Mazungumzo baina ya
Preta na
Katavi yalichukua sura ngeni sana baada ya kutawaliwa na ukimya mwingi,ilikuwa kama kikao ambayo haikuwa na mwenyeketi na wahusika wote walikuwa kama bubu
Katavi akajikaza akakumbuka maneno ya aliyekuwa rafiki yake wa zamani aitwaye
watu8 kuwa "mwanaume lazima siku zote uwe na ujasiri",akiliza Katavi sikajinasua katika giza na kuanza kupata mwanga ndipo midomo ya Katavi ilipomwambia Preta,"Hivi unajua leo ni Ijumaa ,tunaweza kunywa bia moja moja?"ingawa Katavi bado alikuwa na ushamba wa jiji lakini alishawahi kwenda kunywa bia kwenye bar na rafiki yake
Arushaone ambaye ni jirani yake
Preta,kwa vile
Preta alizongwa na mawazo naye akajikuta akikubaliana na mawazo ya
Katavi,moja kwa moja wakaanza kuelekea baa,wakaangiza mishikaki huku wakipata Castle,kila mtu alikuwa hajanywa bia yapata wiki kama tatu kwahiyo bia ilikuwa inaonekana tamu na ujazo wa pombe ulikuwa unapungua kwa haraka,mara wakajikuta wapo bia ya pili huku wakitafuna mishikaki,mara chupa za zikabaki kavu wakaongeza zingine
Preta alianza kuwa na maneno ya kuvutia,Katavi alikuwa anachanganya stori ambazo zilihusu maisha yake ya tabu na mateso,Preta hakufurahishwa nazo na kuanza kuchomekea stori za mapenzi na kujadili mahusiano na wapenzi wao wa zamani.
................Excy nilikuwa nimekaa kwenye meza ya nyuma yao na kuona kila kilichoendelea,nilisikia kila kitu walichoongea maana walikuwa wanaongea kwa sauti ya juu,ila Preta na Katavi walionekana kwenye ulimwengu wa mapenzi yaliyorahisishwa na bia bila wao wenyewe kujitambua,gafla wakaanza kuelewa na yapata mida ya saa nne usiku,wakaanza kuelekea nyumbani kwa Preta,walipoingia ndani Preta alimkumbatia Katavi na kumwambia "Unajua mara ya kwanza nilipokuona kwenye basi nilikupenda ila ulipotapika nilikudharau ila mwenzio nilijawa na huruma ndo maana mpaka leo upo na mimi"halafu akamkumbatia tena,Katavi hakuamini.
..................Hisia za mapenzi zilizotawaliwa na pombe zikamjia,ila alijizuia
Preta akasikika akimwambia
Katavi sema kweli leo silali mwenyewe naogopa,twende chumbani kwako",katavi alikosa ujasiri maana alikuwa Nyumbani kwa Preta na pia akawaza kama atakataa labda Preta anaweza kufanya maamuzi ya ajabu kutokana na pombe,Katavi akamshika Preta kiuno,wakaelekea chumbani,wakakaa juu ya kitanda,Katavi akamvuta Preta polepole juu ya kitanda,akamlaza kifuani,Preta alijihisi kama kinda la ndege linalolishwa na mama yake,akamwambia Katavi kwa sauti ya upole,"mwenzio sema kweli nakupenda,nimejaribu kuficha hisia zangu ila nimeshindwa,"kisha akamwangalia Katavi machoni,kila moja aliona macho ya mwenzake yanavutia,wakapeana busu na kukumbatiana tena...........