Tuwape mimba Wachumba zetu jamani

DissDotCom

JF-Expert Member
Mar 31, 2014
395
268
Habari za muda mrefu wakuu wakazi.

Leo ningependa kushare jambo moja muhimu hasa kwa wanaume wenzangu, unajua kumbe sisi vijana wakiume tunapochelewa kuoa au kupata watoto huwa inawakwaza sana wazazi wetu.

Hii imenitokea mimi binafsi na nimeshuhudia, kwanza nilipanga nisizae nje hadi nifunge ndoa na ili nilipanga kuoa hadi nitakapoona nimejitosheleza kimaisha I mean niwe na kila kitu nyumba, biashara na gari.

Lakini kutokana na kuwa Mungu hajalia vyote kutimia kwa wakati basi nimejikuta nachelewa sana kuzaa nikisubilia hadi ndoa, kumbe nyumbani wazazi wangu wanasubiria hatma yangu lakini wanashindwa namna ya kuniambia, mbaya zaidi imetokea mdogo wangu ambaye nimemzidi miaka kadhaa amempa mimba binti na ameshajifungua na hii imemfanya yule dogo kuheshimika sana nyumbani.

Kimoyomoyo nikasema ngoja nifanye maamuzi magumu bahati nzuri kuna binti mpooolee akajitokeza nikamfata naye akanitunuku basi Mungu si Athumani mara kibendi, nikawaza hapa simwambii mtu hadi ajifungue, nikasubiri ilipofika miezi 8 nikaenda kuwaambia nyumbani. Huwezi amini walishangilia hadi watoto wadogo ambao wapo shule ya msingi huku dogo mmoja akisema afadhali kaka umetuletee mtoto maana tulikua tunajiuliza kulikoni?

Na wazazi nao wakaniambia ulikua unasubiri nini muda wote, hapo ndio nikawaza kumbe muda wote walikua wananijadili.

KIJANA WAKIUME KAMA UMEONA UMRI UNAENDA MAMBO HAYAENDI CHA MSINGI TAFUTA BINTI MKAPIME AFYA KISHA MPACHIKE MIMBA, FAMILIA NZIMA ITAKUSHANGILIA
 
Unazaa ili kuwaridhisha wazazi au unazaa kwa sababu upo tiyari
 

Similar Discussions

14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom