JK ni zaidi ya mzigo, maana mzigo unaweza kuutua hata kwa hasara.
JK ni janga.
Mara zote nikisikia "Rais ni mchapakazi, anaangushwa na washauri/ watendaji wake tu" nataka kutapika. Kama angekuwa mchapakazi asingeweza kuchagua washauri/ watendaji ovyo, na ingetokea hivyo kwa bahati mbaya -inatokea mara moja moja- angekuwa na mechanism ya kuwajua wazembe ni nani na kuwatoa mara moja. Mbona huyu kila mara tunasikia apologists wanamtetea kwa kuwatoa "bangusilo" washauri/ watendaji wake tu?
Halafu tusimuangalie sana JK na kumtupia lawama yeye kama vile yeye kajifikisha hapo mwenyewe.
JK ni kielelezo tu cha jamii nzima, kwamba mtu anaweza kuwa bw.ege mtozeni kama JK na bado akawa rais wa Tanzania.
Sasa hapo tatizo ni kubwa kuliko JK, ni kwa wote waliomchagua, ni katika mifumo yote aliyopitia mpaka kufika alipo, kuanzia shule alizosoma -mpaka UDSM- kwenda jeshini, kwenda bungeni, kwenye wizara nyeti alizoshika, mpaka Mkapa kumuweka Mambo ya Nje miaka 10 akimtayarisha kwamba siku moja akishika nchi asiwe zezeta.
Inaonekana kote kume fail.
Hata watu wa upinzani nao wana sehemu yao ya lawama kwa kutokuwa na upinzani tahbiti ambao ungewapa Watanzani chaguo la mbadala lenye matumaini. Maana sasa hivi kuna Watanzania wanaipigia kura CCM si kwa sababu wanaipenda sana, ila wakiangalia upinzani wanaona kila siku migogoro, not ready for the prime time - not that CCM is overly ready itself.
Kwa hiyo jamii nzima collectively ime fail, si suala la rais tu.
Rais anachukua lawama kubwa kwa sababu ana wajibu mkubwa na haki / ushawishi kufanya mengi.
Tatizo ni ninyi wanafiki wakubwa mlitarajia rais afanye nini akafanye na kazi za uwaziri hamna haya nyie ni mangapi JK ameifanyia hii kweli fadhila ya Punda mateke.
Mambo aliyofanya JK hayajapata kufanywa na Rais yeyote tangu tupate uhuru kama kuna mtu anapinga basi atakuwa anasumbuliwa na mambo mawili udini au ukabila.