Tuwe na utu na tukubali kushauriwa

Tuwe na utu na tukubali kushauriwa

THT

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2016
Posts
737
Reaction score
873
Habarini wapenda,

Binafsi nafurahi sana kuwa mahali hapa najifunza mnooo.

Ila nilikuwa nina ombi. Mtu anapoleta uzi kutaka ushauri au msaada. Tujifunze kuwa na utu kuwaelekeza watu bila kuwatukana, kuwakejelia na kuumiza hisia za watu wengine bila sababu za msingi. Kuna baadhi ya watu tunaleta utani ambao hata hauna maana ya msingi wakati mtu anahitaji ushauri.

Comment yako inaweza kubadilisha maisha ya mtu inaweza kumuokoa mtu, usiandike tu ilimradi

Wengine tujifanya malaika, kukosoa watu mpaka wanajisikia vibaya badala ya kuwasaidia tunawaumiza na kuwavuruga kabisaa.

Pia tunapoleta uzi na mtu akajibu ukajisikia vibaya,tujitahidi kuwa positive na kuchukua comment hizo kwa namna ya kujifunza.

Ninaomba radhi kama kuna popote nimemkwaza mtu katika uzi huu.
 
Umeandika kwa hisia sana. Pole kama ulishakutana na miamba ya humu JF ukaishia kuambiwa "you are a wasted sperm!"

Ukweli hata hivyo ni kwamba kwenye kusanyiko la watu wengi kama hili, tena wasiofahamiana, watu hawawezi kufanana kwa sababu hata malezi yao na moral compass ni tofauti.

Wengine wana maumivu makali mioyoni mwao kutoka utotoni kwao huko. Wengine wana stress kali za maisha...Wengine hata wenyewe hawajipendi na hawana hata fununu kwa nini wapo hapa duniani. Umri unakwenda na wanaona hawapigi hatua yo yote ya maana katika maisha yao. Wote hawa wapo mitandaoni humu kujitafutia unafuu.

Na njia bora kwao ni kujifanya wako juu sana kimaisha, kudogosha wengine na kuwaumiza. Hawa ndo ukiingia kwenye anga zao siku hiyo utajuta. Utaporomoshewa matusi hata kama hujamkosea. Ndo hawa unakuta mtu ameleta uzi yuko suicidal anaomba ushauri anaishia kuambiwa "nenda tu ukajiue kmmk kwanza huna faida yo yote hapa duniani". Hakuna ubinadamu. Hakuna compassion. Ila waki-log out hapa wanarudi kwenye uhalisia wao na moto wao wa mateso unaendelea kuwawakia.

Kwa vile siyo rahisi kuwadhibiti, jambo la muhimu ni kutochukulia mambo ya humu personal. Mtu akikuporomoshea matusi bila sababu jua kuwa mwenye tatizo ni yeye na siyo wewe. Na njia nzuri ni kumtia kwenye iginoa listi na kuachana naye mazima halafu unaendelea na mambo yako. Ukichukulia personal kila jambo mitandaoni humu kila siku utakuwa mtu wa kudhurika, kutukanana na mwenye hasira. Wewe unaumia kumbe yeye huko ndiyo furaha yake. It is not worth it.

Choose your battles carefully...
Don't take things personal...
Ignore and move on...
Fight if necessary....

Utaishi vizuri tu mbona?...
 
Umeandika kwa hisia sana. Pole kama ulishakutana na miamba ya humu JF ukaishia kuambiwa "you are a wasted sperm!"

Ukweli hata hivyo ni kwamba kwenye kusanyiko la watu wengi kama hili, tena wasiofahamiana, watu hawawezi kufanana kwa sababu hata malezi yao na moral compass ni tofauti.

Wengine wana maumivu makali mioyoni mwao kutoka utotoni kwao huko. Wengine wana stress kali za maisha...Wengine hata wenyewe hawajipendi na hawana hata fununu kwa nini wapo hapa duniani. Umri unakwenda na wanaona hawapigi hatua yo yote ya maana katika maisha yao. Wote hawa wapo mitandaoni humu kujitafutia unafuu. Na njia bora kwao ni kujifanya wako juu sana kimaisha, kudogosha wengine na kuwaumiza. Hawa ndo ukiingia kwenye anga zao siku hiyo utajuta. Utaporomoshewa matusi hata kama hujamkosea. Ndo hawa unakuta mtu ameleta uzi yuko suicidal anaomba ushauri anaishia kuambiwa "nenda tu ukajiue kmmk kwanza huna faida yo yote hapa duniani". Hakuna ubinadamu. Hakuna compassion. Ila waki-log out hapa wanarudi kwenye uhalisia wao na moto wao wa mateso unaendelea kuwawakia.

Kwa vile siyo rahisi kuwadhibiti, jambo la muhimu ni kutochukulia mambo ya humu personal. Mtu akikuporomoshea matusi bila sababu jua kuwa mwenye tatizo ni yeye na siyo wewe. Na njia nzuri ni kumtia kwenye iginoa listi na kuachana naye mazima halafu unaendelea na mambo yako. Ukichukulia personal kila jambo mitandaoni humu kila siku utakuwa mtu wa kudhurika, kutukanana na mwenye hasira. Wewe unaumia kumbe yeye huko ndiyo furaha yake. It is not worth it.

Choose your battles carefully...
Don't take things personal...
Ignore and move on...
Fight if necessary....

Utaishi vizuri tu mbona?...
Nilianza kusoma tu comment yako bila kuangalia ID. Nilipofika mwisho nikawa nimepata hisia kuwa huyo ni yule asiyependa kupindisha pindisha. Kuja kuanga lia kweli ni wewe Shimba ya Buyenze. Nakukubali.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Asante mkuu...

Mimi najiandikiaga tu ninavyoona....na kushea mawazo yangu.

I am humbled [emoji1545]
 
  • Thanks
Reactions: THT
Aiseee sawa kabisa ila kuna wakati mtu ukiwa unaandika kitu mtandaoni kama hapa Jf ukipewa reply mbaya usichukie maana mtu hata humjui ila ingekua mtu unamuona yes unamind ila mtu humjui hakujui hata akiandika reply mbaya achana nayo we chukua zile unaona zina mchango kwako.
 
  • Thanks
Reactions: THT
Back
Top Bottom