: Kwanini harakati hizo ziambatane na kuchoma makanisa na magari ya wachungaji? Ni Misikiti mingapi imechomwa?
Ni wazi kwamba muungano umepoteza maana kwa sasa, lakini tatizo sio muungano, ni udini. Kwa Zanzibar, Mtu yeyote anayetoka bara wanamchukulia kama Mkristu na ni adui.
Nilikua Z'bar siku 3 zilizopita, nilipata taarifa kwamba mjumbe mmoja wa baraza la wawakilishi alipokua akichangia hoja na Mhe. Jussa Ladhu kuhusu sehemu ya bahari ya zanzibar kufanywa ya muungano na Mhe. Tibaijuka alitumia maneno "Tusipokuwa makini na mambo haya tunaweza kujikuta WAKRISTU toka bara wanakuja kututawala!"
Inasemekana ndo sababu Rais wa Z'bar Dr. Shein anakuwa mzito kuchukua hatua kwa ghasia za namna hii maana naye ni mdini.
Nawasilisha.
Mkuu hapo mbona hakuna cha kujadili? Labda cha kujadili kiwe hiki:
1. Tuivunjeje (rasmi) hii kitu?
2. Tukishauvunja hawa wapemba waliojaa huku kwetu wamepora ardhi yetu na kujenga kwenye ardhi yetu tumawapeleka wapi?
Mkuu uko nyuma ya mada.
John Okello ndiye aliyechangia kupatikana na uhuru wa zanzibar. Baada ya hapo akina Karume walimfanyia hila nyingi sana, mojawapo ilikuwa udini pamoja na uraia. Hao wengine sidhani kama walipata nyadhifa za juu kama alivyoainisha mtoa mada. Balozi Isack Sepetu alikuwa waziri wa nini, Charles Hilary Nkwanga aliwahi kuwa waziri?
Acha kukurupuka!
Kwamwewe
Naskitika kwamba kama reference ni mwalimu nyerere tena kwa kutafutiza vijimakosa hatuwezi kufika popote.
Nyerere huyu ndiye aliyekuwajasiri kuwakemea maskofu na pia mashekhe huko zanzibar. Ukiangalia hotuba za mwalimu nyingi amekea sana udini tena sana. Tatizo ikatokea ameusema uislam tena pengine kwa maana nzuri tu anazuka mtu bila kutafakali kwa malengo yake ANACHOP KASENTENSI KATIKATI NA KUPOTOSHA UMMA, Tunajenga au lengo nikubomoa.
Juzi nimekuuliza humu ndani ya jamii forum
1. Nimisikiti mingapi imechomwa au kuhalibiwa dhidi ya makanisa 26, hukunijibu labda leo utanijibu
2. umesikia wapi huku tanzania bara ubaguzi wa wapemba au wanguja au wakifukuzwa ututolee mifano
3. Kama suala ni waislam kubaguliwa hususani hapo zanzibar 99% ya viongozi wa serikali ni waislamu je wanawabaguwa wenzao?
4. Umetowa reference nyingi za miaka ya 196.... Naomba pia utoe reference nyingi za mageuzi ya chinichini huko zanziba miaka ya karibuni.
5. Hivi wewe kwa mfano baba yako alikosea ulipokuwa na miaka kumi hivi utaendelea kumlaani mpaka kuuzeeka kwako, utampiga mara baada ya kukuwa? utamdharirisha kisa alikupiga utotoni? Sisemi Karume au Nyerere alikosea hasha, lakini unajenga hoja katika mising ya ajabu kabisa. upo kutafuta justification ambazo kwa miaaka yakaribun inabidi kukushagaa. Yamiaka ya 196.. ilifaa watoto wafundishe na walimu wa historia lakini tunapotafuta amani ya taifa la watanzani- Waislam, wakristu, wasionadini na wenyedini zingine pia, tunahitaji kujenga kwa kuchangia mawazo yatakayotutoa kweneye hilo dudu ubaguzi wa kiimani.
6. Ni haki yako kumsema nyerere kama alikosea, lakini pia kubambikia misalaba, vimedali na matatizo madogomadogo hakufai, baadhi ya vitabu vinapicha za majalada ya nje either majengo, maeneoflani nk nidhambi? Je kama ilikuwatatizo kwa vimedali vilivyo na bikra maria na bendela ya Tanzani hao walibuni hivyo wakiamini katika imani yao, wewe kwa upandewako ulifanya ubunifu wowote katika dini yako yenye kufanana na hiyo ukakatazwa???
Tatizo nilionalo mimi ni pale unatafuta ushahidi tu hata usio na guvu kuchochea matatizo ni vibaya sana
anaongea halafu anajijibuUshasema wapemba alafu watapelekwa wapi tena?