Wadau hali ya wakulima wa korosho ni mbaya sana tofauti kabisa na inavyoripotiwa ktk vyombo vya Habari...
Katika Kijiji chenye watu mia sita wanalipwa watu nane au watu kumi na tatu kisha inatangazwa watu wengi wanalipwa huu uongo unaotangazwa mchana kweupe ni kwa maslahi ya nani.
Wakulima wengi ambao walitarajia kupokea malipo ya korosho ili waandae mashamba ya mpunga Au Mahindi wamebaki tu hawana la kufanya.
mfumo huu sio tuu utaathiri uzalishaji wa korosho msimu ujao bali utaathiri hadi mazao mengine ikiwemo Mpunga na Mahindi.
Imefika pahala mtu anachukua risiti zake za korosho anaenda kuziweka bondi kwa mtu kwa makubaliano kwamba akilipwa watagawana nusu kwa nusu.
Watu wamekwama sana.
Kipindi hiki cha mvua ndo watu hupalilia mikorosho hununua mbolea na salfa kwa ajili ya kuandaa uzalishaji.
Kiukweli serikali inaangamiza kilimo na uchumi wa wananchi wake yenyewe ingawa kwa nje inajinadi kutaka kuwasaidia.
Msaada pekee wa kumpa mkulima wa korosho ni kupeleka pesa ktk maghala mapema kwa ajili ya ununuzi kuliko kumkopa mkulima Tangu mwezi wa tisa na hadi inafika mwezi January hajapata senti yake huo ni unyonyaji usio na mfano.
Tunaiomba serikali iwalipe wakulima pesa zao baada ya kuwa imeshachukua korosho zote iache kutengeneza figisu na kutaka kuwadhulumu wakulima kwa kisingizio cha uhakiki wa mashamba hiyo ni dhulma ya serikali dhidi ya wananchi wake yenyewe.
Sent from my iPhone using JamiiForums