Tuwe wakweli: Tatizo La Zanzibar sio Muungano, ni Udini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwe wakweli: Tatizo La Zanzibar sio Muungano, ni Udini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bundewe, Jun 3, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Viongozi wetu hawatuambii ukweli kwamba tatizo la Zanzibar sio kero za Muungano, ni ubaguzi wa kidini. Viongozi wanafanya hivyo kwa makusudi wakidhani kwamba wakieleza ukweli wataamsha chuki za kidini. Mimi ni muumini wa ukweli maana maandiko yananiambia "ukweli utaniweka huru".

  Ukiondoa Bri. Gen. Adam Mwakanjuki ambaye pia ana asili ya uislamu, hakuna Mkristo aliye shika nafasi ya juu katika SMZ na mpaka sasa SUK (SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA).

  Hata ukijiuliza maswali mawili madogo utapata jibu.
  Mosi: Kwanini harakati za "kupinga muungano" ziendeshwe na kikundi cha kidini JUMIKI (Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu?

  Pili: Kwanini harakati hizo ziambatane na kuchoma makanisa na magari ya wachungaji? Ni Misikiti mingapi imechomwa?

  Ni wazi kwamba muungano umepoteza maana kwa sasa, lakini tatizo sio muungano, ni udini. Kwa Zanzibar, Mtu yeyote anayetoka bara wanamchukulia kama Mkristu na ni adui.

  Nilikua Z'bar siku 3 zilizopita, nilipata taarifa kwamba mjumbe mmoja wa baraza la wawakilishi alipokua akichangia hoja na Mhe. Jussa Ladhu kuhusu sehemu ya bahari ya zanzibar kufanywa ya muungano na Mhe. Tibaijuka alitumia maneno "Tusipokuwa makini na mambo haya tunaweza kujikuta WAKRISTU toka bara wanakuja kututawala!"

  Inasemekana ndo sababu Rais wa Z'bar Dr. Shein anakuwa mzito kuchukua hatua kwa ghasia za namna hii maana naye ni mdini.

  Nawasilisha.
   
 2. M

  Mwanantala Senior Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Serikali hii inatupeleka pabaya sana. Ni busara sasa kuvunja muungano kabla ya kujiingiza kwenye ugaidi.
   
 3. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo mbona hakuna cha kujadili? Labda cha kujadili kiwe hiki:

  1. Tuivunjeje (rasmi) hii kitu?
  2. Tukishauvunja hawa wapemba waliojaa huku kwetu wamepora ardhi yetu na kujenga kwenye ardhi yetu tumawapeleka wapi?
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ushasema wapemba alafu watapelekwa wapi tena?
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Udini utakuja kulimaliza hili taifa utakuja kufanya hii amani tuliyo nayo itajabaki kuwa historia na lawama zitamwelekea jk aliyeanzisha mwaka 2010 kwenye campain
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tatizo la Zanzibar sio udini, it is lack of leadership. Basi.
   
 7. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Watajuta kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa maana CUF imeamua kuja "kivingine!"
   
 8. magosha

  magosha JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  huo udini unaendekezwa na nani kama sio viongozi ambao ni wanasiasa so kama ni udini basi uko serikalini.
   
 9. j

  jerry-B Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hv zanzibar iliungana na makanisa?jamaa wana roho mbaya,wabinafsi na wadini,bora uvunjwe
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,590
  Likes Received: 18,573
  Trophy Points: 280
  Sio kweli Mkiristu kwenye BLM ni Mwakanjuki pekee, alishakuwepo John Okello, Isack Sepetu na kuna wakristu wengi tuu wenye majina ya Kiislamu.

  Hata kina Wolfgang Dourado, Agustino Ramadhani, Charles Hillary etc ni Wakristo Wanzanzibari!.

  Kanisa lilianzia Zanzibar na Bagamoyo kufuatia kupigwa marufuku biashara ya utumwa. Soko lilikuwa Bagamoyo na Zanzibar, Kanisa liliwalipia fidia watumwa ili kuwagomboa na ndio Wakristu wa kwanza!.

  Kiukweli udini halihawahi kuwa tatizo Zanzibar!.
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mkuu uko nyuma ya mada.
  John Okello ndiye aliyechangia kupatikana na uhuru wa zanzibar. Baada ya hapo akina Karume walimfanyia hila nyingi sana, mojawapo ilikuwa udini pamoja na uraia. Hao wengine sidhani kama walipata nyadhifa za juu kama alivyoainisha mtoa mada. Balozi Isack Sepetu alikuwa waziri wa nini, Charles Hilary Nkwanga aliwahi kuwa waziri?
  Acha kukurupuka!
   
 12. M

  Mohamed Ngwasu JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2012
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 304
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  namuunga mkono huyu aliyesema wamekuja kivingine, kama wanataka uvunjike kwa nini tuwalazimishe vunja tupa kule.
   
 13. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,316
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160

  hii ilikuwa 1993


  MJADALA unaendelea nchini kote juu ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na muundo wa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Inavyoelekea yapo matatizo, dosari na sababu za msingi zilizopelekea wananchi kuhoji muundo wa sasa wa Muungano na kuleta hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika ni yenye kuundwa kama si leo kesho.

  Lakini wapo pia wanaopinga kabisa kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.


  Aliyejitokeza kwa nguvu na kwa ukali hadharani kupinga hoja hiyo ni Mwalimu Julius Nyerere, katika kupinga hoja hiyo Mwalimu anatoa hoja zifuatazo:


  Hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika imeletwa kwa kuwachoka Wazanzibari na Waislamu. Ufupi wa maneno Mwalimu Nyerere anadai hoja ya kuundwa Serikali ya Tanganyika imetokana na chuki za kidini - Wakristo kuwachukia Waislamu.  Hoja haipo katika sera za CCM na taratibu zimekosewa.


  Kuundwa kwa serikali ya Tanganyika kutavunja Muungano na kutavunja Tanganyika pia.

  Ukizingatia sifa nyingi ambazo Nyerere alijilimbikizia wakati wa utawala wake na sasa si vigumu kuelewa kwa nini anapinga kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.

  Mambo yake yote aliyoyaanzisha kwa vishindo huku akisifiwa kuwa zidumu fikra zake, yamekuwa yakiporomoka moja baada ya jingine huku mwenyewe akiona. Lililosalia ni Muungano; nao ukiporomoka haitaleta picha nzuri katika historia yake katika siasa.  Lakini lililo gumu kueleweka ni hatua ya Mwalimu Nyerere kutumia Turufu ya udini kuwagawa Wabunge; wana-CCM na Wa-Tanzania kwa ujumla katika suala hili. Kauli hiyo ingesemwa na Muislamu ingepewa mtizamo tofauti na labda isingeeleweka hasa miongoni mwa Waislamu.

  Lakini kusemwa na Mwalimu Nyerere kunaleta mkanganyiko zaidi. Kwanini; (udini ulikuwa umejengeka). Hali hiyo ilipelekea Masheikh kumlalamikia lakini akawanyamazisha kwa kuwashutumu kuwa wanachanganya dini na siasa. Miongoni mwa Masheikh hao wapo waliofukuzwa nchini; waliowekwa kizuizini, waliofukuzwa katika chama na kadhalika.  Sheikh Hassan bin Amir katika waraka wake kwa Waislamu mwaka 1963 aliutaja udini uliokuwa unajengwa Tanzania kwa kutoa mifano ifuatayo:  Kuingizwa nchini Tanganyika mara tu baada ya uhuru vimedali vidogo vidogo vyenye picha ya bendera ya Tanganyika usoni na katikati ya bendera hiyo amesimama Mama Maria na mtoto mchanga na nyuma yake maandiko 'MARIA MTAKATIFU ULINDE UHURU WA TANGANYIKA'.  Gazeti la KIONGOZI la tarehe 1/8/1963 lilimuonyesha Bwana George Kahama akipewa cheo cha dini na Pope kwa kuwakilisha serikali ya Tanganyika katika mkutano wa Makanisa ya Roma.  Mwaka huo huo wa 1963, mnamo tarehe 24 mwezi wa nane, Baraza Kuu la Makanisa ya Kilutheri Tanganyika lilitoa matangazo kuwa Uhuru wa Tanganyika ulikuwa 'Chini ya Msalaba'.
   
 14. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa .Msukuma siruhusiwi kumiliki kiwanja Z'bar wakati mpemba anaruhusiwa kumiliki ardhi popote Tanganyika. Hii naona ni kero nyingine, tuuvunjilie mbali muungano huu kandamizi.
   
 15. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na John Okelloh "alifukuzwa" baada ya kuongoza mapinduzi, mchango wake mpaka sasa hakuna anayeukumbuka na kuuenzi. Anaenziwa Karume ambaye aliitwa tu aende akakalie kiti cha ikulu baada ya vijana kumaliza kazi
   
 16. j

  junior05 Senior Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu trust my words

  Umeona mbali sana,umeweza kugundua siri ya vurugu za znz na umewasilisha vizuri

  Nawasilisha  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 17. a

  adolay JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Kwamwewe

  Naskitika kwamba kama reference ni mwalimu nyerere tena kwa kutafutiza vijimakosa hatuwezi kufika popote.

  Nyerere huyu ndiye aliyekuwajasiri kuwakemea maskofu na pia mashekhe huko zanzibar. Ukiangalia hotuba za mwalimu nyingi amekea sana udini tena sana. Tatizo ikatokea ameusema uislam tena pengine kwa maana nzuri tu anazuka mtu bila kutafakali kwa malengo yake ANACHOP KASENTENSI KATIKATI NA KUPOTOSHA UMMA, Tunajenga au lengo nikubomoa.

  Juzi nimekuuliza humu ndani ya jamii forum

  1. Nimisikiti mingapi imechomwa au kuhalibiwa dhidi ya makanisa 26, hukunijibu labda leo utanijibu

  2. umesikia wapi huku tanzania bara ubaguzi wa wapemba au wanguja au wakifukuzwa ututolee mifano

  3. Kama suala ni waislam kubaguliwa hususani hapo zanzibar 99% ya viongozi wa serikali ni waislamu je wanawabaguwa wenzao?

  4. Umetowa reference nyingi za miaka ya 196.... Naomba pia utoe reference nyingi za mageuzi ya chinichini huko zanziba miaka ya karibuni.

  5. Hivi wewe kwa mfano baba yako alikosea ulipokuwa na miaka kumi hivi utaendelea kumlaani mpaka kuuzeeka kwako, utampiga mara baada ya kukuwa? utamdharirisha kisa alikupiga utotoni? Sisemi Karume au Nyerere alikosea hasha, lakini unajenga hoja katika mising ya ajabu kabisa. upo kutafuta justification ambazo kwa miaaka yakaribun inabidi kukushagaa. Yamiaka ya 196.. ilifaa watoto wafundishe na walimu wa historia lakini tunapotafuta amani ya taifa la watanzani- Waislam, wakristu, wasionadini na wenyedini zingine pia, tunahitaji kujenga kwa kuchangia mawazo yatakayotutoa kweneye hilo dudu ubaguzi wa kiimani.

  6. Ni haki yako kumsema nyerere kama alikosea, lakini pia kubambikia misalaba, vimedali na matatizo madogomadogo hakufai, baadhi ya vitabu vinapicha za majalada ya nje either majengo, maeneoflani nk nidhambi? Je kama ilikuwatatizo kwa vimedali vilivyo na bikra maria na bendela ya Tanzani hao walibuni hivyo wakiamini katika imani yao, wewe kwa upandewako ulifanya ubunifu wowote katika dini yako yenye kufanana na hiyo ukakatazwa???

  Tatizo nilionalo mimi ni pale unatafuta ushahidi tu hata usio na guvu kuchochea matatizo ni vibaya sana
   
 18. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,316
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  NIPE REFERENCE YOYOTE YA NYERERE KUWAKEMEA MAASKOFU ZANZIBAR

  NIMEKUWEKEA CHANZO CHA HII MITAFARUKU YA KIDINI UNANIAMBIA HAYO YOTE NI HISTORIA ,

  WEWE UNAZUNGUMZIA KUCHOMWA MAKANISA KULE ZANZIBAR , UNAUSHAHIDI GANI KUWA WALIOCHOMA NI UAMSHO???

  KUNA IMAMU WA MSIKITI ALIUWAWA MSIKITINI NA POLISI MWAKA 2001 SIKU MOJA KABLA YA MAANDAMANO , KUNA ASKOFU ALILAANI MAUWAJI YALE??? JEE KUNA MTU ALIKAMATWA KWA MAUWAJI YALE????

  KUNA WATU WALIUWAWA PALE MUEMBE CHAI WEWE ULIKUWA HUJAZALIWA???

  BAADA YA MAUWAJI PENGO ALISEMA NINI???

  MIKANDA YA MAUWAJI IPO. SOMA HICHI KITABU Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania

  NAFIKIRI WEWE NDIO HUNA USHAHIDI WA UNAYOYASEMA
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,892
  Trophy Points: 280
  anaongea halafu anajijibu
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Udini huo kwa mujibu wa mtazamo wako unaouona upo Zanzibar tu umeangalia upate wa pili wa kidole ukaangalia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wakristo mpo wangapi? Tukichanganua Wizara za JK zaidi ya 70% ya mawaziri ni WAKRISTO !!! Wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano Wakristo mpo wengi? Wakurugenzi wa taasisi za serikali almost 90% ni wakristo? Ajira vijana wengi wa kiislamu hawana kazi je nikuulize NCHI HII NI YA KIKRISTO!!!!! TUONDOSHEE UPUUZI WAKO HAPA
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...