Tuwe na utaratibu wa kupima afya ya akili kama kigezo cha mtu kupewa au kugombea uongozi hapa nchini

Kubwa lao Linagonga mukaka a.k.a munjenje na yule mvamizi wa vituo vya TV wale wote wagonga mmea tena kama siyo kitu cha njombe basi cha Jamaica
 
Kweli kabisa bora wawe wanapimwa maana hii nchi viongozi vichaa wanazidi kuongezeka kila kukicha .
Sasa wameanza kuzurura zurura huko Ulaya wakiunga mkono ushoga. Hii ni hatari kwa taifa maana mtu huyu ni chief whip kabisa.
 
Hili wazo nimekuww nalo kichwani mwangu kwa karibu miezi mitatu au minne sasa ila kadri siku zinavyoenda nazidi kupata msukumo wa kulileta hapa mtandaoni kama wazo au maoni yangu.

Nafikiri wakati umefika tujiridhishe na historia ya afya ya akili ya watu wanaotaka kushika uongozi katika nafasi mbalimbali hasa kama watu hao waliwahi kutumia madawa ya kulevya yanayoharibu au kuathiri akili za binadamu.

Vile vile kujua historia ya familia wanazotoka kama baadhi ya ndugu zake huwa wana matatizo ya afya ya akili ya kurithi n.k.

Kwa mfano kama inawezekana vipimo vya kitaalamu kuthibitisha mtu fulani aliwahi tumia bangi kilpindi fulani katika maisha yake basi mtu huyo azuiwe na sheria ikiwezekana hata na katiba kugombea au kuteuliwa katika nafasi yoyote ile ya uongozi.

Hata serikalini mtu unapotaka kuajiriwa huwa unatakiwa kuchunguzwa afya yako(medical examination) ambapo daktari hukufanyia vipomo na kukujazia form maalumu kuelezea juu ya afya yako tena huwa inasisitizwa vipimo vifanyike katika hospitali za serikali.

Binafsi napendekeza uchunguzi huu wa afya uhusishe mpaka afya ya akili ya mtu kwa wale wanaogombea uongozi au kwa wale wanaoteuliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi hapa nchini.

kwa kila anaegombea uongozi kuwe na form maalumu ya siri(separate form) kwa ajili ya madakari kujaza taarifa za siri za mgombea kuhusu afya yake ya akili na iwe ni kosa la jinai(na si la kiimadili tu) kwa dakari au mtu mwingine yoyote kutoa siri za mgonjwa.

Hili ni pendekezo langu mimi kama mimi ila wadau mbalimbali wakiwemo madaktari wa afya ya akili wanaweza kuliboresha but all in all something must be done.

Ni ushauri tu kwa nia njema.
 
Awamu hii inaongoza kuwa na viongozi vichaa. Mwingine naambiwa huko Singida amemtwanga risasi raia kichwani.

Wengi wa safari hii wamechukuliwa kutoka kikosi kile cha mauaji cha green. Damu za waliowaua zamani zinawalilia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
100% naunga mkono upimaji wa Afya ya Akili kwa wagombea wa nafasi za juu za maamuzi!
 
Hili wazo nimekuww nalo kichwani mwangu kwa karibu miezi mitatu au minne sasa ila kadri siku zinavyoenda nazidi kupata msukumo wa kulileta hapa mtandaoni kama wazo au maoni yangu.

Nafikiri wakati umefika tujiridhishe na historia ya afya ya akili ya watu wanaotaka kushika uongozi katika nafasi mbalimbali hasa kama watu hao waliwahi kutumia madawa ya kulevya yanayoharibu au kuathiri akili za binadamu.

Vile vile kujua historia ya familia wanazotoka kama baadhi ya ndugu zake huwa wana matatizo ya afya ya akili ya kurithi n.k.

Kwa mfano kama inawezekana vipimo vya kitaalamu kuthibitisha mtu fulani aliwahi tumia bangi kilpindi fulani katika maisha yake basi mtu huyo azuiwe na sheria ikiwezekana hata na katiba kugombea au kuteuliwa katika nafasi yoyote ile ya uongozi.

Hata serikalini mtu unapotaka kuajiriwa huwa unatakiwa kuchunguzwa afya yako(medical examination) ambapo daktari hukufanyia vipomo na kukujazia form maalumu kuelezea juu ya afya yako tena huwa inasisitizwa vipimo vifanyike katika hospitali za serikali.

Binafsi napendekeza uchunguzi huu wa afya uhusishe mpaka afya ya akili ya mtu kwa wale wanaogombea uongozi au kwa wale wanaoteuliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi hapa nchini.

kwa kila anaegombea uongozi kuwe na form maalumu ya siri(separate form) kwa ajili ya madakari kujaza taarifa za siri za mgombea kuhusu afya yake ya akili na iwe ni kosa la jinai(na si la kiimadili tu) kwa dakari au mtu mwingine yoyote kutoa siri za mgonjwa.

Hili ni pendekezo langu mimi kama mimi ila wadau mbalimbali wakiwemo madaktari wa afya ya akili wanaweza kuliboresha but all in all something must be done.

Ni ushauri tu kwa nia njema.
Naona Mzee wa salary tangu uondoke magogoni unahangaika sana kumharibia jiwe, lakini ni karata zako hukuchanga vema kutuachia nyapala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom