Tuwe na taratibu ya kunywa dawa za minyoo kila baada ya miezi 3

Siyo kunywa dawa, utakunywaje dawa bila kupima? Sema hivi kila baada ya miezi mitatu watu wapime waangalie km kuna hilo tatizo!!!!!
Mkuu minyoo iko kwa wingi na husababishwa na baadhi ya vyakula tunavyokula.
Pia hali zetu za usafi bado duni hivyo kujikinga nayo kwa kunywa dawa ni muhimu si lazima kupima bhana. Mbona shuleni watoto hugaiwa tu bila kupima.
 
Nilikwenda hospital moja nikataka hizo dawa wakakataa kunipa wakidai nimejuaje nina minyoo, wakasema sharti nipime kwanza ndipo wanipatie dozi inayofaa kama nitakuwa nayo au la!
Kwani hivyo vipimo ni bure? kama sio bure nenda maduka ya dawa utapata dozi uitakayo tu!..
 
Hatari sana mkuu jitahidi unywe dawa miaka kumi na tano ni mingi sana yaan hapo minyoo imekua mpaka kufikia size ya chatu
Hivi nina minyoo ambayo nimetumia Mabendazole lakini bado sijaona nafuu.

Ila kinacho kera ni sehemu ya haja kubwa kuna kitu kina chezacheza /kutekenya. Hivi huo ni mnyoo gani
 
Hivi nina minyoo ambayo nimetumia Mabendazole lakini bado sijaona nafuu.

Ila kinacho kera ni sehemu ya haja kubwa kuna kitu kina chezacheza /kutekenya. Hivi huo ni mnyoo gani
Mkuu ukifanya masihala kuna siku itaanza kutoka utashangaa inatokea kwenye suruari.
Halafu ilivyo na sifa inawasha sana mbele za watu haaaa utageuka huku na huko kutafuta maficho ujikune.
Wahi wataalam watakupa ushauri wa kina.
 
Ahsante Mkuu kwa ushauri wako. Ila bado sijapata Dawa mujarabu.

Ndio maana nimefikia huku Japo nipate ushauri wa kuwadhibiti
 
Back
Top Bottom