Tuwe na taratibu ya kunywa dawa za minyoo kila baada ya miezi 3

NUCLEAR BOMB

JF-Expert Member
Jan 23, 2017
342
323
Wakuu habarini,

Mimi siyo mtaalamu wa AFYA bali ni mdau tu wa Afya. Leo napenda kuwakumbusha ndugu zangu tuwe na utaratibu wa kunywa dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu.

Ahsanteni natumai wataalamu wataongezea zaidi kuhusu madhara ya minyoo mwilini.

Naomba kuwasilisha.
 
Asante mkuu kweli aisei niliwahi ambiwa na dokta baada ya kuwa na ngozi dhaifu akasema kanywe dawa za minnyoo nikapata positive results!
Minnyoo inatumia nutrients nyingi za kujenga mwili.
 
Daa kweli aisee,jana tu nimetoka kupiga dozi ya aloe vera ya kutoa minyoo,minyoo ina madhara mengi sana kiafya hasa kwa watoto wadogo
 
Nilikwenda hospital moja nikataka hizo dawa wakakataa kunipa wakidai nimejuaje nina minyoo, wakasema sharti nipime kwanza ndipo wanipatie dozi inayofaa kama nitakuwa nayo au la!
 
Nasikia mayai ya minyoo yanaweza ikaingia kichwani yakakupa utaahira. Watu wengine wanadumaa na kuwa na matumbo Makubwa, kusikia njaa mara kwa mara na wengine ukutokusikia hamu ya kula ikijaa tumboni.
 
nini adhari ya kutokunywa?

ni vyakula gani husababisha minyoo?

ni vyakula gan au dawa gani za asili hupunguza uwepo wa minyoo?

kuna faida ya minyoo?
 
Nasikia mayai ya minyoo yanaweza ikaingia kichwani yakakupa utaahira. Watu wengine wanadumaa na kuwa na matumbo Makubwa, kusikia njaa mara kwa mara na wengine ukutokusikia hamu ya kula ikijaa tumboni.
hao minyoo wanaishi tumboni lakini wanatagia kichwani au wana njia ya kupeleka mayai kichwani??

wenye taaluma waje waelimishe juu ya hili jambo vinginevyo tutadanganyana sana humu
 
Mungu wangu!! yaani sikumbuki mara ya mwisho nilikunywa dawa za minyoo lini!! lakini inaweza ikawa imepita miaka hata kumi na tano....
 
Wakuu habarini,

Mimi siyo mtaalamu wa AFYA bali ni mdau tu wa Afya. Leo napenda kuwakumbusha ndugu zangu tuwe na utaratibu wa kunywa dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu.

Ahsanteni natumai wataalamu wataongezea zaidi kuhusu madhara ya minyoo mwilini.

Naomba kuwasilisha.
Siyo kunywa dawa, utakunywaje dawa bila kupima? Sema hivi kila baada ya miezi mitatu watu wapime waangalie km kuna hilo tatizo!!!!!
 
Back
Top Bottom