tuwapeni pole CCM kwa msiba huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

tuwapeni pole CCM kwa msiba huu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, Oct 22, 2007.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kada wa CCM Arusha afariki dunia

  Na Magesa Magesa, Arusha

  ALIYEKUWA Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Muleba mkoani Kagera,Bw. Olgenus Mrengus (59) amefariki dunia kutokana na maradhi ya moyo, ini na kisukari.

  Marehemu Mrengus ambaye kwa sasa alikuwa Ofisa wa CCM mkoani Arusha alifariki juzi saa 5 mchana katika Hospitali ya Rufani ya KCMC mjini Moshi baada ya kufikishwa akitokea hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru alikokuwa amelazwa kwa siku mbili, akipatiwa matibabu .

  Habari kutoka ndani ya CCM mkoani Arusha, marehemu Mrengusi ambaye kabla ya kuhamishiwa wilayani Muleba alikuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha kwa muda mrefu, amekuwa akisumbuliwa na maradhi hayo ambayo yalisababisha kurejeshwa Arusha ili awe karibu na Hospitali ya KCMC kwa ajili ya matibabu .

  Akithibitisha kifo hicho Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli Bw. Allan Kingazi,alisema marehemu alizidiwa ghafla siku mbili kabla akiwa nyumbani kwake eneo la Olasiti wilayani Arumeru, ndipo alipelekwa hospital ya mkoa ya Mount Meru

  Alisema kuwa walimhamishia KCMC baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya ambapo alifikishwa saa 3.45 na kufariki saa 5.15 akiwa anapatiwa matibabu na madaktrai bingwa .

  "Tulimchukua jana ( juzi) asubuhi marehemu na kumpeleka KCMC . Tulifika saa 3.45 alifariki saa 5.15 akipatiwa huduma, "alisema Bw.Kingazi

  Alisema kuwa marehemu Mrengusi ameacha mke na watoto na atazikwa nyumbani kwao kijiji cha Kidia Old Moshi mkoani Kilimanjaro siku itayopangwa

  Mwisho....
  http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=4234
   
Loading...