tuwapeni pole CCM kwa msiba huu

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Kada wa CCM Arusha afariki dunia

Na Magesa Magesa, Arusha

ALIYEKUWA Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Muleba mkoani Kagera,Bw. Olgenus Mrengus (59) amefariki dunia kutokana na maradhi ya moyo, ini na kisukari.

Marehemu Mrengus ambaye kwa sasa alikuwa Ofisa wa CCM mkoani Arusha alifariki juzi saa 5 mchana katika Hospitali ya Rufani ya KCMC mjini Moshi baada ya kufikishwa akitokea hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru alikokuwa amelazwa kwa siku mbili, akipatiwa matibabu .

Habari kutoka ndani ya CCM mkoani Arusha, marehemu Mrengusi ambaye kabla ya kuhamishiwa wilayani Muleba alikuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha kwa muda mrefu, amekuwa akisumbuliwa na maradhi hayo ambayo yalisababisha kurejeshwa Arusha ili awe karibu na Hospitali ya KCMC kwa ajili ya matibabu .

Akithibitisha kifo hicho Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli Bw. Allan Kingazi,alisema marehemu alizidiwa ghafla siku mbili kabla akiwa nyumbani kwake eneo la Olasiti wilayani Arumeru, ndipo alipelekwa hospital ya mkoa ya Mount Meru

Alisema kuwa walimhamishia KCMC baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya ambapo alifikishwa saa 3.45 na kufariki saa 5.15 akiwa anapatiwa matibabu na madaktrai bingwa .

"Tulimchukua jana ( juzi) asubuhi marehemu na kumpeleka KCMC . Tulifika saa 3.45 alifariki saa 5.15 akipatiwa huduma, "alisema Bw.Kingazi

Alisema kuwa marehemu Mrengusi ameacha mke na watoto na atazikwa nyumbani kwao kijiji cha Kidia Old Moshi mkoani Kilimanjaro siku itayopangwa

Mwisho....
http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=4234
 
RIP Kiongozi wa CCM, kifo hakichagui uwe kiongozi wa CCM au upinzani........

Lakini kwa Bahati mbaya hao wenzetu ndiyo huwa wanafanya ubaguzi hata katika hali ya shida!

Refer watu waliokuwa wamevaa T/Shirt za PRAY FOR LISSU, walikamatwa na Jeshi letu la Polisi!
 
Hivi saizi jf hakuna habari mpya hadi muanze kutafutiza habari za mwaka 2007
 
Kifo pekee ndio kinaitendea haki kauli ta kutokubaguana.

Huku kwingine tunadanganyana tu. Mbaya zaidi wengine wanaleta siasa kwenye majanga na vifo vya wengine.

Pole kwa wafiwa.
 
Back
Top Bottom