Tuwashauri Azam TV - Sinema Zetu

Tella Mande

JF-Expert Member
Jun 2, 2018
494
673
Mimi ni mpenzi wa Azam Tv kwa ujumla wake ila yapo mambo ambayo nadhani bado ipo fursa ya kuboresha zaidi.

Kwanza niwashukuru Azam TV kwa kuboresha movie za ndani.

1. Waboreshe wigo wa kuchagua sinema za kuonyesha kwa kuzipa nafasi movie zilizogizwa katika mazingira ya mikoani. Kwa sasa sinema nyingi zimeigizwa maeneo ya Dar, pwani na baadhi ya sehemu ya morogoro. Mtu asipokuwa makini atadhani nchi nzima ni kama uzaramoni na mila na desturi zetu ni za kizaramo.

2. Waongozaji movie wahimizwe kutoka mazingira haya haya wajiongeze. Wabadili pia theme mapenziiii na uchawi, kweli?

3. Wanapoandika jina la sinema waandike pia ka short story kuelezea inahusu nini na ya mwaka gani.

4. Ubora wa picha uzingatiwe...majumbani tuna vitu HD, UHD nk...tupeni picha bora...

Ongeza na wewe cha kwako cha kujenga....

Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom