Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,776
Reaction score
46,050
Kutofautiana kimawazo katika nchi ni jambo la afya. Haiwezekani sote tukawa na mtizamo mmoja. Hata watoto mapacha hutokea wakati wakatofautiana.

Kwa bahati mbaya kuna zama zimepita kwa kutofautiana tu pana watu wamekufa, wamepotezwa, wamejeruhiwa, wamedhulumiwa, na mengi ya namna hiyo.

Yaliyopita si ndwele bali kiungwana hayawezi kuachwa kuwa ndiyo ilikuwa malipo stahiki kwa wahanga wale.

Mungu bariki tumepata rubani mpya mwenye kuthamimi maridhiano kwa maneno na kwa vitendo. Rubani aliyedhamiria kutuleta pamoja. Makundi yote kwa ujumla yanamkubali na sasa taifa linakuja pamoja.

Hata hivyo kuna wanaoonekana kutopendezwa na hali hii yenye matumaini mapya. Wao wamedhamiria kwa hali na mali kutusambaratisha.

Hawalali. Kila uchao wanakuja na kila aina ya chokochoko, uzandiki, fitna, uongo, uzushi, na vya namna hiyo. Alimradi tu kututatiza sisi kama wananchi na pia kumtatiza mama.

Wanahangaika mno kuzitatiza agenda zake ikiwamo hata kujaribu kumfarakanisha tu kwa lolote na kwa yeyote.

Haieleweki hasa wanataka nini au hawataki nini. Haijulikani pia kuwa, hii ni kwa maslahi gani hasa.

Watu hawa wapo pia humu JF. Mada zao na mabandiko yao mbalimbali yakiwatambulisha hivyo.

Hii nchi ni ya watanzania wote, ambamo kuna wanachama wa vyama vyote wakiwamo pia wasiokuwa na vyama.

"Hivi wandugu, mkiwamo nyie akina Elitewge, kudadavuwa, Nigrastratat, joni, dugunde, Mulokozae na wenzenu wengine ambao kila uchao ni kutafuta fursa za kupalilia utengano tu, mna madhumuni au maslahi gani hasa?"

Hivi wandugu, "Kwa nini mmedhamiria yasiwepo maridhiano kabisa? Kwa nini ni nia yenu kuona watanzania hawa wakiwamo wa CCM na wa CHADEMA haitokei kabisa nafasi ya kukaribiana? Madhumuni yenu ni nini hasa?"

Hatuwezi sote kupigia chapuo kuwa na taifa lenye ustawi, haki na usawa kwa maslahi yetu, wanetu na hata kwa watoto wa watoto wetu?

Tuwakaribishe ndugu hawa kutusaidia kuwaelewa. Labda wakijieleza wenyewe tutawaelewa. Isije kuwa kila mtu labda ana mshangaa mwenziwe.
 
Kuwasikia ingependeza zaidi. Wana maslahi gani kuona Mama anafarakanishwa na yeyote na kwa lolote.

Au wana maslahi gani kuona watanzania wanafarakana au hata tu kuona CCM na Chadema hawakaribiani kwa sababu zozote hata kama ni za kijinga tu?
 
Namna pekee ya kupony majeraha tuliyo nayo ni serikali kuchukua hatua za kuchunguza na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria wote waliohusika na matendo ya mauaji na uvunjaji wa haki za binaadamu kipindi cha magufuri.

CHADEMA wasije kubali maneno yasiyo na nyama mpaka hatua hizo zimechukuliwa na wale waliohusika kupewa adhabu stahiki.
 
Bavicha hao wanaotaka katiba mpya ikiwa ya zamani hawaijui
Wewe kilaza ndiyo huijui, laiti ungeijua na mapungufu yake usingeandika huu upumbavu wako. Nyie mnaomlalamikia Samia ndiyo mjue kuwa yeye ni Rais,na kutokana na Katiba hii hamuwezi kufanya lolote akiamua kuwashughulikia hamna cha kumfanya kwani Katiba hii inampa madaraka yanayokaribia madaraka ya Mungu.
 
Bavicha hao wanaotaka katiba mpya ikiwa ya zamani hawaijui

Mkuu hivi unayajua kuwa:

1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe?
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe?
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu?
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi?
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe?
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi?
7. Kuna rundo kubwa la vigogo wasio na tija na wasiolipa kodi wanaopata uhalali tokea katika katiba yenyewe?
8. Nk, nk.

Bado unadhani hayo ni ya bavicha tu na kuwa wao hata hawayajui hayo?

Bado hudhani kuwa yote ya namna hiyo yanapaswa kupatiwa ufumbuzi pasipo na kuchelewa sasa, kwa kuyashughulikia ipasavyo kwenye katiba mpya?
 
Maelezo mengi Ila sijayasoma kwa kuwa najua wewe ni zaidi ya mjinga
 
Back
Top Bottom