Tuwe makini tunaowapeleka wanawake zetu Bar

Tuwe makini tunaowapeleka wanawake zetu Bar

Bismack

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2018
Posts
387
Reaction score
496
Kwanza nimshukuru Mungu kwa kuniamsha salama pamoja na member wote wa JF mana bila nyinyi hamna raha yoyote humu ndani.

Jana wakati nimemaliza mishemishe zangu jioni nikasema ngoja nipitie kwenye Bar jirani ili nipate mbili za moto.

Nilipofika nikakuta viti vyote vimejaa ila kuna meza moja tu kakaa mrembo mmoja yuko peke yake nikamuuliza kama kuna mtu yupo kwenye hiki kiti kilichobaki? Akaniambia hamna nikamuomba nikae akaniambia kaa tu hamna shida.

Mwanaume nikaita mhudumu akaja, nikaagiza zangu mbili za moto baada ya dakika kama tano nikamuulza mbona uko peke yako au kuna mtu unamsubili? Akaniambia kunamtu namsubiri ila siyo boyfriend ni rafiki yangu tu nikamwambia poa.

Basi nikaona si mbaya nikamuomba namba, sasa ile tu anaanza kunitajia namba jamaa mwenyewe akafika ikabidi nizuge kama nachat na nikajifanya niko serious sana jamaa akanisalimia nikaitikia basi nikaendelea na kinywaji changu.

Nilichogundua usimwache mwanamke Bar hata dakika mbili kuna watu wanakuwepo wanakuchora tu ukiinuka basi wanatumia nafasi hiyohiyo kuomba namba tena ni mara chache mwanamke atakataa kutoa namba.

Ushauri wangu ni huo mana nishalifanyia uchunguzi hili, ila kwa wanofanya hii michezo wawe makini mana huchelewi kupigwa chupa ya kichwa kisa kuomba namba ya simu ya msichana/mke wa mtu.

Nawatakia Pasaka njema.
 
Sasa si umeambiwa sio mpenzi wake Bali ni rafiki yake?? Ungeendelea tu kuandika no bila papala yeyote ila halafu ungemcheki baadae.utakuwa umepoteza bahati yako kizembe kisa uoga.
 
Sasa si umeambiwa sio mpenzi wake Bali ni rafiki yake?? Ungeendelea tu kuandika no bila papala yeyote ila halafu ungemcheki baadae.utakuwa umepoteza bahati yako kizembe kisa uoga.
Hapana mkuu jamaa alivo fika walianza kushikana shikana na mabusu mwanana nikajua hapa nimekoswakoswa chupa.
 
Labda hiyo dada ni changudoa na jamaa alikua muosha lungu tu, so we ungechukua tu namba. Me kwa kweli naingia bar na mama kama kawaida coz ndio sehemu pekee napenda kutulia, kuhusu namba hiyo ni akili ya mwanamke mwenyewe.
 
Sasa ww unamzoesha mke wako mambo ya baa unatagemea nn, acha usaidiwe tu maana hujielewei
 
Back
Top Bottom