Tuwasimange mpaka waone aibu

Tuwasimange mpaka waone aibu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,193
Reaction score
829,147
Hakuna haja ya kuwachukulia sheria mkononi au hakuna haja ya kuwapeleka mbele ya sheria
Hawa wanafaa kusimangwa
Hawa wanafaa kusemwa
Hawa wanafaa kusutwa

Kule kwetu ukiikosea hatukupeleki kwa balozi wala kwa sungusungu
Tunaalika kigoma
Tunaalika tarumbeta
Tunashona sare ya vijora

Tunakufuata ulipo tangu mwanzo wa mtaa
Tunakusutaa wee mpaka ukonde
Tunakusimanga weee mpaka uone aibu.. Tukimaliza hapo tunaondoka huku tukijisifu tumekukomesha kabisa na hutakaa urudie tena maovu yako!
Sio utamaduni wetu kuwajibishana na kuchukuliana hatua kali sana za kisheria kwakuwa tunaamini katika usemi wa wahenga KULA KWA UREFU WA KAMBA Anayepitiliza kipimo akala akasaza akavimbiwa na kuanza kuharibu hali ya hewa huyu ndio wa kumuundia jopo la msuto.. Professionally maalum kwa kazi hiyo.. Na bajeti kabisa tunaandaa!

Swali la kizushi:
Hivi aibu inakaa sehemu gani ya mwili ili iweze kuonekana!?
Na vipi wale ambao hawajaumbwa na mshipa wa aibu?
Yaani kumbe kwenye mwili wa binadamu kuna kiungio kinachoitwa MSHIPA WA AIBU Ambacho kuna baadhi hawana! Je huo ni ulemavu!?
Aliyeturoga katuweza sana
1774941740872.jpg
 
mkiambiwa kwamba islamic sharia republic iko in final statges msikiri ni utani, its real and its happening na ndiyo maana taasisi zote zilizopo kuanzia bunge, mahakama, wizara zote, takukuru, na mifumo yetu yote tuliozoea ambayo wao wanaita ''mfumo Kristo'' haina kazi (tena), huo msemo msiuchukulie poa umebeba maana kubwa sana, its over guys ...
 
Back
Top Bottom