Tuwapende Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwapende Polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jan 13, 2011.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Naona wengi mnapotea na kupoteza muelekeo wa kisiasa ,jeshi la polisi ni kitengo au ni chombo cha dola,sasa inapotokea migongano na raia kunakuwa na mivutano.Hivyo napenda wengi wenu mfahamu kuwa polisi wetu hawa wanaotumika kulinda amani ni watu walio masikini sana sana pengine kuliko hata raia wa kawaida,hilo napenda mulielewe kiundani kabisa.

  Polisi kama waajiriwa wanapokea kazi kutoka kwa wakubwa wao na pia zipo sheria na maadili katika utendaji wa kazi zao kwa vile zinahusisha mambo ya silaha ,hivyo katika kutekeleza utumiaji wa silaha sidhani kama wanakurupuka tu na kuanza kufyetulia watu risasi za moto au za baridi ni lazima kutakuwa na wahusika ambao ndio wanaoamrisha na wanapotoa amri ni lazima ifuatwe kama hukufuata unaweza ukachezea risasi.

  Hivyo si busara kuwalaumu polisi na kuwachanganya wote kuwa wametenda kosa itakuwa hatuwatendei haki,lawama na vifijo vielekezwe kwa wakubwa wakiwemo waziri wa Ulinzi waziri wa mambo ya ndani ,mkuu wa polisi kwa nchi nzima,mkuu wa polisi mkoa,mkuu wa polisi wilaya na aliewaongoza polisi katika tukio.Hapa itakuwa tunawatendea haki na vilevile tunaweza kufaidika nao hadi kumpata aliefyetua risasi kwa jina lake natumai nimeeleweka.Hii iliwezekana Pemba alietumia risasi na kuuwa alijulikana kwa jina na alihamishwa Unguja kwa vile tayari alijulikana alinadiwa mwizi nae kumfika mauti.

  Sasa kama Wapemba ingekuwa wanawachukia polisi wasingeweza kupata data za ndani ya kundi la polisi ,hapa panahitaji maingiliano ya karibu na wenzetu hawa polisi ambao joto la maisha nalo linawapata.Natumai kabisa hamkosi baadhi yetu mnaishi na ndugu zetu hawa wa kipolisi mitaani na mnazungumza nao na mnafurahi nao kwa kila kitu na si hasha kama nao ni wapenzi wa vyama vyetu hivi vya upinzani,hivyo ni kudumisha kiunganisho hicho ili tufanikiwe mradi wetu.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hilo neno pia...
  Lakini samaki mmoja akioza wote wameoza!
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Usemi huo umeshatenguka na hauna tena ukweli,nilienda ziwa victoria pale Nansio ukerewe nikaona kuna samaki wameoza na karibu yake nikaona samaki wengine wazima wanamla yule alieoza ,upoo na umeelewa kwa kina huo usemi.
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  sawa lakini ni vingumu sana hasa kwasasa hivi hata marafiki zangu mapolisi nisingependa kuwaona, kuna vitu huwa wana vifanya kwa kupokea amri lkn kuna vingine huwa wanafanya kwa maamzi yao, kwenye picha hizo chini ukiangalia kwa makini utaona jamaa wawili walikuwa wamepakizana wakikimbia mabomu wakasimamishwa wakaulizwa mnaenda wapi wakasema tunaenda nyumbani walichezea kibano na wakawekwa ndani na kesho yake mahakamani kwa kosa wakijumlishwa na akina dr slaa, Mbowe, nk sasa swali langu kwako kama ungekuwa wewe au ndungu yako kafanyiwa hivyo ungewapenda polisi au unasema tu kwa sababu hayajakukuta
   

  Attached Files:

 5. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Mwiba ana Point ila naona wana JF mnaisoma hii thread kichwakichwa hebu msomeni vizuri mtamuelewa mkakati anaouelezea unafaa kufanyiwa kazi
   
Loading...